UKOO WA KISHIMBO.

– Kishimbo ni ukoo mdogo wa wachagga wanaopatikana zaidi katika ukanda wa katikati ya Kilimanjaro katika iliyokuwa himaya ya umangi Mbokomu.

– Ukoo wa Kishimbo licha ya kuwa ni ukoo mdogo lakini ni ukoo wenye watu makini na wasomi wengi wanaofanya vizuri katika nyanja mbalimbali. Ukoo wa Kishimbo haujazungumziwa sana katika kitabu cha “Miaka 700 Ya Wachagga” lakini ni ukoo wenye mchango mkubwa katika historia ya wachagga Kilimanjaro.

Ukoo wa Kishimbo ukiwa ni ukoo unaopatikana katika himaya kongwe na ya wachagga mwanzoni kabisa Kilimanjaro ni kati ya koo zilizokuwa na mainjinia mahiri na mashuhuri wa mifereji zamani maarufu kama “furrow surveyors” ambao walifanya kazi kubwa ya kuimarisha miundombinu bora za umwagiliaji katika iliyokuwa nchi ya wachagga Kilimanjaro. Wachagga wa ukoo wa Kishimbo pia walitoa askari mahiri wa kupambana vitani zamani na hata baadaye.

– Ukoo wa Kishimbo haujasambaa sana na hivyo unapatikana zaidi katika ukanda huu huu wa eneo la katikati ya Uchagga, Kilimanjaro hususan eneo la Mbokomu, Old Moshi.

– Ukoo wa Kishimbo unapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Korini Kati, Mbokomu, Old Moshi.

– Ukoo wa Kishimbo unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Tema, Mbokomu, Old Moshi.

Ukoo wa Kishimbo ni ukoo wa wasomi na watu wengi makini. Hata hivyo huu ni ukoo ambao licha ya kuwa na watu makini bado hakuna maudhui mengi yaliyoandikwa kuhusu ukoo huu. Tunahitaji kufahamu mengi zaidi kuhusu ukoo wa Kishimbo na mchango wake mkubwa katika historia ya Uchagga, Kilimanjaro. Tunahitaji kuhifadhi taarifa na maudhui ya ukoo wa Kishimbo katika maktaba za mitandaoni na maktaba halisi pia kwa faida ya kizazi cha sasa na kinachokuja kujitambua na kujijengea kujiamini zaidi kuelekea kufanya makubwa kwenye maisha katika ngazi ya mtu mmoja mmoja kwenye ukoo, kwenye ngazi ya ukoo na jamii nzima ya wachagga kwa ujumla.

Karibu kwa Mchango zaidi wa mawazo na taarifa zaidi kuhusu ukoo wa Kishimbo.

1. Je, unafahamu nini kuhusiana na ukoo wa Kishimbo?

2. Unafikiri ni kijiji gani ambacho kimesahaulika kutajwa lakini kuna ukoo wa Kishimbo.

3. Kijijini kwenu kuna ukoo wa Kishimbo?

4. Kama wewe ni wa ukoo wa Kishimbo una nini cha kutuambia kuhusu ukoo wenu?

5. Huwa mna maadhimisho yoyote au sherehe za ukoo mwezi gani?

6. Wewe ni Kishimbo wa kutokea kijiji gani?

7. Bado kuna ushirikiano wowote katika matukio mbalimbali muhimu na ndugu zenu wengine wa matawi ya ukoo wa Kishimbo kutoka maeneo mengine ya Uchaggani?

8. Ni tabia gani unazozifahamu za wachagga wa ukoo wa Kishimbo?

9. Wanawake wa ukoo wa Kishimbo huitwaje, na kwa nini?

10. Una rafiki yako yeyote wa kutokea kwenye ukoo wa Kishimbo?

11. Ni watu gani mashuhuri unaowafahamu kutoka kwenye ukoo wa Kishimbo?

12. Kuna mnyama yeyote ambaye labda ni mwiko kuliwa na wachagga wa ukoo wa Kishimbo?

13. Kuna ukoo ambao hawaruhusiwi kuoana na Wako-Kishimbo kwa sababu zilizowahi kuwepo miaka ya zamani au nyingine zozote?

Karibu kwa Mchango zaidi au maswali.

Ahsanteni.

Wiki ijayo tutaendelea na ukoo mwingine.

www.wachagga.com

Urithi Wetu Wachagga (Facebook).

urithiwetuwachagga@gmail.com

Whatsapp +255 754 584 270.

You may also like...

Popular Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *