UKOO WA MASSAO.

– Massao ni ukoo maarufu wa wachagga unaopatikana zaidi maeneo ya ukanda wa magharibi ya karibu na katikati ya Uchagga, Kilimanjaro. Kutoka kwenye simulizi za watu wanaufananisha ukoo huu kama ukoo uliotokana na ukoo wa Massawe kwa kiasi ambacho umekaribia kufanana majina yake japo wenye unapatikana maeneo machache sana ukilinganisha na ukoo wa Massawe.

– Kutoka kwenye historia ukoo wa Massao sio ukoo uliozungumziwa sana wala kwenye kitabu cha “Miaka 700 Ya Wachagga” ukoo wa Massao haujatajwa sana. Hata hivyo ukoo wa Massao ni ukoo wenye watu wengi kiasi na wengi wao wakiwa ni wasomi wazuri wanaofanya vizuri katika taasisi mbalimbali ndani na nje ya nchi.

– Ukoo wa Massao umesambaa katika baadhi ya vijiji vya maeneo ya kati ya Uchagga na ni ukoo ulioendelea kukua na kuongezeka sana na unapatikana maeneo haya kama ifuatavyo.

– Ukoo wa Massao unapatikana kwa uchache sana katika kijiji cha Mrawi, Uru.

– Ukoo wa Massao unapatikana kwa wingi sana sana katika kijiji cha Mnini, Uru.

– Ukoo wa Massao unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Mowo, Old Moshi.

Ukoo wa Massao ni ukoo wenye watu wengi sana wasomi na wenye weledi mkubwa lakini bado historia yake haijaelezwa kwa umakini kwenye maandishi. Tunahitaji kufahamu mengi zaidi kuhusu ukoo wa Massao ili kuhifadhi maudhui mengi zaidi katika maktaba ya ukoo huu na jamii ya wachagga kwa ujumla. Tunahitaji kuhifadhi taarifa na maudhui katika maktaba za mitandaoni na maktaba halisi pia kwa faida ya kizazi cha sasa na kinachokuja kujitambua na kujijengea kujiamini zaidi kuelekea kufanya makubwa kwenye maisha katika ngazi ya mtu mmoja mmoja, ngazi ya ukoo na jamii nzima ya wachagga kwa ujumla.

Karibu kwa Mchango zaidi wa mawazo na taarifa kuhusu ukoo wa Massao.

1. Je, unafahamu nini kuhusiana na ukoo wa Massao?

2. Unafikiri ni kijiji gani ambacho kimesahaulika kutajwa lakini kuna ukoo wa Massao?

3. Kijijini kwenu kuna ukoo wa Massao?

4. Kama wewe ni wa ukoo wa Massao una nini cha kutuambia kuhusu ukoo wenu?

5. Huwa mna maadhimisho yoyote au sherehe za ukoo mwezi gani?

6. Wewe ni Massao wa kutokea kijiji gani?

7. Bado kuna ushirikiano wowote katika matukio mbalimbali muhimu na ndugu zenu wengine wa matawi ya ukoo wa Massao kutoka maeneo mengine ya Uchaggani?

8. Ni tabia gani unazozifahamu za wachagga wa ukoo wa Massao?

9. Wanawake wa ukoo wa Massao huitwaje, na kwa nini?

10. Una rafiki yako yeyote wa kutokea kwenye ukoo wa Massao?

11. Ni watu gani mashuhuri unaowafahamu kutoka kwenye ukoo wa Massao?

12. Kuna mnyama yeyote ambaye labda ni mwiko kuliwa na wachagga wa ukoo wa Massao?

13. Kuna ukoo ambao hawaruhusiwi kuoana na Wako-Massao kwa sababu zilizowahi kuwepo miaka ya zamani au nyingine zozote?

Karibu kwa Mchango zaidi au maswali.

Ahsanteni.

Wiki ijayo tutaendelea na ukoo mwingine.

www.wachagga.com

Urithi Wetu Wachagga (Facebook).

urithiwetuwachagga@gmail.com

Whatsapp/Call +255 754 584 270

You may also like...

Popular Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *