TUNA JUKUMU LA KURUDISHA UTUKUFU ULIOPOTEA.

Namna Tulivyokubali Kurudi Nyuma.

– Mpaka Kufikia Miaka Ya 1960’s Wachagga Ilikuwa Ndio Jamii Iliyopiga Hatua Kubwa Zaidi Afrika Mashariki Kwa Maendeleo Ya Kiuchumi, Kisiasa na Hata Kijamii. Hata Wakikuyu wa Kenya Ambao Walionekana Kuchangamka Sana Katika Huu Bado Walikuwa Nyuma Sana Ukilinganisha na Wachagga.

– Hili Linaelezwa Hata na Kathleen Mary Stahl Mara Kadhaa Kwenye Kitabu cha “History of the Chagga People of Kilimanjaro” Ambapo Alijaribu Kulinganisha Jamii Majirani na Wachagga na Kuwataja Wakamba, Wakikuyu, Wataita, Wataveta, Wapare, Wamasai, Wameru na Waarusha. Ilionekana Kwamba Wachagga Ndio Jamii Iliyopiga Hatua Kubwa Zaidi na Ambayo Ina Ari na Shauku Kubwa Ya Kimaendeleo Kuliko Jamii Nyingine Zote. Eva Stuart Naye Anaelezea Aliyoyashuhudia Kwa Wachagga Kilimanjaro Miaka Ya 1920’s Ile Ari na Hasira Kubwa Ya Kimaendeleo Ambayo Hakuiona Sehemu Nyingine Yoyote Kwa Kiasi Hicho.

– Lakini Wachagga Hawakuwa na Utofauti na Upekee Tu Baada Ya Ukoloni Bali Walishaonyesha Upekee na Tofauti Kabisa Kabla Hata Ukoloni Haujaingia Afrika Mashariki. Wachagga Walikuwa na Uwezo Mkubwa Kiakili, Kibunifu na Kupenda Mafanikio Tangu Kale na Kale. Anaeleza Alexander Le Roy na Waandishi Wengine Waliyofika Kilimanjaro Mwishoni mwa Karne Ya 19 Jinsi Walivyoshangazwa na Ubunifu wa Miundombinu Ya Umwagiliaji Ambayo Ilitengenezwa Kwa Maarifa Ya Hali Ya Juu. William Makupa Leo Ame-post Andiko La Namna Wachagga Walivyokuwa Wanaelezewa Kwenye Encyclopedia Ya Brittanica Nimeambatanisha Picha Hiyo na Makala Hii.

– Pia Uchagga Ilikuwa na Wanasiasa na Watawala Mashuhuri Waliokuwa Wanafanya Diplomasia za Kimataifa Mpaka na Watawala wa Nchi za Ulaya Kama Vile Mangi Rindi Mandara Ambaye Alikuwa Akiwasiliana na Malkia Victoria wa Uingereza, Kaizari Wilhelm II wa Ujerumani n.k., na Hata Kupeleka Mabalozi Ujerumani. Hii Ilikuwa ni Hatua Kubwa Ambayo Iliweza Kufanywa na Watawala Kama Wawili Peke Yake Afrika Mashariki Katika Karne Ya 19. Hayo na Mengine Mengi Yalikuwa ni Maendeleo na Hatua Kubwa Sana Ya Jamii Ya Wachagga Kupiga.

– Lakini Baada Ya 1961 Kuna Mambo Muhimu Ambayo Tuliyaruhusu Yaliyoanza Kupelekea Anguko La Wachagga Taratibu Mpaka Kujisahau Kabisa. Kwanza Kabisa Ukiachana na Siasa Potofu za Kijamaa Zilizodhoofisha Sana Uchumi Lakini Pia Kukubali Kuhubiriwa na Watu Wengine Namna Tunavyokosea na Jinsi Tunavyotakiwa Kuishi. Tulifikiri Kwamba Wanafanya Hivyo Kwa Nia Njema na Kwa Maslahi Mapana Ya Nchi Kumbe Lengo ni Kuturudisha Nyuma Kwa Sababu Hawafurahishwi na Hatua Kubwa Tuliyokuwa Tumepiga. Walitamani Wote Tuwe Nyuma Ili na Wao Wajisikie Vizuri. Juhudi Hizi za Kuturudisha Nyuma Nafikiri Tumeendelea Kuzishuhudia Hata Hivi Karibuni Zikiwa ni Agenda za Siri za Baadhi Ya Watu, Lakini Zamani Mambo Hayo Yalifanyika Kwa Nguvu Zaidi na Yalibomoa Sehemu Kubwa Ya Tuliyokuwa Tumejenga Hususan Ari Ya Maendeleo na Kujiamini.

– Hivyo Sehemu Ya Kwanza na Muhimu Iliyoshambuliwa ni Umoja Wetu na Kuua Ile Hali Ya Kujithamini Kihadhi na Kujiamini (Self Esteem). Hilo Lilifanyika Kuanzia Kubana Fursa za Elimu Mpaka Kuitwa Majina Mbalimbali Yanayochafua Hadhi Ya Jamii Kama Vile Wabinafsi, Wezi, Wajanja Wajanja n.k. Badala Ya Wachapakazi, Wenye Umoja na Wanaojijali na Kupenda Maendeleo n.k.,.

– Kwa Maana Hiyo Sehemu Ya Kwanza Ya Muhimu Sana Tunayopaswa Kujenga Kwa Sasa ni Kurudisha Ile Hali Ya Kujitambua Kwamba Sisi ni Nani na Tulikuwa Tumefika Wapi. Hili Ni Muhimu Sana Kwa Sababu Ndio Mwanzo wa Kurudisha Ile “Self Esteem” Inayotokana na Mambo Makubwa Tuliyokuwa Tumefanikisha Kama Jamii. Yaani Mfano Mzuri ni Wewe Kufikiria Hapo Sasa Unawaza Huna Pesa Halafu Akatokea Mtu na Kukwambia Kwamba Kuna Milioni 100 Ya Kwako Benki na Ukathibitisha Hilo. Baada Ya Hapo Kwa Vyoyote Vile Mtazamo na Mwenendo Wako Utabadilika Kwa Taarifa Hiyo Tu Peke Yake.

– Sasa Inatakiwa Tufahamu Kwa Usahihi na Uhakika Sisi ni Watu wa Tofauti Kiasi Gani na Kwamba Kuna Kazi Ilifanyika Huko Nyuma Kuhakikisha Kwamba Tunaaminishwa Kwamba Sisi Sio Lolote Wala Chochote Zaidi Ya Wezi na “Wabinafsi”, Neno Ambalo Halina Hata Mashiko. Kwa Walioangalia Ile Filamu Ya “LION KING” Waliweza Kuona Jinsi Yule Mtoto “SIMBA” Alivyojisahau Kwamba Yeye ni Mfalme wa Pori na Kuishi na Wanyama Wengine wa Kawaida na Kuiga Tabia Zao. Lakini Baada Ya Kuja Kukumbushwa Kwamba Yeye ni Mfalme wa Pori na Kuachiwa Himaya Ya Kifalme Aliunguruma na Kuanzia Siku Hiyo Alianza Kulitawala Pori.

– Hivyo Ndivyo Namna Tunapaswa Kujikumbusha na Kuwarithisha Watoto Wetu Ili Kujijengea Kujiamini na Kuona Tunaweza Kufanya Makubwa Kwa Sababu Tu Ya Tulikotoka. Nilisoma Hotuba Ya Mtawala Maarufu wa Athens Ya Ugiriki Ya Kale Aliyejulikana Kwa Jina La “Pericles” Ambaye Anatajwa Kuwa Moja Ya Watawala Bora Kabisa Kuwahi Kutokea Duniani Katika Historia.

– Pericles Alikuwa Akihutubia Kuwahamasisha Waathenia Kufanikisha Mambo Makubwa Kupitia Histora Zao za Kale Ambazo Zilikuwa Kubwa na Tukufu Sana. Kupitia Yale Ambayo Wakale Wao Walifanikisha Waathenia Waliweza Kujijengea Kujiamini na Kufanya Mambo Makubwa Kwenye Kila Sekta Muhimu Kwao.

– Hivyo ni Wakati Muafaka Kabla Hatujaendelea Kuchelewa Zaidi Tuanze Kujifunza na Kurithisha Historia Yetu Tukufu Ambayo ni Kubwa, Ya Kujivunia na Inayosisimua Sana Kwa Watoto na Vizazi Vinavyofuata. Hiyo Ndio Njia Peke Ya Kuanzia Katika Kurudisha Utukufu Uliopotea Kwa Sababu Inaanza na Mtazamo Ambao Unatokea Kwenye Fikra Sahihi Kisha Mambo Mengine Kufuata. Bila Mtazamo na Fikra Sahihi Tutajikuta Tunaishi Mitazamo na Fikra Potofu za Watu Wenye Chuki na Husda Kwa Maendeleo Yetu na Kwa Ujinga Wetu Tutasikiliza na Kuamini Fikra Zao Hasi Juu Yetu Zilizojificha Kwenye Kivuli cha Nia Njema.

– Tukifanikiwa Kujenga Mitazamo Sahihi Kwa Sehemu Kubwa Kwa Wingi Wetu Kupitia Kufahamu Historia Yetu Kubwa, Itakuwa Ndio Mwanzo Mzuri wa Kuanza Kuweka Mipango na Mikakati Sahihi Ya Kuelekea Kule Tunakopanga Kufika Kama Jamii. Tofauti na Hivyo Mitazamo Potofu na Ujinga Vitaendelea Kutuacha Tukiwa Tunaamini Maneno Yasiyokuwa na Maana Yaliyoandaliwa Maalum Kwa Ajili Ya Anguko Letu.

– Ili Kuchangia Katika Sehemu Ya Kuipeleka Jamii Yetu Mbele, Kuondoa Mitazamo Potofu Iliyoturudisha Nyuma Sana Kwa Miaka Mingi na Kujenga Mitazamo Sahihi, na Zaidi Kuokoa Kizazi Kinachokuja na Kuilinda Jamii Hii Isipotee Nunua Kitabu cha “Miaka 700 Ya Wachagga” Kwako, Kwa Familia Yako na Hata Kwa Watu Wengine Makini wa Karibu. Pia Saidia Katika Kusambaza Jumbe Zinazotangaza Kitabu Hiki Ili Kufikia Watu Wengi Zaidi na Kujenga Umoja na Mshikamano wa Jamii Ya Wachagga Ulio Imara Sana.

– Hii Ni Kwa Sababu Kitabu Hiki Kimeelezea Historia Kwa Kina na Kuelezea Kwa Nini Jamii Ya Wachagga Ilianguka na Nini Kifanyike Ili Kurudisha Utukufu Uliopotea. Hatuna Haja Ya Kulalamika Tena Wala Kulaumu Sana Wale Walioamua Kutupotosha Kwa Makusudi na Kutudhoofisha Bali Kuchukua Hatua Sasa Hivi Ili Kuanza Safari Ya Kurudisha Heshima Iliyopotea. Kulaumu Hakutasaidia Tena Kwani Hatuwezi Kurekebisha Yaliyopita Bali Kuchukua Hatua na Kujenga Kule Kulikobomolewa.

– Twende Sasa Tukarudishe Utukufu Uliopotea Kwa Kuanza Kubadili Mitazamo Ya Watu Wetu na Taratibu Tutaendelea na Hatua Nyingine. Kitabu Kina Nguvu Kubwa Sana Ya Kubadili Mitazamo Hususan Kama Tutaweka Nguvu Kubwa Kuhakikisha Kinafikia Watu Wengi. Nashukuru Kwa Wale Ambao Wameendelea Kusambaza Ujumbe Kwenye Makundi Ya Whatsapp na Watu Wengi Wamechukua Hatua, Hakika Kazi Yenu ni Njema na Mnachangia Sehemu Muhimu Sana Ya Kuijenga Upya Jamii Hii Iliyokuwa Inaelekea Kupotea.

Karibu Kwa Maoni Pia.

Karibu sana Kwa Kitabu.

Whatsapp No. +255 754 584 270.

You may also like...

Popular Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *