UKOO WA MAMKWE.

– Mamkwe ni ukoo wa wachagga wanaopatikana katika eneo la ukanda wa mashariki ya kati ya Uchagga, Kilimanjaro. Huu ni ukoo usio na idadi kubwa ya watu lakini ukiwa pia umetoa watu wengi makini na wasomi katika nyanja mbalimbali. – Kutoka kwenye historia ukoo wa Mamkwe haujazungumzia sana na pia haujatajwa katika kitabu cha “Miaka …

UKOO WA KYARA/MAKYARA.

– Kyara/Makyara ni ukoo maarufu wa wachagga unaopatikana kuanzia ukanda wa maeneo ya katikati kuelekea ukanda wa mashariki ya kati ya Uchagga, Kilimanjaro. Huu ni ukoo wenye watu wengi wasomi wanaofanya vizuri sana katika fani mbalimbali kuanzia taaluma, biashara na ujasiriamali na katika taasisi mbalimbali za umma, taasisi binafsi na hata katika mashirika ya kimataifa. …

UKOO WA MAKYAO.

– Makyao ni ukoo wa wachagga wanaopatikana zaidi katika maeneo ya vijiji vya mashariki ya kati na kwa kiasi mashariki ya mbali ya Uchagga, Kilimanjaro. Ukoo wa Makyao ni ukoo uliopiga hatua kubwa kwa kuzalisha watu wengi wa vipaji mbalimbali na wasomi wa katika nyanja mbalimbali. Huu ni ukoo wenye watu wengi wanaofanya vizuri katika …