HOTUBA YA MANGI MKUU WA WACHAGGA (SIKU YA KUAPISHWA)

HOTUBA YA MANGI MKUU WA WACHAGGA (SIKU YA KUAPISHWA)

“Tunatakiwa Kushirikiana Kwa Karibu Sana Katika Majukumu Yetu Yote Kwa Sababu Bila Ushirikiano Thabiti Malengo Yetu Yote na Jitihada Zetu Vitakuwa ni Kazi Bure. Mimi Kwa Upande Wangu Ni Kama Nilivyoapa, Nitafanya Kila Kitu Ndani Ya Uwezo Wangu Kuweka Mbele Maslahi Ya Baraza Kuu La Wachagga”.

Mangi Mkuu Aliendelea Kusema

“Kwa Nyinyi Ambao Mlikuwa Hamridhishwi na Mwenendo wa Mambo Hapa Awali, Napenda Kuwakumbusha Kwamba Katiba Ya Sasa Ni Hatua Kubwa Kwamba Imeweka Kwenye Mabega Yetu Wenyewe Majukumu Ya Kasi Ya Maendeleo Kwa Nchi Yetu Kilimanjaro na Watu Wetu”.

– Tofauti na Wanasiasa Wengi Ambao Huwaaminisha Wananchi Kwamba Serikali Ndio Inawaletea Maendeleo, Mangi Mkuu wa Wachagga Aliwaweka Wazi Kabisa Wachagga Kwamba Nafasi Yao Kuendelea Iko Katika Mikono Yao Wenyewe Kwa Kutumia Juhudi Zao, Kwa Ushirikiano wa Karibu na Baraza Kuu La Wachagga Ambalo Mangi Mkuu Alikuwa Mwenyekiti Wake.

– Mangi Mkuu Aliwataka Pia Wamangi Waitori wa Majimbo Kumpa Ushirikiano wa Kutosha Katika Kuibadili Kilimanjaro Kuwa Iliyoendelea na Kustaarabika Zaidi.

– Wachagga Walifanya Kazi Kwa Bidii Sana Huku Wakizingatia Ushauri Wa Wataalamu Kwa Usahihi Sana Ambao Walikuwa Wanazunguka Kilimanjaro Nzima Kuhakikisha Kila Mkulima Anafuata Taratibu Zote Zilizopangwa na Mamlaka.

– Chini Ya Uongozi wa Mangi Mkuu, Kilimanjaro Ilipiga Hatua Kubwa Kuwa Kushuhudiwa Hapo Kabla. Zao La Kahawa Liliboreshwa Sana Kupitia Vituo Vya Tafiti za Kisayansi Zilizoanzishwa Sambamba na Wataalamu Wengi Walikuwa Wanaajiriwa na KNCU Kuhakikisha Wakulima Wanazingatia Taratibu Zote Muhimu Zilizowekwa na Bodi Ya Kahawa Moshi Kuhakikisha Ubora wa Zao Hili Uko Katika Viwango Vya Juu Sana.

– Kahawa Ya Kilimanjaro Ilifikia Ubora wa Juu Kabisa Katika Soko La Dunia Ikizishinda Kahawa Kutoka Nchi za Amerika Ya Kusini Kama Vile Brazili Hivyo Kuleta Mapato Makubwa Sana Kilimanjaro. Kilimanjaro Ilitajirika Sana Kuanzia Levo Ya Mtu Binafsi Mpaka Levo za Taasisi na Wachagga Wakiwa Jamii Iliyopiga Hatua Zaidi Afrika Mashariki na Kati Ya Chache Zilizokuwa Kwenye Viwango Vya Juu Kabisa Kimaendeleo Afrika.

– Mafanikio Haya Makubwa Kiuchumi Yalipelekea Wachagga Kujenga na Kuboresha Sana Huduma za Kijamii Kwa Wingi Kama Vile Mashule, Vyuo, Vituo vya Afya, Barabara, Miundombinu Ya Mabomba Ya Maji n.k.,. Sambamba na Kuleta Ufahari Mkubwa na Kujiamini Zaidi Kwa Wachagga Kabla Ya Uhuru wa Tanganyika, Uliopelekea Kilimanjaro Kuanza Kuporomoka Kuelekea Kupoteza Ustaarabu Uliokuwa Umeanza Kuimarisha Misingi.

Ahsanteni.

Urithi Wetu Wachagga

urithiwetuwachagga@gmail.com

You may also like...

Popular Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *