WACHAGGA NI WACHAGGA

WACHAGGA NI WACHAGGA

Zimekuwepo Nadharia Nyingi Zinazojaribu Kuja na Majibu Ya Wachagga Ni Watu Gani, Nyingi Zikitokana na Wachagga Wenyewe Wengine Wanasema Wachagga Ni Wamasai, Wengine Wanasema Wachagga ni Wakamba, Wengine Wanasema Wachagga Ni Wataita N.k.,

Leo Mimi Nakwambia Kwamba Wachagga Ni Wachagga. Yaani Wachagga Ni Jamii Ya Kipekee Ambayo Ni Wachagga.

Japo Ni Kweli Kwamba Kuna Wachagga Asili/Umbo People Waliofika Kilimanjaro Miaka Kama 700 Iliyopita Wakitokea Kwenye Safari Ndefu Iliyoanzia Huko Kaskazini Ya Nchi Ya Ethiopia na Kusini Ya Nchi Ya Misri, Ambao Ndio Walibeba Tamaduni Nyingi za Wachagga wa Leo na Wakaja Kuchanganyika na Jamii Nyingine Za Jirani na Kilimanjaro Kama Wataita, Wakamba, Wamasai na Pengine Hata Wakikuyu Kidogo na Kutengeneza Jamii Ya Wachagga wa Leo Hii, Lakini Jamii Hii Iliyotengenezwa Ndio Wachagga Wenyewe.

Wale Washaka Asili Waliotokea Kaskazini Ya Nchi Ya Ethiopia Ya Leo na Kusini Ya Nchi Ya Misri Ya Leo Wanajumuisha Chini Ya 40% Ya DNA Ya Wachagga wa Leo, Kisha Majirani Kama Wakamba, Wamasai, Wataita, na Wengine Wachache Wanachukua Asilimia Zilizobaki Lakini Haimaanishi Sasa Kwamba Wachagga ni Wataita au Wakamba au Wamasai Bali Ni Sehemu Yao na Wachagga Wanabakia Kuwa Ni Wachagga Kwani Jamii Iliyotengenezwa Kutoka Kwenye Huo Mchanganyiko Ni Ya Tofauti Kabisa Ambayo Ndio Wachagga. Hivyo Sisi Wachagga Ni Wachagga, Period. Ni Ajabu Unakuta Baadhi Ya Wachagga Wanasema O, Sisi Ni Wamasai, Sijui Sisi Ni Wakamba Tena Kwa Kubashiri Tu. Hapana Sisi Ni Wachagga na Hatufanani na Hizo Jamii Nyingine Unazozitaja Wewe, Hata Ukijaribu Kuzitembelea Utaona Hatufanani Nazo, Sisi Ni Jamii Ya Tofauti na Hao.

Tuna Mila na Desturi za Tofauti, Tuna Tamaduni za Tofauti, Tuna Historia Ya Tofauti na Hata Imani Ya Tofauti. Ndio Maana Utakuta Jamii Tatu Kubwa Majirani Zetu za Wakamba, Wamasai na Wakikuyu Wote Kwa Pamoja Mungu Wao ni Ngai, Yaani Wakamba Mungu Wao Ni Ngai, Wakikuyu Mungu Wao Ni Ngai na Wamasai Mungu Wao Ni Ngai, Wakati Sisi Wachagga Mungu Wetu Ni Ruwa/Iruwa, Maana Yake Sisi Ni Jamii Nyingine Kabisa.

Wengine Wanasema Sisi Wachagga Ni Makabila Madogo Madogo Tumeunda Kabila Moja Kubwa. Nafikiri Sisi Wachagga Sio Makabila Madogo Madogo, Sisi Ni Kabila Moja Kubwa, Tungekuwa Makabila Madogo Madogo Neno Wachagga Lisingekuwepo. Sisi Ni Wachagga na Huwezi Kututenganisha Kwenye Makabila Madogo Madogo Licha Ya Kwamba Tulishagawanyika Mara Kadhaa Katika Historia. Nitatoa Sababu.

Kama Nilivyoeleza Hapo Juu Namna Jamii Ya Wachagga Imeundwa Lakini Jamii Hii Imeingiliana Yenyewe Kwa Yenyewe Kwa Karne Nyingi Sana Katika Historia. Kwanza Ile Jamii Ya Wachagga Asili Iliyotokea Kaskazini Ya Ethiopia na Kusini Ya Misri Ambayo Ndio Mama Wa Tamaduni Nyingi Za Wachagga wa Leo Ilisambaa Karibu Kilimanjaro Yote Japo Mwanzoni Walikuwa Wengi Zaidi Upande Magharibi Ya Kilimanjaro. Wageni Wengi Waliochanganyika na Jamii Hii Iliyotokea Kaskazini Ya Ethiopia na Kusini Ya Misri na Kuzaa Jamii Ya Wachagga Walitokea Zaidi Upande Wa Mashariki Kuingia Kilimanjaro Lakini Miaka Ya Baadaye Tena Walihamia Tena Kwa Wingi Sana Upande wa Magharibi Wakachanganyika Zaidi na Watu wa Magharibi na Kutokana na Sababu Nyingine Mbalimbali za Kibinadamu Kama Vita, Njaa, Magonjwa, Uhasama na Changamoto Nyingine za Kimaisha Wachagga Waliendela Kuingiliana Wengine Kwenda Mashariki na Wengine Kurudi Magharibi Kwa Karne Nyingi na Kwa Matukio Mengi Ambayo Hata Historia Haijaweza Kuyarekodi.

Ndio Maana Leo Utakuta Rombo Kuna Massawe, Mwika Kuna Massawe, Mamba Kuna Massawe, Marangu Kuna Massawe, Kilema Kuna Massawe, Kirua Kuna Massawe, Old Moshi Kuna Massawe, Mbokomu Kuna Massawe, Uru Kuna Massawe, Kibosho Kuna Massawe, Machame Kuna Massawe, Sanya Juu Kuna Massawe. Je Unaweza Kusema Watu Wote Hawa Ni Zaidi Ya Makabila Kumi Tofauti?

Yaani Unaweza Kusema Kwamba Temu Iliyoko Rombo Mahida Ni Kabila Lingine, Temu Iliyoko Mwika Kondeni Ni Kabila Lingine, Temu Iliyoko Mamba Komakundi Ni Kabila Lingine, Temu Marangu Ashira Ni Kabila Lingine, Temu Iliyoko Kilema Masaera Ni Kabila Lingine, Temu Iliyoko Kirua Ni Kabila Lingine, Temu Iliyoko Old Moshi Mahoma Ni Kabila Lingine, Temu Iliyoko Uru Ni Kabila Lingine na Temu Iliyoko Kibosho Umbwe Ni Kabila Lingine?

Wote Tunajua Kwamba Koo Nyingi Sana Uchaggani Ziko Kila Mahali na Koo Hizi Nyingi Ni Ndugu wa Damu Ukirudi Kuangalia Walikotoka, Sasa Je, Ndugu Hawa Wanaweza Kuwa Makabila Tofauti? Yaani Kwamba Ngowi Iliyopo Mwika Msae, Nyingine Ipo Mamba, Nyingine Marangu Lyasongoro, Nyingine Kilema, Nyingine Old Moshi Tella, Nyingine Uru, Nyingine Kibosho Mweka, Je Hawa Ni Makabila Tofauti? Tunajua Kwamba Koo Nyingi Zaidi Za Wachagga Ziko Kila Mahali Kilimanjaro Aidha Kwa Wingi au Kwa Uchache na Zamani Watu Hawa Walikuwa Wakitembeleana Katika Matukio Yote Kuanzia Misiba Mpaka Sherehe. Yaani Urassa wa Machame Akipata Shida Alikuwa Analetewa Misaada na Ndugu Zake Wengine Wa Urassa Waliopo Uru, Waliopo Mwika na Waliopo Rombo.

Ikiwa Swai wa Rombo Wamepata Njaa Kidogo Basi Waliletewa Vyakula na Ndugu Zao wa Swai Kutoka Machame, Wengine Kutoka Mwika na Maeneo Mengine Kuhakikisha Ndugu Zao Wanaishi Vizuri, Hili Lilikuwa Ni Jukumu La Lazima La Kiukoo na Watu Walilitimiza Kwa Uhakika Mkubwa.

Lakini Pia Kwa Karne Nyingi Tumeendelea Kuoana na Kuzaliana Wenyewe Kwa Wenyewe Sana na Hivyo Utakuta Kama Mimi Binafsi Nina Bibi Yake Mama Anatoka Marangu, Bibi Yake Baba Anatoka Uru, Babu Yake Baba Asili Yake Ni Kibosho, Bibi wa Baba Asili Yake Ni Old Moshi, Babu wa Mama Anatokea Machame, Yaani Ukifuatilia Kiundani Unaishia Kujiita Tu Wewe Ni Mchagga. Ukirudi Nyuma Zaidi Utakuta Lyimo na Massawe Ni Ndugu wa Damu na Lyimo Huyo Anapatikana Vunjo Yote na Old Moshi na Uru, na Massawe Anapatikana Kwa Wingi Sana, Rombo, Kibosho na Machame, Ni Hivyo Hivyo na Koo Nyingine Pia.

Hivyo Vitu Ambavyo Watu Wanaita Ni Makabila Madogo Madogo Ya Kichagga Ni Himaya za Uchaggani Zilizotokana na Maendeleo Ya Kisiasa Uchaggani Lakini Nazo Ziliendelea Kuungana Mpaka Kufikia Kuwa Tena na Serikali Moja Karne Ya 20, na Hata Karne Za Nyuma Pia Kwa Nyakati Tofauti Tofauti Wapo Wamangi Ambao Walitawala Kilimanjaro Yote Au Sehemu Kubwa Ya Kilimanjaro Kama Mangi Rindi Mandara, Mangi Horombo, Mangi Rengua, Mangi Rongoma, Mangi Mashina n.k.,

Na Hata Hizo Himaya Unazoziona Leo Ukirudi Karne Ya 18 na 17 Nyingi Hazikuwa Moja Bali Zilikuwa Zimegawanyika Zaidi, Kwa Mfano Samanga Ilikuwa Ni Himaya Huru na Haikuwa Chini Ya Marangu Kama Ilivyo Sasa, Kuna Wakati Marangu na Mamba Waliungana Kuivamia Himaya Ya Samanga. Mweka na Kindi Hazikuwa Sehemu Ya Kibosho Bali Ilikuwa Ni Himaya Huru Ambayo Baadaye Ilivamiwa na Kibosho na Kulazimishwa Kuwa Sehemu Ya Kibosho na Iliwahi Kutumika Kuihujumu Kibosho Pia. Sango na Tela Hazikuwa Sehemu Ya Old Moshi, Bali Zilivamiwa na Kulazimishwa Kuwa Sehemu Ya Old Moshi. Uru Haikuwa Himaya Moja Bali Ilikuwa Imegawanyika Kama Mara Tatu Karne za Nyuma. Mbokomu Ilikuwa Ni Himaya Huru Kabla Haijalazimishwa Kuwa Sehemu Ya Old Moshi. Hata Machame Iliwahi Kugawanyika Magharibi na Mashariki Pia. Lakini Kadiri Miaka Ilivyokwenda Mbele Kilimanjaro Ilikuwa Inaendelea Taratibu Kuwa Himaya Moja Kubwa Yenye Nguvu.

Ni Sahihi Zaidi na Faida Zaidi Kwetu Kujitambua na Kujiona Kama Jamii Moja Kubwa Iliyopitia Katika Vipindi Vingi Tofauti Vya Kihistoria Vilivyoleta Utofauti Mdogo Tunaouona Lakini Tunabaki Kuwa Sisi Ni Wachagga. Tuna Mengi Ya Kujivunia Kama Wachagga na Kuna Mengi Tunayoweza Kufanikisha Kama Wachagga Pia na Sio Dhambi Wala Hakuna Ubaya Wowote Kufanya Hivyo Ikiwa Hatujamdhuru Mtu.

WACHAGGA NI WACHAGGA.

Urithi Wetu Wachagga

urithiwetuwachagga@gmail.com

You may also like...

Popular Posts

8 Comments

  1. Kilema hakuna Massawe mbona??

    1. Wapo kidogo sana na wana ndugu zao Kirua Vunjo.

  2. Many many thanks for this article and others!

    1. Wapo kidogo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *