UKOO WA MAKYAO.

– Makyao ni ukoo wa wachagga wanaopatikana zaidi katika maeneo ya vijiji vya mashariki ya kati na kwa kiasi mashariki ya mbali ya Uchagga, Kilimanjaro. Ukoo wa Makyao ni ukoo uliopiga hatua kubwa kwa kuzalisha watu wengi wa vipaji mbalimbali na wasomi wa katika nyanja mbalimbali. Huu ni ukoo wenye watu wengi wanaofanya vizuri katika sekta binafsi na hata katika taasisi za umma na taasisi za kimataifa pia.

– Kutoka kwenye historia ukoo wa Makyao unaonekana kuwa umeanza kusambaa katika maeneo ya vijiji mbalimbali katika Uchagga kuanzia mwanzoni mwa karne ya 20. Japo ukoo huu haujazungumziwa kwenye kitabu chetu cha “Miaka 700 Ya Wachagga” lakini ni ukoo wenye watu makini na uliojiimarisha kwa kuwa na mshikamano mkubwa kwa wanaukoo wenyewe.

– Kwa umakini mkubwa ukoo huu umeweza kuandika kitabu chao cha ukoo kinachoonyesha historia ya ukoo wao pamoja na vizazi vyake na matawi yaliyosambaa maeneo ya vijiji mbalimbali vya Uchagga, Kilimanjaro. Ukoo wa Makyao pia ni kati ya koo ambazo huwa zina sherehe rasmi muhimu sana za kiukoo zinazokutanisha wana-Makyao wote waliopo maeneo ya vijiji vyote na kanda zote za Uchaggani, Kilimanjaro mwezi desemba. Ni ukoo uliojenga ukaribu na maelewano sana baina ya wanaukoo unaostahili kuigwa na koo nyingine zote kubwa na ndogo.

– Ukoo wa Makyao kama walivyoweza kujieleza wenyewe umesambaa maeneo ya vijiji mbalimbali vya Uchagga, Kilimanjaro wanakopatikana.

– Ukoo wa Makyao unapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Mkyashi, Kilema.

– Ukoo wa Makyao unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Kokirie, Mamba.

– Ukoo wa Makyao unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Msae Nganyeni, Mwika.

– Ukoo wa Makyao unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Msae Nganyeni, Mwika.

– Ukoo wa Makyao unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Lole Marera, Mwika.

– Ukoo wa Makyao unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Maringá, Mwika.

– Ukoo wa Makyao unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Kiruweni, Mwika.

– Ukoo wa Makyao unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Aleni Chini, Keni, Rombo.

Ukoo wa Makyao ni ukoo wenye watu wengi sana wasomi na wenye weledi mkubwa lakini licha ya kwamba wamejitahidi kuandika kitabu cha kuelezea ukoo wao lakini bado tunahitaji maudhui zaidi kwa maswali ambayo bado hayajajibiwa na mambo mengine zaid. Tunahitaji kufahamu mengi zaidi kuhusu ukoo wa Makyao ili kuhifadhi maudhui mengi zaidi katika maktaba ya ukoo huu na jamii ya wachagga kwa ujumla. Tunahitaji kuhifadhi taarifa na maudhui katika maktaba za mitandaoni na maktaba halisi pia kwa faida ya kizazi cha sasa na kinachokuja kujitambua na kujijengea kujiamini zaidi kuelekea kufanya makubwa kwenye maisha katika ngazi ya mtu mmoja mmoja, ngazi ya ukoo na jamii nzima ya wachagga kwa ujumla.

Karibu kwa Mchango zaidi wa mawazo na taarifa kuhusu ukoo wa Makyao.

1. Je, unafahamu nini kuhusiana na ukoo wa Makyao?

2. Unafikiri ni kijiji gani ambacho kimesahaulika kutajwa lakini kuna ukoo wa Makyao?

3. Kijijini kwenu kuna ukoo wa Makyao?

4. Kama wewe ni wa ukoo wa Makyao una nini cha kutuambia kuhusu ukoo wenu?

5. Huwa mna maadhimisho yoyote au sherehe za ukoo mwezi gani?

6. Wewe ni Makyao wa kutokea kijiji gani?

7. Bado kuna ushirikiano wowote katika matukio mbalimbali muhimu na ndugu zenu wengine wa matawi ya ukoo wa Makyao kutoka maeneo mengine ya Uchaggani?

8. Ni tabia gani unazozifahamu za wachagga wa ukoo wa Makyao?

9. Wanawake wa ukoo wa Makyao huitwaje, na kwa nini?

10. Una rafiki yako yeyote wa kutokea kwenye ukoo wa Makyao?

11. Ni watu gani mashuhuri unaowafahamu kutoka kwenye ukoo wa Makyao?

12. Kuna mnyama yeyote ambaye labda ni mwiko kuliwa na wachagga wa ukoo wa Makyao?

13. Kuna ukoo ambao hawaruhusiwi kuoana na Wako-Makyao kwa sababu zilizowahi kuwepo miaka ya zamani au nyingine zozote?

Karibu kwa Mchango zaidi au maswali.

Ahsanteni.

Wiki ijayo tutaendelea na ukoo mwingine.

www.wachagga.com

Urithi Wetu Wachagga (Facebook).

urithiwetuwachagga@gmail.com

Whatsapp +255 754 584 270.

You may also like...

Popular Posts

2 Comments

  1. Ukoo wa Makyao, umebarikiwa kwa kuwa na wachapa kazi, pia wanawake wa Makyao huwa na ushawishi mkubwa sana kwenye Sekta zote pamoja na masuala ya Kiroho, biashara na Elimu.
    Namjua msajili wa NGOs nchini ni dada Makyao
    Wengine ni Neema Makyao
    Mwingine ni mwenyekiti wetu makin sana Eng Joel Makyao
    Na wengine wengi

    Watoto wao ni werevu

    1. Ahsante sana kwa mchango zaidi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *