MANGI MELI MANDARA ANASTAHILI HESHIMA KUBWA ZAIDI YA CHIFU MKWAWA NA ZAIDI YA CHIFU YEYOTE TANGANYIKA KATIKA KUPAMBANA NA WAKOLONI.

Nimeleta Hii Mada Kwa Makusudi, Sio Kwa Lengo La Kupunguza Hadhi Au Umaarufu wa Mtawala Yeyote Bali Kuweka Rekodi Sawa na Kusahihisha Propaganda Ya Kihistoria Tuliyorithi Kwa Wakoloni na Kuendelea Kuishi Nayo Mpaka Leo.

Mangi Meli Mandara, Mtoto wa “The Great Mangi Rindi Mandara Moshi” ni Kati Ya Wamangi Waliokuwa Jasiri Sana Katika Historia, Ni Mangi Aliyekuwa Hajui Nini Maana Ya Woga Hata Mbele Ya Kifo. Lakini Pia Alikuwa Ni Mangi Mwenye Ari Kubwa na Uwezo Mkubwa Kivita Licha Ya Kutokuwa na Umri Mkubwa. Lakini Sasa Katika Mashujaa Wanaotambuliwa Zaidi Kupambana na Wakoloni Katika Iliyokuja Kuwa Nchi Ya Tanganyika Mtawala wa Wahehe Aliyeitwa Mkwawa Anatajwa Zaidi na Kupewa Heshima Zaidi Kuliko Mangi Meli Mandara Ambaye Mapambano Yake Hayapewa Uzito Unaostahili.

Kiuhalisia Ukiangalia Vigezo Walivyotumia Kumtukuza Mkwawa Kwa Ushujaa Huu, Ni Uwezo Mkubwa wa Kivita Aliouonyesha Kwenye Vita Yake Dhidi Ya Wajerumani. Lakini Kwa Vigezo Hivyo, Mangi Meli Mandara Alionyesha Uwezo Mkubwa Zaidi wa Kivita Dhidi Ya Wajerumani Kumzidi Mkwawa na Wengine Wote. Na Kama Swala Ni Uwezo Mkubwa wa Kiutawala, Umashuhuri na Umaarufu Basi Hakuna Chifu Tanganyika Katika Karne Ya 19 Hata Anayemkaribia “The Great Mangi Rindi Mandara” au Baada Yake “The Great Mangi Sina Mushi”. Hata Hivyo Mwandishi wa Kitabu Cha “History of the Chagga People of Kilimanjaro” Mary Kathleen Stahl Anakiri Kwamba Waingereza na Hata Wajerumani Walikuwa na Kawaida Ya Kusambaza Propaganda Kwa Kuyakuza Mapigano Yao na Jamii Fulani Ili Kuitisha Jamii Nyingine Ambayo Ni Imara Zaidi Isijaribu Kupambana Nao.

Licha Ya Wajerumani Kupigana Vita Tatu Kubwa na Wachagga, Moja Wakipigana na Majeshi Ya Mangi Sina, Kibosho 1891 na Nyingine Mbili Wakipigana na Majeshi Ya Mangi Meli Mandara 1892 na 1893 na Kushindwa Vibaya Kiasi Cha Kulazimika Kukimbia Kilimanjaro Kwa Zaidi Ya Mwaka Mmoja Lakini Hawajawahi Kukiri Kwamba Wachagga Ni Wapiganaji Hodari, Waliendelea Kuwahubiria Wachagga Kwamba Ni Watulivu Kwa Kuogopa Kwamba Wakikiri Ukweli Itasababisha Wachagga Kujiamini Zaidi na Kupelekea Tena Vita Vitakavyowaondoa Kabisa Kilimanjaro.

VITA YA MANGI MELI MANDARA NA WAJERUMANI vs VITA YA MKWAWA NA WAJERUMANI.

Nataka Tuone Mambo Yalivyokwenda, Halafu Tutaamua Kwamba Ni Nani Anastahili Heshima Zaidi Katika Mapambano Dhidi Ya Wakoloni. Mkwawa Alikuwa na Mashushushu Ambao Mwaka 1898 Waliweza Kumpa Taarifa za Ujio wa Majeshi Ya Wajerumani Katika Ngome Yake Huko Kalenga Hivyo Aliamsha Majeshi Yake Kwenda Kuwawahi Wajerumani Kuwafanyia Mashambulizi Ya Kushtukiza na Kuuwa Askari Wengi Wa Kijerumani, Wajerumani Walijiongeza Haraka Mapambano Yakaendelea, Mapigano Yalikuwa Makubwa Pande Zote Zikipambana Lakini Mwishowe Majeshi Ya Mkwawa Yalizidiwa Nguvu na Kushindwa Vita na Mkwawa Mwenyewe Akakimbia Kwenda Kujiua.

Mangi Meli Mandara Yeye Wajerumani Walimpelekea Vita Old Moshi Wakitokea Marangu, Mashushushu wa Mangi Meli Waliweza Kuwaona Wakati Ndio Wanaingia Old Moshi, Mara Moja Walijiandaa na Vita Kubwa Ilianza. Upande wa Wachagga Walijipanga Vizuri na Walikuwa na Walenga Shabaha(Snipers) Hodari Ambao Walilenga Zaidi Wale Viongozi wa Vikosi Vya Majeshi Ya Wajerumani Ili Kuua Ari Ya Askari Wengine na Kurahisisha Vita. Majeshi Ya Wajerumani Yaliyokuwa Yamejumuisha Askari Mamluki Kutokea Sudani na Afrika Kusini Walishambulia Ngome Ya Mangi Meli Mandara Tsudunyi, Old Moshi Kutokea Mto Msangachi Upande wa Mashariki. Majeshi Ya Mangi Meli Yakiwa Yamejumuisha Askari wa Kichagga Kutoka Uru, Old Moshi na Kilema Pekee Waliwazidi Nguvu Wajerumani na Kuwaua Kwa Wingi Sana Kuanzia Makamanda wa Vikosi Vya Wajerumani Mpaka Askari Mamluki, Mwisho Walikimbia Kila Mtu na Njia Yake Huku Gavana wa Wajerumani na Mkuu wa Majeshi Ya Wajerumani Kilimanjaro Kapteni Von Bulow Akikimbilia Kahe Kujificha.

Hata Hivyo Askari wa Mangi Meli Walimsaka Wakamkamata Kahe Akiwa Mafichoni na Kumuua pia. Wajerumani Wote Waliokuwepo Kilimanjaro Walikimbia, Hata Wale Waliokuwa Wamebaki Marangu Walitelekeza Kituo Chao Cha Kijeshi Marangu na Kukimbia Kabisa Kilimanjaro. Hakuna Mjerumani Aliyethubutu Kurudi Kilimanjaro na Walipaogopa Sana, Waliwaogopa Sana Wachagga pia. Ni Baada Ya Kushawishiwa Sana Mpaka na Kanisa na Iliwachukua Karibu Mwaka na Nusu Kukubali Kurudi Kilimanjaro, Wakiwa na Silaha Nyingi, Zenye Nguvu Kubwa na Idadi Kubwa Sana Ya Askari na Waliingia Old Moshi Usiku wa Manane na Kufanya Vita Ya Kushtukiza Tena Safari Hii Wakiishambulia Ngome Ya Mangi Meli Mandara Kutokea Upande wa Magharibi Ulipo Mto Kidokonyi, na Hata Hivyo Bado Vita Haikuwa Rahisi.

Sasa Unaweza Kupata Picha Nani Alistahili Heshima Zaidi Katika Kupambana na Wokoloni Wajerumani.

Mapigano Ya Mkwawa na Wajerumani Tunaweza Kuyalinganisha na Mapigano Ya Mangi Sina Mushi, Kibosho na Wajerumani, Kwamba Vita Ilikuwa Ngumu, Askari Wengi wa Kijerumani Waliuawa Lakini Mwisho Wajerumani Walishinda Vita, Hivi.

SANAMU YA MANGI MELI MANDARA

Urithi Wetu Wachagga

urithwetuwachagga@gmail.com

You may also like...

Popular Posts

9 Comments

  1. Everlyn Nicodemus says:

    Simply

    Chagga Woman .

    No

    Comment,

    MARANGU.

    Born

    MARANGU.

    AIKA.

  2. Nimefurahi sana kuona hii website ya Wachaga, naomba niombe kuona historia ya koo zinazo fanana
    mfano
    Mamuya na Lyamuya
    Moshi na Mushi na Mosha
    Mawalla na Sawaya

    1. Jaribu ku-google ukoo wowote utaletwa huku.

    2. Mimi pia nimefurahi sana kufahamu Website hii

  3. Adrian Peter Ossen Kiwera Kitoro Njau says:

    Nimesoma historia ya Wachagga na koo za wachagga. Nimefurahi sana na nashauri tuendeleze huu Urithi wetu.

    1. Ahsante sana, karibu sana.

  4. Nimesoma histori hii inasisimu. Nimuhimu historia kama hii ifahamika kwa vijana wote wakichagga.

    Nadhani kwa Makusudi viongozi wa Tanzania wanafifisha historia ya wachagga kwa Makusudi.

    Nimefurahi sana kufahamu Website hii. Hongereni sana mnaoisimamia

    1. Ahsante sana Mr. Kimaro.

      Karibu sana.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *