SIKUKUU YA WACHAGGA DUNIANI (WACHAGGA DAY FESTIVAL)

SIKUKUU YA WACHAGGA DUNIANI (WACHAGGA DAY FESTIVAL)

– Kila Tarehe 10/Novemba Ya Kila Mwaka Ilikuwa Ni Sikukuu Kubwa Sana Ya Maadhimisho Ya Siku Ya Wachagga Duniani Yaliyoendelea Kufanyika Mpaka Miaka Ya 1960’s.

– Siku Hii Ilikuwa Inasherehekewa Kama Siku Ambayo Mangi Mkuu wa Kwanza wa Wachagga Aliapishwa Rasmi Mwaka 1952 na Hivyo Ikatangazwa Kuwa Sikukuu Rasmi Ya Wachagga Yenye Lengo La Kuimarisha Umoja na Mshikamano wa Taifa La Wachagga Kilimanjaro. Sherehe Hii Ilisherehekewa Katika Kila Levo Kuanzia Levo Ya Familia, Eneo, Jimbo na Mpaka Levo Ya Taifa Zima La Kilimanjaro Kwenye Ikulu Ya Mangi Mkuu wa Wachagga.

– Watu Wengi Walihudhuria Katika Levo Mbalimbali, Kuanzia Watoto, Wanafunzi wa Shule, Mpaka Wazee. Wanafunzi Waliimba Nyimbo Nzuri Mbalimbali Za Kimaendeleo na Zinazoimarisha Umoja na Mshikamano Baina Ya Wachagga, Sambamba na Uzalendo na Ufahari Kwa Taifa La Wachagga, Kilimanjaro. Vijana Walifanya Maonyesho Ya Umahiri Wao wa Ujuzi na Mbinu Mbalimbali za Kivita Zilizoburudisha Sana Hadhira.

– Watu Mbalimbali Mashuhuri Kama Vile Wamangi, Wachili, Wazee wa Baraza La Wachagga(CC), Wakuu wa Idara Mbalimbali Ndani Ya KNCU na Bodi Ya Kahawa Moshi(Moshi Native Coffee Board(MNCB)) na Watu Wengine Wenye Ushawishi Mkubwa Ndani Ya Jamii Ya Wachagga Walitoa Hotuba Mbalimbali Juu Ya Mshikamano, Umoja na Maendeleo Ya Wachagga, Kilimanjaro. Watu Walikunywa Kula na Kusaza na Watoto Walipewa Zawadi Mbalimbali.

– Japo Ilikuwa Ni Sherehe Ya Kijamii Kama Ilivyo Christmas, Idd au Pasaka Lakini Ilikuja Kuwekewa Vikwazo Baada Ya Uhuru wa Tanganyika na Watu Wa Jamii Nyingine Ambao Hawakupendezwa Nayo Licha Ya Kutokuwa na Uhalali wa Kisheria Kuizuia.

– Hata Hivyo Sisi Kama Wachagga Tunaweza Kuendelea Kuitambua Tarehe 10/Novemba Kama Siku Muhimu Kwetu na Kuendelea Kuisherehekea Angalau Katika Levo Ya Familia.

– Kama Tulivyojifunza Wayahudi Wana Sherehe Kubwa 3 Ambazo Zimekuwa Chachu Ya Maendeleo Zaidi Kwao, Kwani Zinawaunganisha na Kuwafanya Wamoja Zaidi Hata Wanapokuwa Katika Nchi za Watu, Sisi Tuna Sherehe Moja Ambayo Tunaweza Kuitumia Vizuri Kuimarisha Umoja na Mshikamano Wetu. Tukiwa Kwenye Nafasi Nzuri Tutaweza Kuwa Tunaandaa Maadhimisho Ya Sherehe Hii Kwa Lengo Lile Lile La Kuimarisha Umoja na Mshikamano Baina Yetu Katika Kuchochea Maendeleo Zaidi Ya Kiuchumi, Kijamii na Kiutamaduni.

Ahsanteni.

Urithi Wetu Wachagga

urithiwetuwachagga@gmail.com

You may also like...

Popular Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *