ENEO MAARUFU NA MASHUHURI LA ASILI YA WAFINYANZI LINALOKUMBWA NA CHANGAMOTO YA ULEVI.

ENEO MAARUFU NA MASHUHURI LA ASILI YA WAFINYANZI LINALOKUMBWA NA CHANGAMOTO YA ULEVI.

– KIJIJI/KATA YA NARUMU, MACHAME.

– Kijiji/Kata Ya Narumu Ni Eneo Lililopo Katika Tarafa Ya Machame, Katika Wilaya Ya Hai, Magharibi Ya Kilimanjaro. Narumu Kwa Upande wa Magharibi Imepakana na Kijiji cha Nshara, Machame Ikitenganishwa na Mto Weruweru na Upande wa Magharibi Ikipakana na Kijiji cha Manushi, Kibosho Ikitenganishwa na Mto Sere.

– Narumu Pamoja na Usseri, Rombo ni Maeneo Yaliyokuwa Mashuhuri Sana Zamani kwa Shughuli za Ufinyanzi Kilimanjaro. Vyungu na Vyombo na Vifaa Vyote Vinavyotokana na Shughuli za Ufinyanzi Vilivyokuwa Vinatumia na Wachagga Kilimanjaro Zamani Vilikuwa Vinatengenezwa Narumu na Usseri, Rombo.

– Narumu ni Eneo Lenye Hali Ya Hewa Nzuri Sana, Ardhi Yenye Rutuba Nyingi Inayostawisha Karibu Kila Aina Ya Mmea na Mazingira Yake Ya Asili ni Yenye Kuvutia Sana.

– Narumu ni Eneo Linalokuwa kwa Kasi Kimaendeleo na Linaloendelea Kujengeka na Limeendelea Zaidi Ukilinganisha na Jirani Zao Upande wa Mashariki Kijiji cha Manushi, Kibosho Kuvuka Mto Sere. Watu wa Narumu ni Wenye Kujituma Sana na Wenye Ari Kubwa Ya Maendeleo. – Changamoto Kubwa Ya Narumu ni Ulevi.

– Narumu ni Eneo Lenye Vilabu Vingi Vya Pombe, na Hata Sehemu Kubwa Ya Pombe Inayouzwa Vijiji Jirani Kama Nshara, Manushi, Lyamungo na Maeneo Ya Kusini Ya Machame kwa Ujumla Inatokea Narumu.

– Ukoo Mkubwa Zaidi Narumu ni Ukoo wa Kweka Ambao Upo Pia Maeneo Mengine Ya Machame Lakini Shughuli za Ufinyanzi Zilizoipatia Umaarufu na Umashuhuri Mkubwa Narumu Zamani Miongoni mwa Wachagga, Kilimanjaro Zimedorora.

Karibuni kwa Maoni.

KIJIJI CHA WAFINYANZI NARUMU
KIJIJI CHA WAFINYANZI NARUMU
KIJIJI CHA WAFINYANZI NARUMU
KIJIJI CHA WAFINYANZI NARUMU
KIJIJI CHA WAFINYANZI NARUMU
KIJIJI CHA WAFINYANZI NARUMU
KIJIJI CHA WAFINYANZI NARUMU
KIJIJI CHA WAFINYANZI NARUMU
KIJIJI CHA WAFINYANZI NARUMU
KIJIJI CHA WAFINYANZI NARUMU
KIJIJI CHA WAFINYANZI NARUMU
KIJIJI CHA WAFINYANZI NARUMU

Urithi Wetu Wachagga

urithiwetuwachagga@gmail.com

You may also like...

Popular Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *