KAMBI YA WATALII “MANDARA HUT” MARANGU ROUTE, MLIMA KILIMANJARO

MANDARA HUT! Unapopanda Mlima Kilimanjaro Kupitia Njia Ya Marangu(Marangu Route), Kambi Ya Kwanza Unayokutana Nayo(Campsite) Ambapo Watalii Wanalala Siku Ya Kwanza Ya Kupanda Mlima Kilimanjaro Inaitwa Mandara Hut.

Hili Ni Eneo Lingine Lililopewa Jina Hili Kwa Heshima Ya “The Great Mangi Rindi Mandara Moshi” Au “Mangi Rindi Mandara Moshi, Mashuhuri” (1860-1891).

Tunashukuru Kwa Mamlaka Husika Kutambua Mchango wa Wamangi Wetu Waliofanya Makubwa Sana Na Kutujenga Wachagga Hivi Tulivyo, Lakini Tunasikitika Kwamba Wachagga Wengi Hawajui Historia Yao Na Wengine Wanafika Mbali Zaidi Kwa Sababu Ya Kupotoshwa, Ujinga Na Ulimbukeni Wanaona Kama Ni Mambo Ya Kizamani Yasiyokuwa Na Maana, Sio Sahihi Kisiasa(Politically Incorrect) au Hata Kuwa Na Mtazamo Hasi Sana Juu Ya Wamangi.

Hawa Ndio Viongozi Tunaopaswa Kujivunia Kuliko Viongozi Wengine Wowote Maana Sifa Nyingi Tulizonazo Kama Wachagga Ambazo Zimechangia Kuleta Mapinduzi Mengi Kiuchumi Hata Katika Nchi Hii Zilijengwa Na Hawa Wamangi Wetu Kwa Karne Nyingi Zilizopita.

Tunapaswa Tuendelee Kuwatambua Zaidi Kama Jamii Nyingine Zenye Kujielewa Duniani.

Urithi Wetu Wachagga

urithiwetuwachagga@gmail.com

You may also like...

Popular Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *