MANGI MKUU THOMAS LENANA MAREALLE

Huyu Aliitwa MSHUMBUE(MPAKWA MAFUTA) AU MANGI THOMAS LENANA MAREALLE

Alikuwa Mangi Mkuu Wa Wachagga Kuanzia Januari 1952 Baada Ya Kushinda Uchaguzi Uliohusisha Wagombea 4. Uongozi Wake Kama Mangi Mkuu Ulikuwa Wa Mafanikio Sana Kwani Uchaggani Kulikuwa Na Maboresho Mengi Katika Elimu, Afya, Miundombinu Ya Maji, Njia Za Mawasiliano, Katika Chama Cha Ushirika Na Ujenzi Wa Shule Na Vyuo.

Kabla Ya Kuwa Mangi Mkuu Wa Wachagga Alikuwa Meneja Wa Programu Wa Dar es Salaam Broadcasting Station (DBS) Baada Ya Kutoka Masomoni Uingereza. Lakini Inasemekana Alipuuza Harakati Za Chama Cha TANU Na Kusema Bado Hawajawa Na Uwezo Wa Kujiongoza Na Kwamba Wanahitaji Angalau Miaka 25 Mbele Kuweza Kujiongoza, Inasemekana Hakuwa Na Mahusiano Mazuri Na Nyerere Na Mwanzoni Aliwapiga Marufuku TANU Kuingia Kilimanjaro.

Baada Ya Uhuru Wa Tanganyika Hakujihusisha Tena Na Siasa Za Nchi Hii Badala Yake Aliondoka Na Kwenda Kufanya Kazi Umoja Wa Mataifa(UN) Na Kubakia Huko Mpaka Kustaafu Kwake. Alizaliwa Mwaka 1915 na kufariki 2007 Akiwa Na Umri Wa Miaka 92, Na Kuzikwa Huko Marangu, Lyamrakana.

MANGI MKUU WA WACHAGGA
MANGI MKUU WA WACHAGGA NA MKE WAKE

Urithi Wetu Wachagga

urithiwetuwachagga@gmail.com

You may also like...

Popular Posts

11 Comments

  1. T.Marealle 0754 074 533 says:

    Nimesoma yaliyoandikwa kuhusu Mangi Mkuu Thomas Marealle .
    Ukiweza kupata nakala za gazeti la Jamhuri za 10-16 na 17-23 2015″Msimamo wa Nyerere na Marealle UN ulikuwa mmoja” utaona kwamba Chifu hakuipinga TANU yeye na Mwalimu walipoenda UN kudai uhuru.Tarehe 17.6.57 Chifu alipohutubia UN alisema tunahitaji kati ya miaka 10-15(sio 25) kujiandaa kabla ya kupata uhuru.Mwalimu alihutubia UN 18.6.57 na alisema tunahitaji kati ya miaka 10-12 na alisema hakuna tofauti kati ya hotuba zao na kwamba hotuba ya Chifu ilikuwa ya maana kuliko ya kwake.
    Hotuba zote 2 ninazo.
    Chifu aliwahi kumsifu Mwalimu kwenye magazeti mara nyingi kwa mfano katika MWANGAZA ya 17.11.1958 Chifu alisema Nyerere ndio anafaa kuongoza nchi.Aliwahi kumsifu Mwalimu pia alipohojiwa na NATION ya Kenya.
    Kule UN Chifu alisifu TANU na alisema malengo na maslahi ya TANU na Machifu yanafanana.
    Alijiuzulu uenyekiti wa chama cha Machifu baadhi ya Machifu wengine walipopinga mwaliko alitoa kwa Mwalimu kuja kuwahutubia.Alitaka kumkaribisha Mwalimu kwa vile alikuwa anaunga mkono jitihada zake za kudai uhuru.Hii story iko kwenye New York Times ya USA ya 28.2.59. Kwa hiyo Chifu na Mwalimu waliheshimiana.
    Waliokuwa na mamlaka ya kuipiga marufuku TANU au kuiruhusu kwenda popote nchini ni watawala (wakoloni) wa Kizungu
    sio machifu.Na hata Nyerere alisema huko UN 17.6.57 kwamba
    watawala walimpa ruksa kufanya mikutano Dar na Moshi lakini walimnyima ruksa ya kufanya mkutano Tanga.Kwa hiyo sio kweli kwamba Chifu aliipiga marufuku
    TANU kuingia Kilimanjaro kwani hakuna na mamlaka hayo.
    Chifu ndiye alipigania tupate Askofu wa kwanza wa Kilutheri barani Afrika,ndiye aliyeanzisha
    TBC na chuo kikuu cha kwanza nchini.Alitafsiri vitabu pamoja na kimoja cha historia ya kanisa la KKKT.Alikuwa wa kwanza kuhifadhi mazingira ,kukaribisha
    watalii na wawekezaji na alifanya mengine mengi.
    Naomba aliyeandika hizo habari za Chifu aje anione nimpe nakala za hizo hotuba na JAMHURI ilu aandike vizuri habari za Chifu.

    Asante.
    T.Marealle

  2. T.Marealle 0754 074 533 says:

    .

  3. Aika .

    Important

    historical

    Chagga historicals .

    Aika

    Dr EVERLYN Nicodemus PhD

  4. AIKA !

    EVERLYN.

    Chagga Woman

    In

    The World…

    AIKA

    WACHAGGA.

  5. AIKA

    MARANGU

    AIKA

    KILIMANJARO

    AIKA

    RUWA

    NAKUTARAME

    DADA

    DR EVERLYN NICODEMUS PhD

    MIMI
    NI
    MCHAGGA

    BORN

    MARANGU .

    1954
    MARANGU Lutheran hospital

    LUTHERAN .

    MOTHER

    LUTHERAN

    MAMA
    Luterewasia Lauwo

    Father
    NICODEMO MASAOE
    MARANGU

  6. My

    kibosho relations ?

    Yep.

    I am

    Of

    both

    MARANGU and KIBOSHO

    CHAGGA HERITAGE.

    EVERLYN

    1. Which village in Kibosho are you coming from?

  7. Dismas Kimario (Rombo) says:

    Nice to find our history alive

  8. Lenana ni jina la kimasai, inaonekana ukoo huu wa Mareale unaingiliana na wamasai.

    1. Hapana hauingiliana, ni jina tu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *