UKOO WA MAMKWE.

– Mamkwe ni ukoo wa wachagga wanaopatikana katika eneo la ukanda wa mashariki ya kati ya Uchagga, Kilimanjaro. Huu ni ukoo usio na idadi kubwa ya watu lakini ukiwa pia umetoa watu wengi makini na wasomi katika nyanja mbalimbali.

– Kutoka kwenye historia ukoo wa Mamkwe haujazungumzia sana na pia haujatajwa katika kitabu cha “Miaka 700 Ya Wachagga” lakini ni ukoo wenye umaarufu mkubwa katika eneo la katikati ya ukanda huu wa mashariki ya kati.

Wachagga wa ukoo Mamkwe wamesambaa na wanapatikana maeneo mbalimbali ndani na nje ya Kilimanjaro na hata nje ya nchi na wengi wao unaweza kukutana nao katika mashirika makubwa na katika taasisi za umma pia na wachache katika sekta binafsi kwenye biashara na ujasiriamali.

– Ukoo wa Mamkwe umesambaa kiasi katika ukanda na unapatikana kwenye vijiji kadhaa huku idadi yake ikizidi kuongezeka.

– Ukoo wa Mamkwe unapatikana kwa uchache katika kijiji cha Rauya, Marangu.

– Ukoo wa Mamkwe unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Arisi, Marangu.

– Ukoo wa Mamkwe unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Kokirie, Mamba.

– Ukoo wa Mamkwe unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Komakundi, Mamba.

– Ukoo wa Mamkwe unapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Mboni, Mamba.

– Ukoo wa Mamkwe unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Lekura, Mamba.

– Ukoo wa Mamkwe unapatikana katika kijiji cha Kimarango, Shokony, Mwika.

– Ukoo wa Mamkwe unapatikana katika kijiji cha Mawanda, Kata ya Mahida, Rombo.

Ukoo wa Mamkwe ni ukoo wenye wasomi wengi na watu wenye weledi mkubwa lakini lakini bado hakuna maudhui mengi yaliyoandikwa kuhusu ukoo huu, hivyo kuna maswali mengi ambayo hayajajibiki kuhusu ukoo wa Mamkwe. Tunahitaji kufahamu mengi zaidi kuhusu ukoo wa Mamkwe ili kuhifadhi maudhui mengi zaidi katika maktaba ya ukoo huu na jamii ya wachagga kwa ujumla. Tunahitaji kuhifadhi taarifa na maudhui katika maktaba za mitandaoni na maktaba halisi pia kwa faida ya kizazi cha sasa na kinachokuja kujitambua na kujijengea kujiamini zaidi kuelekea kufanya makubwa kwenye maisha katika ngazi ya mtu mmoja mmoja, ngazi ya ukoo na jamii nzima ya wachagga kwa ujumla.

Karibu kwa Mchango zaidi wa mawazo na taarifa kuhusu ukoo wa Mamkwe.

1. Je, unafahamu nini kuhusiana na ukoo wa Mamkwe?

2. Unafikiri ni kijiji gani ambacho kimesahaulika kutajwa lakini kuna ukoo wa Mamkwe?

3. Kijijini kwenu kuna ukoo wa Mamkwe?

4. Kama wewe ni wa ukoo wa Mamkwe una nini cha kutuambia kuhusu ukoo wenu?

5. Huwa mna maadhimisho yoyote au sherehe za ukoo mwezi gani?

6. Wewe ni Mamkwe wa kutokea kijiji gani?

7. Bado kuna ushirikiano wowote katika matukio mbalimbali muhimu na ndugu zenu wengine wa matawi ya ukoo wa Mamkwe kutoka maeneo mengine ya Uchaggani?

8. Ni tabia gani unazozifahamu za wachagga wa ukoo wa Mamkwe?

9. Wanawake wa ukoo wa Mamkwe huitwaje, na kwa nini?

10. Una rafiki yako yeyote wa kutokea kwenye ukoo wa Mamkwe?

11. Ni watu gani mashuhuri unaowafahamu kutoka kwenye ukoo wa Mamkwe?

12. Kuna mnyama yeyote ambaye labda ni mwiko kuliwa na wachagga wa ukoo wa Mamkwe?

13. Kuna ukoo ambao hawaruhusiwi kuoana na Wako-Mamkwe kwa sababu zilizowahi kuwepo miaka ya zamani au nyingine zozote?

Karibu kwa Mchango zaidi au maswali.

Ahsanteni.

Wiki ijayo tutaendelea na ukoo mwingine.

www.wachagga.com

Urithi Wetu Wachagga (Facebook).

urithiwetuwachagga@gmail.com

Whatsapp +255 754 584 270.

You may also like...

Popular Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *