– Mremi ni ukoo wa wachagga wenye umaarufu kiasi unaopatikana kwa wingi zaidi katika ukanda wa mwishoni mwa mashariki ya kati ya Uchagga na mwanzoni mwa ukanda wa mashariki ya mbali ya Uchagga, Kilimanjaro. Ni ukoo wenye watu mbalimbali makini wanaofanya vizuri sana katika maeneo mbalimbali hasa biashara na ujasiriamali. – Kutoka kwenye historia Mremi …
UKOO WA MKENDA.
– Mkenda ni ukoo wa wachagga wanaopatikana kwa wingi zaidi katika ukanda wa mashariki ya mbali ya Uchagga, Kilimanjaro. Huu ni ukoo wenye chimbuko lake zaidi katika eneo la Mashati, Rombo ambao umekuwa na watu wengi mashuhuri katika historia. – Ukoo wa Mkenda ni ukoo wenye watu wanaofanya vizuri katika nyanja mbalimbali kuanzia biashara na …
Mfahamu ELIFURAHA NDESAMBURO URIO MAREALLE.
– Elifuraha alizaliwa huko Mwika, Moshi, Kilimanjaro mwaka 1929. – Alisoma katika shule ya Sekondari ya wasichana Ashira ambapo baadaye alikuja pia kufundisha tena kama mwalimu katika shule hiyo. – Mwaka 1955 Elifuraha alikuwa mmoja kati ya wanawake watatu wa kwanza kuwa wabunge Tanganyika, yeye peke yake akiwa ndiye mwafrika. Hivyo ni mwanamke wa kwanza …
Habari Ndugu Wana-Urithi Wetu Wachagga.
Leo Tunafunga Mwaka 2023 na Kwenda Kuuanza Mwaka Mpya wa 2024. Kwa Muda Mrefu Tumekuwa Tunaweka Hapa Makala Mbalimbali za Kuelimisha na Nyingine za Kuburudisha. Leo Kabla Ya Kuufunga Mwaka Huu wa 2023 Tungependa Kupata Mrejesho na Maoni Yako Juu Ya Mambo Mbalimbali. 1. Nini Kikubwa Ulichojifunza Ambacho Hukuwa Unafahamu Kabla? 2. Nini Kilikuvutia Zaidi …
SALAMU ZA SIKU YA WACHAGGA, (HAPPY CHAGGA’S DAY TO Y’ALL).
– Leo Tarehe 10/Novemba Ndio Siku Ya Wachagga, “Chagga’s Day”. – Ni Siku Maalum Kwa Wachagga Wote Waliopo Mijini na Vijijini, Ndani na Nje Ya Kilimanjaro na Ndani na Nje Ya Nchi Pia Kukumbuka Siku Ambayo Watangulizi Wetu Waliiazimia Siku Hii Kama Siku Maalum Ya Kupumzika na Kusherehekea Maendeleo Ya Wachagga. – Ni Siku Kubwa …
UCHAMBUZI WA KITABU. – SEHEMU YA 11.
*Maisha Ya Mchagga Hapa Duniani Na Ahera” By Mangi Petro Itosi Marealle* Uchambuzi by Mary Assenga. USAWI (UCHAWI) KWA WACHAGGA. -Katika nchi ya Uchagga tuliogopa sana “usawi” (uchawi) toka zamani sana. Huu uchawi ulitisha watu wote, wakubwa kwa wadogo, waume kwa wake, watoto mpaka Wamangi. Ulitisha kuliko magonjwa ya kifua kikuu na ndui. Kwani mtu …
UCHAMBUZI WA KITABU. – SEHEMU YA 10.
*Maisha Ya Mchagga Hapa Duniani Na Ahera” By Mangi Petro Itosi Marealle* Uchambuzi by Mary Assenga. “MIZIMU” -Wachagga zamani waliamini na kutambikia mizimu, yaani watu wao walio marehemu. Waliamini mtu akishakufa bado alikwenda kuishi tena kule kuzimuni, lakini si kwa mwili huu tulio nao. Wachagga walisadiki kuwa hawa mizimu hula na kunywa, na kuweza kuja …
UCHAMBUZI WA KITABU. – SEHEMU YA 9.
*Maisha Ya Mchagga Hapa Duniani Na Ahera” By Mangi Petro Itosi Marealle* Uchambuzi by Mary Assenga. IMANI YA WACHAGGA. “RUWA” -Wachagga huamini “Ruwa”(Mungu) kwamba ni Mkuu kupita mizimu yote wanayotambikia. Huyu Ruwa hasumbui wanadamu kwa sababu ndogondogo kama vile mizimu iwasumbuavyo ikiwa haikutambikiwa. Tambiko alilotolewa Ruwa ni tofauti na tambiko la mizimu kwa hali na …
UCHAMBUZI WA KITABU. – SEHEMU YA 8.
*Maisha Ya Mchagga Hapa Duniani Na Ahera” By Mangi Petro Itosi Marealle* Uchambuzi by Mary Assenga. MAZISHI YA WAMANGI. -Mangi walizikwa mchangani kama watu wengine, lakini kabla ya kuzikwa walitiwa ndani ya chombo cha mti uliochongwa ndani yake wazi kama mzinga wa nyuki mkubwa kama pipa. Kifo cha Mangi hapo zamani kilifichwa sana, pia siku …
UCHAMBUZI WA KITABU. – SEHEMU YA 7.
*Maisha Ya Mchagga Hapa Duniani Na Ahera” By Mangi Petro Itosi Marealle* Uchambuzi by Mary Assenga. KIFO NA MAZISHI YA WACHAGGA. -Mchagga yeyote alisemekana hawezi kufa kiurahisi isipokuwa kwa kukosea yeye mwenyewe, yaani ikiwa hakutimizi desturi za ukoo wake au kwa bahati mbaya akiugua na hivi huweza kufa upesi. Kwa hiyo mara auguapo humbidi kufikiri …