UKOO WA SHUMA.

– Ukoo wa Shuma ni ukoo wa wachagga mashuhuri wenye watu wengi makini na wanaojituma sana katika nyanja mbalimbali kwenye maisha ndani na nje ya Kilimanjaro na hata nje ya nje. Wachagga wa ukoo wa Shuma asili yao Uchaggani ni Machame ambapo wanapatikana kwa wingi zaidi katika kijiji cha Foo kitongoji cha Foo, Machame.

– Wachagga wa ukoo wa Shuma ni watu wasio na fujo wala kelele sana lakini wenye uwezo wa kufanikisha mambo makubwa. Kutoka kwenye historia inasemekana kwamba zamani ilikuwa ni mwika kwa mchagga yeyote wa ukoo wa Shuma kula nyama ya porini kwani akifanya hivyo huwezi kuumwa vibaya.

– Japo ukoo wa Shuma haujasambaa maeneo mengi ya Kilimanjaro lakini unapatikana kwa kiasi kuanzia katika vijiji vya Machame ya magharibi au Masama kuanzia Ng’uni.

– Ukoo wa Shuma unapatikana kwa kiasi pia katika kijiji cha Uswaa, Machame.

– Ukoo wa Shuma unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Wari, Machame.

– Ukoo wa Shuma unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Foo kitongoji cha Foo, Machame.

– Ukoo wa Shuma unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Foo, Nkwamwasi, Machame.

– Ukoo wa Shuma unapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Nkuu, Machame.

– Ukoo wa Shuma unapatikana kwa kiasi katika vijiji vya kata ya Lyamungo, Machame.

Ukoo wa Shuma ni ukoo wa watu mashuhuri lakini kuna taarifa chache sana kuhusiana na ukoo huu, tunahitaji mchango zaidi wa mawazo ili kuongezea kwenye utafiti na maudhui zaidi juu ya ukoo huu.

1. Je, unafahamu nini kuhusiana na ukoo wa Shuma?

2. Unafikiri ni kijiji gani ambacho kimesahaulika kutajwa lakini kuna ukoo wa Shuma?

3. Kijijini kwenu kuna ukoo wa Shuma?

4. Kama wewe ni wa ukoo wa Shuma una nini cha kutuambia kuhusu ukoo wenu? Huwa mna maadhimisho yoyote au sherehe za ukoo mwezi gani? Wewe ni Shuma wa kutokea kijiji gani?

5. Bado kuna ushirikiano wowote katika matukio mbalimbali muhimu na ndugu zenu wengine wa matawi ya ukoo wa Shuma kutoka maeneo mengine ya Uchaggani?

6. Ni tabia gani unazozifahamu za wachagga wa ukoo wa Shuma?

7. Wanawake wa ukoo wa Shuma huitwaje?

8. Una rafiki yako yeyote wa kutokea kwenye ukoo wa Shuma?

9. Watu gani mashuhuri unaowafahamu kutoka kwenye ukoo wa Shuma?

Karibu kwa Mchango zaidi au maswali.

Ahsanteni.

Kesho tutaendelea na ukoo mwingine.

Whatsapp +255 754 584 270.

You may also like...

Popular Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *