KITABU CHA “MIAKA 700 YA WACHAGGA” KINAPATIKANA.

– Baada ya Safari Ndefu Iliyoambatana na Vikwazo na Changamoto Nyingi Hatimaye Tumefanikiwa Kukamilisha Uandishi na Uchapishwaji wa Kitabu Muhimu Kwa Wachagga cha “Miaka 700 Ya Wachagga”. Safari Imekuwa Ngumu Zaidi Ya Ilivyotegemewa Kutokana na Sababu Mbalimbali, Tunashukuru Kwamba Tumekamilisha.

– Wote Tunajua Dhahiri Kwamba Kama Tusipochukua Hatua Sasa Hivi Historia Yetu Inakwenda Kupotea, Tena Inapotea Kwa Kasi Kubwa Sana Kiasi Kwamba Watu Wengi Wameshaikatia Tamaa. Lakini Habari Njema Ni Kwamba Bado Kuna Nafasi Kubwa Ya Kulirekebisha Hilo Kwa Sisi Kuchukua Hatua Sasa Hivi Badala Ya Kuendelea Kujichelewesha. Itakuwa ni Kosa Kubwa Sana Endapo Tutaruhusu Historia Yetu Tukufu Sana Kupotea Kwani Ikipotea Kabisa Kama Ilipokuwa Imefikia na Jamii Yetu Itakuwa Imekufa na Inazikwa. Hili Litapelekea Kuwa na Kizazi Mbumbumbu cha Wachagga Kisicho na Heshima Yoyote Mbele Ya Jamii Nyingine za Dunia Hii Kwani Dharau Itaanzia Ndani Yao Wenyewe Kwa Sababu Hakuna Watakachokuwa Wanajua Kuhusu Wao Wenyewe.

– Jamii Inayotunza Historia Siku Zote ni Jamii Makini na Ambayo Hufanya Makubwa Kwenye Maisha. Kwa mfano Angalia Jamii Kama Ya Wayahudi Walioweza Kutunza Historia Yao Vizuri na Kwa Umakini Mkubwa Imeweza Kuwasaidia Hata Kurudi Katika Nchi Yao Ya Asili Ya Israel Mwaka 1948. Hii ni Baada Ya Kupotelea Maeneo Mbalimbali Duniani Kwa Takriban Miaka 2,000. Hapa Unaweza Kuiona Vizuri Nguvu Ya Historia, Jamii Imeweza Kurudisha Ardhi Yao Baada Ya Miaka 2,000 Ya Kupotelea Uhamishoni. Jamii Nyingi Zimeshindwa Kufanya Hivi Kwa Sababu Ya Kukubali Kupoteza Historia Yao. Wayahudi Pia Wameweza Kutawala Biashara na Uchumi Kwa Ujumla Ulaya na Marekani Kwa Kuwa Makini Sana na Mambo Yao na Hususan Historia Yao. 40% Ya Mabilionea Marekani ni Wayahudi.

– Kupoteza Historia ni Kuelekea Kudhalilika na Kujidharau, Lakini ni Pamoja na Kuwadhulumu Sana Vizazi Vinavyofuata Ambao Hawatakuwa na Cha Kuonyesha Wala Kujivunia. Leo Hii ni Wachagga Wangapi Wasiojijali Wala Kujithamini Kwa Sababu Tu Hawajui Chochote Juu Ya Kule Walikotoka? Vizazi Hivyo Vitajikuta ni Mbumbumbu na Kulaumu Sana Vizazi Vilivyotangulia Ambao Walikuwa Kwenye Nafasi Nzuri Zaidi Ya Kuhifadhi Historia Lakini Walipuuza Hilo na Hivyo Hawatawasamehe Kamwe.

– Leo Hii Kuna Baadhi Ya Jamii Chache Zinazojitambua Afrika Wako Makini Sana Kujifunza na Kuhifadhi Historia Zao na Hata Zimeendelea Kuwa na Ushawishi Mkubwa Kwenye Siasa Zao Pia, Lakini Muhimu Zaidi Zinawajengea Kujiamini Sana(Self Esteem) Katika Kukabiliana na Watu Wengine Wa Dunia Wenye Kujitambua Sana. Jamii Nyingi za Asia Zimepiga Hatua Kupitia Kujifunza Historia Zao na Kuona Kwamba Walikuwa na Uwezo Mkubwa Zamani Tofauti na Propaganda za Kikoloni na Watu Wengine Wenye Wivu Waliotaka Kuwaaminisha Kwamba Wao Sio Lolote Sio Chochote. Kwa Kuweza Kuepuka Hilo Wameweza Kufanya Makubwa Sana Ambayo Yanaonekana Wazi Leo Hii.

– Historia Yetu Imekuwa Ikifichwa na Kugandamizwa na Watu Ambao Hawakututakia Mema Sana Tangu Mwanzoni Kabisa Wala Kupenda Kuona Tukijitambua Kwamba Tulikuwa ni Watu Wakuu na Tuliofanya Makubwa Sana Siku Zilizopita na Badala Yake Walitaka Tujidharau na Kupotea Kabisa. Ni Jukumu Letu Sasa Kuhakikisha Kwamba Maarifa Haya Ya Historia Yetu Yanasomwa na Kufahamika Miongoni Mwetu na Hususan Kwa Watoto Wanaokua. Hilo Litasaidia Kujenga Kizazi Kinachoanza Kuelewa Wametokea Wapi, Walikuwa nani na Hivyo Kuamua Kwa Usahihi Kwamba Waelekee Wapi. Inapaswa Ifike Mahali Kijana au Mtoto Wa Kichagga Anapokutana na Changamoto Ajisemee Mwenyewe “Mimi ni Mchagga ni Lazima Nitafanikisha Hili Kama Alivyofanikisha Mangi Horombo na Wazee Wengine Wengi Waliotangulia”. Hivyo Ndivyo Watoto wa Kkichina Husema Kwa Historia Zinazokwenda Mpaka Miaka 3,000 Iliyopita. “Mimi ni Mwanajeshi wa Sparta Lazima Nifanikishe Hili”. “Mimi Natokea Athens Hili Haliweza Kunishinda”. Sasa Mtoto au Kijana wa Kichagga Atawezaje Kusema Hivyo Ikiwa Hajui Chochote Juu Ya Yaliyopita? Si Atamsikiliza Mtu Anayetokea Kwenye Jamii Nyingine Duni Akisema, “Haya Mambo ni Magumu na Makubwa Sisi Hatuyawezi” na Kisha Kumfuata Huyo Kwa Kujiona Hawezi?

– Tunapaswa Kuepuka Kufanya Makosa Ya Kusikiliza Watu Kutoka Nje Ya Jamii Yetu Wanaojaribu Kutuaminisha Kwamba Historia Hii Haina Umuhimu. Hiyo ni Kwa Sababu Kwamba Wengi Wao ni Watu Wasiofurahia Historia Hii, Hivyo Siku Zote Watabaki Kuwa na Mtazamo Hasi Juu Ya Historia Hii. Sisi Tutakuwa Wajinga Sana Endapo Tutasikiliza Watu Wanaoongozwa na Hisia za Chuki Dhidi Ya Maendeleo Yetu Wenyewe na Mwishoni Kuja Kutucheka Sana Kwa Ujinga Wetu wa Kuwasikiliza Wao, Halafu Ukute Pengine Wakati Huo Wao Walitunza Historia Zao. Tunahitaji Kuwafundisha Watoto Wetu Historia Yao Bila Kujali Nani Anasema Nini. Hii Ni Kwa Faida Ya Leo na Kesho Ya Jamii Hii. Mtoto Aone Kwamba Ana Jukumu La Kurudisha Heshima Nyumbani Kwao Kama Mwanajeshi wa Sparta Badala Ya Kujiona Hana Lolote La Maana La Kufanya Kwa Sababu Hana Jamii Yoyote Yenye Kujitambua Anayowajibika Kwayo Kisaikolojia.

– Kwa Karne Ya 21 Historia Ya Jamii Pia ni Sehemu Muhimu Sana Ya Kukuza Utalii wa Eneo Husika na Hivyo Kukuza Uchumi wa Eneo Hilo Pia Kwa Namna Moja Au Nyingine. Historia Ya Jamii Inasaidia Kuongeza Umaarufu wa Eneo Husika, Sambamba na Heshima na Hadhi Ya Jamii Hii Mbele Ya Macho Ya Watu Wa Jamii Nyingine. Kufahamu Historia Pia Kunasaidia Kuongeza Mshikamano, Upendo, Kuthaminiana na Kuheshimiana Kwa Watu wa Jamii Husika.

– Kuhifadhi, Kutunza na Kujifunza Historia Ndio Njia Pekee Ya Kuhakikisha Kwamba Jamii Husika Inadumu Kwa Maelfu Ya Miaka Bila Kupotea Wala Kupoteza Ile Thamani Ambayo Kila Mtu wa Jamii Hiyo Anakuwa Nayo Kwa Kujihusianisha na Jamii Husika.

– Tukirudi Kwenye Kitabu Chetu Cha “Miaka 700 Ya Wachagga”, Kwanza ni Kitabu Ambacho Kinatoa Picha Ya Jamii Ya Wachagga Kwa Mapana Lakini Kikiwa Zaidi Kimeegemea Kwenye Mtazamo Chanya Unaolenga Kuileta Pamoja Jamii Yote Kwa Pamoja Kufahamu Ilikotokea na Yale Iliyopitia Kwa Ajili Ya Kuamua Kwa Usahihi Zaidi ni Wapi Inataka Kuelekea.

– Hivyo Kutoka Kwenye Zile Makala za Historia Tulizokuwa Tunaweka Hapa Mwezi Novemba na Desemba Mwaka Jana 2021, Tumefanya Maboresho Mbalimbali na Nyongeza Kiasi Katika Historia Nzima Kwa Ujumla. Hii ni Baada Ya Kutembelea Familia Zote za Wamangi Kilimanjaro, Sambamba na Baadhi Ya Watu Wengine Waliokuwa na Mchango Kiasi.

– Katika Himaya Ya Umangi Siha/Sanya Juu Tumezungumza na Mangi Godfriend Kileo na Kupata Uelewa wa Kile Anachoenda Kutekeleza Katika Majukumu Yake Mapya Baada Ya Kuapishwa Desemba 2021. Tumeweza Kuongezea Majukumu Yake Ya Sasa Ya Umangi Kwenye Kitabu Hiki. Katika Himaya Ya Umangi Kibosho Tumefanya Maboresho Ya Matukio Muhimu Ya Kihistoria na Masahihisho Kidogo Kwa Matukio Ya Miaka Ya Kuanzia Mwanzoni Mwa 1700 Mpaka Katikati Ya Miaka Ya 1850. Tumeweza Pia Kuongezea Himaya Ya Umangi Kindi Ambayo Ilikuwepo Zamani Ikiwa na Uhasama Mkubwa na Kibosho Kihistoria Kabla Ya Kuanguka na Kuunganishwa Kuwa Sehemu Ya Himaya Ya Umangi Kibosho.

– Katika Himaya Ya Umangi Uru Tumeweza Kupata Taarifa Sahihi za Mtiririko wa Watawala na Matukio Yao Kihistoria Kuanzia Wakati wa Utawala wa Mangi Mkoruo Karne ya 16 Mpaka Kwenye Utawala wa Mangi Sabas Kisarika Katika Karne Ya 20. Hii ni Sambamba na Kuelezea Utawala wa Mangi Warsingi wa Uru na Siasa za Nyakati Zake Aliyepata Kuwa na Nguvu Sana Hata Kuiangusha na Kuitawala Kibosho Kwa Muda Katika Miaka Ya 1700. Tumefanya Maboresho Kidogo Pia Katika Himaya za Katikati Ya Kilimanjaro.

– Tumeongeza Taarifa Nyingi na Kufanya Maboresho Katika Himaya za Umangi za Rombo Kwa Ujmla Wake Kuanzia Keni-Mriti-Mengwe, Mkuu, Mashati na Zaidi Usseri Ambayo Kulikuwa na Taarifa Nyingi Muhimu Zinazokosekana, Zimeweza Kupatikana na Kujumuishwa.

Muhimu Zaidi Tumeambatanisha Picha za Watawala na Watu Wengine Mashuhuri wa Nchi Ya Uchagga Sambamba na Watu Wengine Waliopata Kuhusika na Matukio Muhimu Katika Nchi Ya Uchagga Tangu Karne Ya 19 Ambazo ni.

Picha Zifuatazo;-

– Mwanahistoria Nathaniel Mtui Kutokea Mshiri, Marangu.

– Joseph Merinyo Maro, Mwanamapinduzi wa Harakati za Utaifa.

– Mmisionari wa Kwanza Kilimanjaro Johannes Rebmann 1848.

– Mwanajiografia Baron Karl Klaus Von Der Decken 1861.

– Mmisionari wa The United Methodist Church, Charles New 1871.

– Mwanajiografia wa Kwanza Kufike Kileleni Hans Meyer 1889.

– Mchagga Aliyeambatana na Hans Meyer Yohane Lauwo 1889.

– Mangi Sinare Kileo wa Siha/Sanya Juu.

– Mangi Jacobus Sinare Kileo wa Siha/Sanya Juu.

– Mangi Godfriend Jacobus Kileo wa Siha(Mangi wa Sasa).

– Mangi Shangali Ndesserua Mushi wa Machame.

– Mangi Ngulelo Ndesserua Mushi wa Machame.

– Mangi Abdiel Shangali Mushi wa Machame.

– Mangi Gilead Abdiel Mushi wa Machame.

– Mangi Charles Shangali Mushi wa Masama.

– Mangi Sina Mushi wa Kibosho.

– Father Martin Rohmer wa Parokia Ya Kibosho.

– Mangi Ngilisho Sina Mushi wa Kibosho.

– Mangi Alex Ngilisho Mushi wa Kibosho.

– Mangi Kisarika Seiya Mushi wa Uru.

– Mangi Sabhas Laiseri Kisarika wa Uru.

– Mangi Philipo Mlatie Moshi wa Mbokomu.

– Mangi Harry Philipo Mlatie Moshi wa Mbokomu(Mangi wa Sasa).

– Mangi Rindi Mandara.

– Mpelelezi wa Uingereza Sir Harry Hamilton Johnston.

– Father Alexander Le Roy wa “Mission To Kilimanjaro”.

– Mjumbe wa GEACO Dr. Karl Julke.

– Mangi Meli Mandara wa Old Moshi.

– Mmisionari na Mwanataaluma Dr. Bruno Guttman.

– Mangi Abrahamu Salema Mandara wa Old Moshi.

– Mangi Thomas Abraham Salema Mandara wa Old Moshi.

– Mangi Kiting’ati Kirumi wa Kirua Vunjo.

– Mangi Mashingia Kiting’ati wa Kirua Vunjo.

– Mangi Baltazari Mashingia wa Kirua Vunjo.

– Mwanzilishi wa Katoliki Kilimanjaro Askofu Raoul de Courmont.

– Mangi Fumba wa Kilema.

– Mangi Joseph Kiritta wa Kilema.

– Mangi Wilbald Kirita wa Kilema.

– Mangi Aloyce Kiritta wa Kilema.

– Mangi Ndegoruo wa Marealle.

– Gavana wa Kijermani Dr. Karl Peters.

– Mangi Mlang’a Marealle wa Marangu.

– Mangi Petro Itosi Marealle wa Marangu.

– Mangi Augustine Mlang’a Marealle wa Marangu.

– Mangi Kuimbera Mlawi Moshi wa Mamba.

– Mangi Lemnge Kuimbera Moshi wa Mamba.

– Mangi Samweli Weria Kuimbera Moshi wa Mamba.

– Mangi Ndemasi Solomon wa Mwika.

– Mangi Herabdieli Solomon wa Mwika.

– Mangi Herman Tengia wa Keni-Mriti-Mengwe.

– Mangi Wingia Ngache wa Keni-Mriti-Mengwe.

– Mangi Selengia Kinabo wa Mkuu, Rombo.

– Mangi George Selengia Kinabo wa Mkuu, Rombo.

– Mangi Senguo Shirima wa Mashati, Rombo.

– Mangi Edward Latemba wa Mashati, Rombo.

– Mangi John Ndemasi wa Usseri, Rombo.

– Mangi Alfred Salakana Moshi wa Usseri, Rombo.

– Petro Njau, Mwanaharakati wa Taifa la Wachagga.

– Mangi Mkuu wa Wachagga Thomas Lenana Marealle.

– Rais wa Wachagga Eliufoo Solomon.

– Picha za Watu Hao Wote Zimeambatanishwa Kwenye Kitabu cha “Miaka 700 Ya Wachagga” Sambamba na Picha Nyingine Nyingi Muhimu za Maeneo Yenye Umuhimu Mkubwa Kihistoria Katika Kipindi Cha Miaka 700 Ya Wachagga. Baadhi Pia Ya Picha za Mito na Majengo Muhimu Kihistoria Pia Zimeambatanishwa Kwenye Kitabu.

Karibu Kwa Pamoja Tuijenge Jamii Bora Sana Ya Wachagga Inayojitambua Kama Jamii Nyingine Bora Sana za Dunia Hii Kwa Faida Yetu Wenyewe na Tanzania Kwa Ujumla.

Gharama Ya Kitabu Hiki ni Tshs 35,000/=. Kitabu Kimetengenezwa Dar es Salaam Hivyo Kwa Mtu Aliyeko Mbali Atalipia Gharama Za Kusafirisha.

Kama Una Swali Lolote,

Unaweza Kutuma Ujumbe Kwa Whatsapp,

No. +255 754 584 270.

Kulipia.

CRDB BANK,

Acc. No. 01J2030386900.

Jina: SEBASTIAN DASTAN MOSHI.

MPESA.

No. +255 754 584 270.

Jina: SEBASTIAN MOSHI.

Ukikamilisha Malipo,

Tuma Ujumbe wa Muamala Kwa Whatsapp.

No. +255 754 584 270.

Karibu Sana.

You may also like...

Popular Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *