ASILI YA WACHAGGA KUJIVUNIA NCHI YAO.

Sir Charles Dundas, Ambaye Pia Aliwahi Kuwa Gavana wa Serikali Ya Waingereza Kilimanjaro Aliwahi Kusema Kwamba Amezunguka Sana Afrika Lakini Hakuwahi Kukutana na Watu Wazalendo na Wanaoipenda na Kujivunia Nchi Yao Kama Wachagga na Kilimanjaro.

Major Dundas Anasema Kwamba Hilo Inawezekana Lilitokana na Hali Nzuri Ya Hewa Ya Kilimanjaro, Vyakula Tele na Uzuri na Umaridadi wa Mlima Kilimanjaro. Ilikuwa ni Adhabu Kubwa Sana Kwa Mchagga Kupelekwa Kuishi Uhamishoni Nje Ya Kilimanjaro Kwani Waliamini Hakuna Sehemu Nzuri Zaidi Ya Kilimanjaro na Maeneo Mengine Yote Nje Ya Kilimanjaro Wachagga Waliyaita ni Porini.

Wachagga wa Zamani Waliamini Kwamba Hakuna Kitu Kisafi na Kitakatifu Duniani Zaidi Ya Kilele Cha Kibo Cha Mlima Kilimanjaro, Ambacho Waliamini Pia Ndio Nyumba Ya RUWA.

Hata Hivyo Dunia Imekuja Kulidhihirisha Hilo Kwa Kilimanjaro Kutajwa Kati Ya Maeneo Ya Asili Yenye Kuvutia Zaidi Duniani.

Kujivunia Kwetu Ardhi Yetu Takatifu Ya Kijimanjaro Ni Urithi Kutoka Kwa Babu Zetu Ambao Walijivunia Zaidi.

Urithi Wetu Wachagga

urithiwetuwachagga@gmail.com

You may also like...

Popular Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *