UKOO WA MALEKO.

– Maleko ni ukoo maarufu wa wachagga wanaopatikana zaidi maeneo ya mashariki ya kati ya Uchagga, Kilimanjaro. Ukoo wa Maleko wengi ni watu makini na wasomi sana na wanaofanya vizuri sana katika nyanja mbalimbali katika maisha hasa taaluma na biashara katika taasisi za umma, taasisi binafsi na kwenye taasisi za kimataifa.

– Kutoka kwenye historia ukoo wa Maleko unafahamika kwamba ni tawi la uliokuwa ukoo mkubwa sana, mashuhuri sana na maarufu sana katika Uchagga, Kilimanjaro yote ukoo wa Mboro. Ukoo huu mama wa Mboro ulikuwa na makazi yake ya kudumu katika kijiji cha Lyamrakana, Marangu kabla haujazidiwa ujanja na akili na ukoo wa Lyimo ambao walifanikiwa kuwaangusha na kisha baadaye ukaja kusambaratika na kutengeneza matawi mengi sana ya ukoo huu kila mahali na karibu kila kijiji cha Uchagga, Kilimanjaro.

– Tawi la ukoo wa Maleko lililotokea kwenye ukoo mama ni kati ya matawi ambayo hayakwenda mbali sana na chimbuko kwani wengi waliteremka na kuweka makazi kwa chini yake kidogo katika kijiji cha Sembeti, Marangu. Inasemekana kwamba kitongoji cha Kirefure katika kijiji cha Sembeti ndio kilifanywa kuwa ndio eneo takatifu zaidi la kuabudiwa na eneo muhimu zaidi la tawi hili la wakina Maleko ambao waliteremka kutoka juu kidogo katika kijiji cha Lyamrakana. Tawi lingine lililotokea katika ukoo huo lililo karibu sana na ukoo wa Maleko katika eneo hili ni ukoo wa Kipokola.

– Ukoo huu wa Maleko walisambaa na kuelekea upande wa mashariki zaidi pia huko Mamba na kwingineko. Hivyo tawi la ukoo wa Maleko waliendelea kuongezeka na kusambaa zaidi na wanapatikana kwenye vijiji kadhaa hususan maeneo haya haya ya mashariki ya karibu na mashariki ya kati ya Uchagga, Kilimanjaro.

– Ukoo wa Maleko unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Arisi, Marangu.

– Hivyo ukoo wa Maleko unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Lyamrakana, Marangu.

– Ukoo wa Maleko unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Sembeti, Marangu.

– Ukoo wa Maleko unapatikana kwa uchache sana katika kijiji cha Samanga, Marangu.

– Ukoo wa Maleko unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Mkolowony, Mamba.

– Ukoo wa Maleko unapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Kir’ia, Mamba.

– Ukoo wa Maleko unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Kimbogho, Mamba.

– Ukoo wa Maleko unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Kimangara, Mamba.

Ukoo Maleko ukiwa umetokea kwenye moja ya koo mashuhuri sana na wenye nguvu sana katika historia ya wachagga, Kilimanjaro kuna mengi yanayohusishwa nao. Tunahitaji kupata taarifa zaidi ambazo zitaendelea kutufungua sana kuhusu ukoo huu. Tutaweza pia kuongeza kwenye maktaba ya maudhui ya ukoo huu na jamii nzima ya wachagga, hivyo tunahitaji taarifa hizi muhimu.

Karibu kwa mchango zaidi wa Mawazo kuhusu ukoo wa Maleko.

1. Je, unafahamu nini kuhusiana na ukoo wa Maleko?

2. Unafikiri ni kijiji gani ambacho kimesahaulika kutajwa lakini kuna ukoo wa Maleko?

3. Kijijini kwenu kuna ukoo wa Maleko?

4. Kama wewe ni wa ukoo wa Maleko una nini cha kutuambia kuhusu ukoo wenu?

5. Huwa mna maadhimisho yoyote au sherehe za ukoo mwezi gani?

6. Wewe ni Maleko wa kutokea kijiji gani?

7. Bado kuna ushirikiano wowote katika matukio mbalimbali muhimu na ndugu zenu wengine wa matawi ya ukoo wa Maleko kutoka maeneo mengine ya Uchaggani?

8. Ni tabia gani unazozifahamu za wachagga wa ukoo wa Maleko?

9. Wanawake wa ukoo wa Maleko huitwaje, na kwa nini?

10. Una rafiki yako yeyote wa kutokea kwenye ukoo wa Maleko?

11. Ni watu gani mashuhuri unaowafahamu kutoka kwenye ukoo wa Maleko?

12. Kuna mnyama yeyote ambaye labda ni mwiko kuliwa na wachagga wa ukoo wa Maleko?

13. Kuna ukoo ambao hawaruhusiwi kuoana na Wako-Maleko kwa sababu zilizowahi kuwepo miaka ya zamani au nyingine zozote?

Karibu kwa Mchango zaidi au maswali.

Ahsanteni.

Kesho tutaendelea na ukoo mwingine.

www.wachagga.com

Urithi Wetu Wachagga (Facebook).

You may also like...

Popular Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *