UKOO WA LASWAI.

– Laswai ni ukoo wa wachagga unaopatikana kwa wingi kiasi katika ukanda wa mashariki ya mbali ya Uchagga, Kilimanjaro hususan maeneo ya katikati ya ukanda huu wa mashariki ya mbali ya Uchagga. Wachagga wa ukoo wa Laswai ni watu wachangamfu, wajasiriamali wazuri na baadhi wamefanikisha mambo makubwa sana kwenye maisha.

– Kutoka kwenye historia ukoo wa Laswai unasemekana kuwa ilikuwa ni kama tawi lililotokea kwenye ukoo wa Swai na kuanzisha tawi jipya. Anaeleza Bruno Guttman na Charles Dundas pia kwamba jina kama Laswai, Lashayo au Lamassawe liliashiria kwamba ni mtoto wa kutoka ukoo huo aliyeenda kuanzisha tawi jipya la ukoo eneo lingine. Yaani Laswai ni mtoto kutoka kwa Swai, Lashayo ni mtoto kutoka kwa Shayo, Lamassawe ni mtoto kutoka kwa Massawe n.k.,.

– Ukoo wa Laswai ni mmoja ya koo zenye baadhi ya watu mashuhuri wanaofanya vizuri katika maeneo mbalimbali ndani na nje ya Kilimanjaro na hata nje ya nchi katika kitaaluma na katika ujasiriamali, biashara, kwenye taasisi na mashirika binafsi na hata taasisi za umma na mashirika ya kimataifa.

– Ukoo wa Laswai ni ukoo uliosambaa kiasi upande wa mashariki ya mbalimbali katika maeneo ya katikati ya eneo la Rombo.

– Hivyo ukoo wa Laswai unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Shimbi Kati, Shimbi, Mkuu, Rombo.

– Ukoo wa Laswai unapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Shimbi Mashariki, Shimbi, Mkuu, Rombo.

– Ukoo wa Laswai unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Ibukoni, Mkuu, Rombo.

– Ukoo wa Laswai unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Maharo, Mkuu, Rombo.

– Ukoo wa Laswai unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Makiidi, Mkuu, Rombo.

– Ukoo wa Laswai unapatikana kwa wingi kiasi katika vitongoji vya kata ya Kelamfua, Mkuu Mjini, Rombo.

– Ukoo wa Laswai unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Mokala, Mkuu, Rombo.

– Ukoo wa Laswai unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Ushiri, Ushiri/Ikuini, Mkuu, Rombo.

– Ukoo wa Laswai unapatikana kwa wingi sana sana katika kijiji cha Ubaa, Ushiri/Ikuini, Mkuu, Rombo.

– Ukoo wa Laswai unapatikana kwa wingi sana sana katika kijiji cha Ikuini, Ushiri/Ikuini, Mkuu, Rombo.

Karibu kwa Mchango zaidi wa mawazo au taarifa ya nyongeza juu ya ukoo wa Laswai. Maudhui haya ya ukoo wa Laswai yana lengo la kutoa chachu na kuongeza hamasa zaidi za utafiti na kufahamu zaidi kuhusu ukoo wa Laswai ili kuhifadhi maudhui zaidi kuhusiana na ukoo huu katika maktaba ya ukoo wa Laswai. Maudhui zaidi yana lengo la kuongeza hamasa na kujenga kujitambua sambamba na kujenga mshikamano kwa wanaukoo wa Laswai na wachagga kwa ujumla katika kuelekea kwenye mafanikio makubwa kuanzia katika ngazi ya mtu mmoja mmoja na jamii nzima ya wachagga.

Karibu kwa mchango zaidi wa Mawazo kuhusu ukoo wa Laswai.

1. Je, unafahamu nini kuhusiana na ukoo wa Laswai?

2. Unafikiri ni kijiji gani ambacho kimesahaulika kutajwa lakini kuna ukoo wa Laswai?

3. Kijijini kwenu kuna ukoo wa Laswai?

4. Kama wewe ni wa ukoo wa Laswai una nini cha kutuambia kuhusu ukoo wenu?

5. Huwa mna maadhimisho yoyote au sherehe za ukoo mwezi gani?

6. Wewe ni Laswai wa kutokea kijiji gani?

7. Bado kuna ushirikiano wowote katika matukio mbalimbali muhimu na ndugu zenu wengine wa matawi ya ukoo wa Laswai kutoka maeneo mengine ya Uchaggani?

8. Ni tabia gani unazozifahamu za wachagga wa ukoo wa Laswai?

9. Wanawake wa ukoo wa Laswai huitwaje, na kwa nini?

10. Una rafiki yako yeyote wa kutokea kwenye ukoo wa Laswai?

11. Ni watu gani mashuhuri unaowafahamu kutoka kwenye ukoo wa Laswai?

12. Kuna mnyama yeyote ambaye labda ni mwiko kuliwa na wachagga wa ukoo wa Laswai?

13. Kuna ukoo ambao hawaruhusiwi kuoana na Wako-Laswai kwa sababu zilizowahi kuwepo miaka ya zamani au nyingine zozote?

Karibu kwa Mchango zaidi au maswali.

Ahsanteni.

Kesho tutaendelea na ukoo mwingine.

www.wachagga.com

Urithi Wetu Wachagga (Facebook).

Email: urithiwetuwachagga@gmail.com

Whatsapp +255 754 584 270.

You may also like...

Popular Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *