– Koka ni ukoo wa wachagga wanaopatikana katika eneo la katikati ya ukanda wa mashariki ya kati ya Uchagga, Kilimanjaro. Ukoo wa Koka sio mkubwa sana lakini ni ukoo wenye wasomi wengi na wajasiriamali wakubwa na hata vijiji wanavyotokea kwa sehemu kubwa vimepiga hatua kubwa kimaendeleo.
– Ukoo wa Koka ni sehemu ya koo ambazo zamani ziliweza kutoa wafua vyuma hodari ambao mpaka leo bado fani hiyo inaendelea sambamba na koo nyingine za wafua vyuma kama vile Makundi, Kiria, Malisa, Chuwa, Shayo, Ngowi n.k. katika maeneo mengine ya Uchagga, Kilimanjaro.
– Ukoo wa Koka ambao pengine chimbuko lake ni katika kijiji cha Komakundi, Mamba umeendelea kukua na kusambaa zaidi katika maeneo mengine ya vijiji vya eneo la ukanda wa mashariki ya kati ya Uchagga, Kilimanjaro.
– Ukoo wa Koka unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Lyamrakana, Marangu.
– Ukoo wa Koka unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Komakundi, Mamba.
– Ukoo wa Koka unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Mkolowony, Mamba.
Ukoo wa Koka ni ukoo wenye watu wengi na wasomi wengi pia na watu wengi makini na wenye umoja na mshikamano wanaofanya vizuri katika maeneo mbalimbali. Lakini huu ni ukoo ambao licha ya kuwa na wasomi wengi bado hakuna maudhui mengi yaliyoandikwa kuhusu ukoo huu. Tunahitaji kufahamu mengi zaidi kuhusu ukoo wa Koka na namna ulivyotengeneza matawi yake katika maeneo ya vijiji mbalimbali vya Uchagga, Kilimanjaro hasa katika eneo la ukanda wa mashariki ya kati, ili kuhifadhi maudhui mengi zaidi katika maktaba ya ukoo huu na jamii ya wachagga kwa ujumla. Tunahitaji kuhifadhi taarifa na maudhui ya ukoo wa Koka katika maktaba za mitandaoni na maktaba halisi pia kwa faida ya kizazi cha sasa na kinachokuja kujitambua na kujijengea kujiamini zaidi kuelekea kufanya makubwa kwenye maisha katika ngazi ya mtu mmoja mmoja kwenye ukoo, kwenye ngazi ya ukoo na jamii nzima ya wachagga kwa ujumla.
Karibu kwa Mchango zaidi wa mawazo na taarifa kuhusu ukoo wa Koka.
1. Je, unafahamu nini kuhusiana na ukoo wa Koka.
2. Unafikiri ni kijiji gani ambacho kimesahaulika kutajwa lakini kuna ukoo wa Koka.
3. Kijijini kwenu kuna ukoo wa Koka.
4. Kama wewe ni wa ukoo wa Koka una nini cha kutuambia kuhusu ukoo wenu?
5. Huwa mna maadhimisho yoyote au sherehe za ukoo mwezi gani?
6. Wewe ni Koka wa kutokea kijiji gani?
7. Bado kuna ushirikiano wowote katika matukio mbalimbali muhimu na ndugu zenu wengine wa matawi ya ukoo wa Koka kutoka maeneo mengine ya Uchaggani?
8. Ni tabia gani unazozifahamu za wachagga wa ukoo wa Koka?
9. Wanawake wa ukoo wa Koka huitwaje, na kwa nini?
10. Una rafiki yako yeyote wa kutokea kwenye ukoo wa Koka?
11. Ni watu gani mashuhuri unaowafahamu kutoka kwenye ukoo wa Koka?
12. Kuna mnyama yeyote ambaye labda ni mwiko kuliwa na wachagga wa ukoo wa Koka?
13. Kuna ukoo ambao hawaruhusiwi kuoana na Wako-Koka kwa sababu zilizowahi kuwepo miaka ya zamani au nyingine zozote?
Karibu kwa Mchango zaidi au maswali.
Ahsanteni.
Wiki ijayo tutaendelea na ukoo mwingine.
Urithi Wetu Wachagga (Facebook).
urithiwetuwachagga@gmail.com
Whatsapp +255 754 584 270