UKOO WA KYARA/MAKYARA.

– Kyara/Makyara ni ukoo maarufu wa wachagga unaopatikana kuanzia ukanda wa maeneo ya katikati kuelekea ukanda wa mashariki ya kati ya Uchagga, Kilimanjaro. Huu ni ukoo wenye watu wengi wasomi wanaofanya vizuri sana katika fani mbalimbali kuanzia taaluma, biashara na ujasiriamali na katika taasisi mbalimbali za umma, taasisi binafsi na hata katika mashirika ya kimataifa.

– Kutoka kwenye hostoria ukoo wa Kyara unaonekana kushamiri zaidi katika eneo la himaya ya umangi Kirua Vunjo kuelekea Kilema. Hata hivyo ukoo Kyara haujatajwa sana kwenye historia na kuzungumziwa kwenye kitabu cha chetu cha “Miaka 700 Ya Wachagga” lakini ni ukoo wenye umaarufu zaidi katika maeneo ya mwanzoni mwa ukanda wa mashariki ya kati ya Uchagga, Kilimanjaro baada ya kuvuko mto Nanga, japo unapatikana pia upande wa magharibi wa mto huu.

– Ukoo wa Kyara umeendelea kukua na kusambaa zaidi maeneo mbalimbali na unapatikana kwa wingi kwenye baadhi ya vijiji na kwa uchache kwenye vijiji vingi vya maeneo ya ukanda huu.

– Hivyo ukoo wa Makyara unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Kidia, Old Moshi.

– Ukoo wa Kyara unapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Mero, Kirua Vunjo.

– Ukoo wa Kyara unapatikana kwa wingi sana sana katika kijiji cha Legho, Kirua Vunjo.

– Ukoo wa Kyara unapatikana kwa uchache sana katika kijiji cha Pofo, Kilema.

– Ukoo wa Kyara unapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Leghomulo, Kilema.

– Ukoo wa Kyara unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Kimangara, Mamba.

– Ukoo wa Kyara unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Kiruweni, Mwika.

– Ukoo wa Kyara unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Mawanjeni, Mwika.

Ukoo wa Kyara/Makyara ni ukoo wenye watu wengi sana wasomi na wenye weledi mkubwa lakini lakini bado hakuna maudhui mengi yaliyoandikwa kuhusu ukoo huu, hivyo kuna maswali mengi ambayo bado hayajajibiki kuhusu ukoo huu. Tunahitaji kufahamu mengi zaidi kuhusu ukoo wa Kyara/Makyara ili kuhifadhi maudhui mengi zaidi katika maktaba ya ukoo huu na jamii ya wachagga kwa ujumla. Tunahitaji kuhifadhi taarifa na maudhui katika maktaba za mitandaoni na maktaba halisi pia kwa faida ya kizazi cha sasa na kinachokuja kujitambua na kujijengea kujiamini zaidi kuelekea kufanya makubwa kwenye maisha katika ngazi ya mtu mmoja mmoja, ngazi ya ukoo na jamii nzima ya wachagga kwa ujumla.
Karibu kwa Mchango zaidi wa mawazo na taarifa kuhusu ukoo wa Kyara/Makyara.

1. Je, unafahamu nini kuhusiana na ukoo wa Kyara/Makyara?

2. Unafikiri ni kijiji gani ambacho kimesahaulika kutajwa lakini kuna ukoo wa Kyara/Makyara?

3. Kijijini kwenu kuna ukoo wa Kyara/Makyara?

4. Kama wewe ni wa ukoo wa Kyara/Makyara una nini cha kutuambia kuhusu ukoo wenu?

5. Huwa mna maadhimisho yoyote au sherehe za ukoo mwezi gani?

6. Wewe ni Kyara/Makyara wa kutokea kijiji gani?

7. Bado kuna ushirikiano wowote katika matukio mbalimbali muhimu na ndugu zenu wengine wa matawi ya ukoo wa Kyara/Makyara kutoka maeneo mengine ya Uchaggani?

8. Ni tabia gani unazozifahamu za wachagga wa ukoo wa Kyara/Makyara?

9. Wanawake wa ukoo wa Kyara/Makyara huitwaje, na kwa nini?

10. Una rafiki yako yeyote wa kutokea kwenye ukoo wa Kyara/Makyara?

11. Ni watu gani mashuhuri unaowafahamu kutoka kwenye ukoo wa Kyara/Makyara?

12. Kuna mnyama yeyote ambaye labda ni mwiko kuliwa na wachagga wa ukoo wa Kyara/Makyara?

13. Kuna ukoo ambao hawaruhusiwi kuoana na Wako-Kyara/Makyara kwa sababu zilizowahi kuwepo miaka ya zamani au nyingine zozote?

Karibu kwa Mchango zaidi au maswali.

Ahsanteni.

Wiki ijayo tutaendelea na ukoo mwingine.
www.wachagga.com
Urithi Wetu Wachagga (Facebook).

urithiwetuwachagga@gmail.com

Whatsapp +255 754 584 270

You may also like...

Popular Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *