MTAA WA MANGI MAMKINGA – MOSHI MJINI

MAMKINGA STREET, MOSHI MJINI Kwa Heshima Ya MANGI MAMKINGA RENGUA MUSHI. Mangi Mamkinga Mushi Alikuwa Mangi wa Machame Miaka 200 Iliyopita Tangu Mwaka 1820 – 1858. Alikuwa Ni Mangi Mwenye Nguvu Sana Kilimanjaro Akizitiisha Machame, Kibosho, Uru, Old Moshi, Kirua, Kilema, Marangu, Mamba mpaka Mwika. Yaani Kumbukumbu Zinaonyesha Katika Kipindi Chake Aliitiisha Kilimanjaro yote isipokuwa …

ASILI YA WACHAGGA KUJIVUNIA NCHI YAO.

Sir Charles Dundas, Ambaye Pia Aliwahi Kuwa Gavana wa Serikali Ya Waingereza Kilimanjaro Aliwahi Kusema Kwamba Amezunguka Sana Afrika Lakini Hakuwahi Kukutana na Watu Wazalendo na Wanaoipenda na Kujivunia Nchi Yao Kama Wachagga na Kilimanjaro. Major Dundas Anasema Kwamba Hilo Inawezekana Lilitokana na Hali Nzuri Ya Hewa Ya Kilimanjaro, Vyakula Tele na Uzuri na Umaridadi …

MACHAME NKWARUNGO, USHARIKA WA KWANZA WA KKKT, TANZANIA

KKKT – NKWARUNGO LUTHERAN PARISH, MACHAME. Hili Ndilo Kanisa La Kwanza La Kilutheri, Afrika Mashariki. – Wamisionari wa Kilutheri Kutoka Leipzig, Ujerumani Walifika Kilimanjaro, Mwezi Septemba Mwaka 1893 Walipokaribishwa Na Serikali Ya Wakoloni Wajerumani Kuchukua Nafasi Ya Wamisionari Waliowatangulia Kutoka London, Uingereza wa CMS Society Waliofukuzwa Kilimanjaro na Serikali Ya Wajerumani. – Wamisionari wa CMS …

KITIMBIRIHU HOLISTIC CENTRE!

KITIMBIRIHU HOLISTIC CENTRE! Ni Mtaa Katika Kijiji Cha Mdawi Ya Juu, Old Moshi. Ni Sehemu Ya Kwanza Ambapo Injili Ya Yesu Kristo Ilianza Kuhuburiwa, Sio Tu Ndani Ya Uchaggani Na Kanda Ya Kaskazini Bali Ni Sehemu Ya Kwanza Kufanyika Ibada Ya Kikristo Katika Tanganyika Nzima Ukiondoa Bagamoyo. KKKT, Dayosisi Ya Kaskazini Walitangaza Rasmi Eneo Hili …

KAMBI YA WATALII “MANDARA HUT” MARANGU ROUTE, MLIMA KILIMANJARO

MANDARA HUT! Unapopanda Mlima Kilimanjaro Kupitia Njia Ya Marangu(Marangu Route), Kambi Ya Kwanza Unayokutana Nayo(Campsite) Ambapo Watalii Wanalala Siku Ya Kwanza Ya Kupanda Mlima Kilimanjaro Inaitwa Mandara Hut. Hili Ni Eneo Lingine Lililopewa Jina Hili Kwa Heshima Ya “The Great Mangi Rindi Mandara Moshi” Au “Mangi Rindi Mandara Moshi, Mashuhuri” (1860-1891). Tunashukuru Kwa Mamlaka Husika …

BARABARA YA RENGUA, MOSHI MJINI

RENGUA ROAD. Hii Ni Moja Ya Barabara Katika Mitaa Ya Moshi Mjini, Lakini Ni Watu Wachache Sana Wanaoweza Kufahamu Rengua Alikuwa Ni Nani Hasa, Hii Ni Kutokana Na Sisi Wachagga Kutojihangaisha Kabisa Kufahamu Historia Yetu. MANGI RENGUA KOMBE KIWARIA MUSHI Alikuwa Mangi Wa Machame Mpaka Mwanzoni Mwa Miaka Ya 1800. Alikuwa Mangi Mwenye Nguvu Sana …

LUGHA YA KICHAGGA

Tofauti Ndogo Ndogo Zilizopo. Kwa mfano neno “Sikiliza” Machame wanasema “Aghanyia” Kibosho na Old Moshi wanasema “Adanyia” Uru na Vunjo(Kirua, Kilema, Marangu, Mamba na Mwika) wanasema “Aranyia” Rombo wanasema “Atanyia” Urithi Wetu Wachagga urithiwetuwachagga@gmail.com

MTI MREFU KULIKO YOTE AFRICA

Mti Mrefu Kuliko Yote Afrika Ndani Ya Msitu Wa Kilimanjaro. -Mti Huu Kwa Jina La Kitaalamu Unaitwa “ENTANDROPHRAGMA EXCELSUM”, Una Urefu wa Mita 81.5m -Kwa Kiswahili Unaitwa MKUKUSU, Unapatikana Katika Kijiji Cha Tema, Mbokomu, Old Moshi. -Unakadiriwa Kuwa Na Umri Wa Zaidi Ya Miaka 600, Na Unaweza Kuishi Miaka 300 Zaidi. -Kijiji Cha Tema Na …