UKOO WA MAUKI.

– Mauki ni ukoo wa kichagga unaopatikana kwa wingi zaidi katika eneo la ukanda wa katikati, magharibi ya karibu na mashariki ya kati ya Uchagga, Kilimanjaro. Huu sio ukoo wenye idadi kubwa sana ya watu wala wenye umaarufu sana lakini ni ukoo wenye watu makini sana pia. Kutoka kwenye historia ukoo wa Mauki kuna wakati katika karne zilizopita ulisifika kwa kuwa na watu bahili zaidi.

– Wachagga wa ukoo wa Mauki wanapatikana maeneo mbalimbali ndani na nje ya Kilimanjaro na hata nje ya nchi wakifanya vizuri katika tasnia mbalimbali hususan taaluma na biashara. Ukoo wa Mauki umeendelea kukua na kusambaa katika maeneo ya vijiji vingi zaidi Kilimanjaro ambapo kuna maeneo unapatikana kwa wingi kiasi na maeneo mengine kwa uchache.

– Ukoo wa Mauki unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Mrawi, Uru.

– Ukoo wa Mauki unapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Materuni, Uru.

– Ukoo wa Mauki unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Tella, Old Moshi.

– Ukoo wa Mauki unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Kidia, Old Moshi.

– Ukoo wa Mauki unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Shia, Old Moshi.

– Ukoo wa Mauki unapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Sango, Old Moshi.

– Ukoo wa Mauki unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Kyala, Marangu.

Ukoo wa Mauki umezungumziwa kidogo sana katika vitabu vya historia lakini unaonekana ni ukoo wenye historia kubwa nyuma yake ambayo bado haiko wazi sana. Tunahitaji kufahamu zaidi kuhusu ukoo huu wa kichagga ambao unapatikana katika vijiji mchanganyiko bila kujua chimbuko lake halisi. Karibu kwa mchango wa mawazo tuweze kuongeza maudhui zaidi ya ukoo wa Mauki ambayo yatahifadhiwa katika maktaba ya mtandaoni na baadaye katika maktba halisi. Zoezi hili la kuongeza sana maudhui ya koo za kichagga linalenga kujenga hamasa na mshikamano miongoni mwa wanaukoo na jamii nzima ya wachagga kuelekea kujitambua na kutaka kufahamu zaidi chimbuko na asili katika kuongeza zaidi ari na hamasa ya kuyaendea mafanikio makubwa kwa ngazi ya mtu mmoja mmoja na jamii kwa ujumla.

Karibu kwa mchango zaidi wa Mawazo kuhusu ukoo wa Mauki.

1. Je, unafahamu nini kuhusiana na ukoo wa Mauki?

2. Unafikiri ni kijiji gani ambacho kimesahaulika kutajwa lakini kuna ukoo wa Mauki?

3. Kijijini kwenu kuna ukoo wa Mauki?

4. Kama wewe ni wa ukoo wa Mauki

una nini cha kutuambia kuhusu ukoo wenu?

5. Huwa mna maadhimisho yoyote au sherehe za ukoo mwezi gani?

6. Wewe ni Mauki wa kutokea kijiji gani?

7. Bado kuna ushirikiano wowote katika matukio mbalimbali muhimu na ndugu zenu wengine wa matawi ya ukoo wa Mauki kutoka maeneo mengine ya Uchaggani?

8. Ni tabia gani unazozifahamu za wachagga wa ukoo wa Mauki?

9. Wanawake wa ukoo wa Mauki huitwaje, na kwa nini?

10. Una rafiki yako yeyote wa kutokea kwenye ukoo wa Mauki?

11. Ni watu gani mashuhuri unaowafahamu kutoka kwenye ukoo wa Mauki?

12. Kuna mnyama yeyote ambaye labda ni mwiko kuliwa na wachagga wa ukoo wa Mauki?

13. Kuna ukoo ambao hawaruhusiwi kuoana na Wako-Mauki kwa sababu zilizowahi kuwepo miaka ya zamani au nyingine zozote?

Karibu kwa Mchango zaidi au maswali.

Ahsanteni.

Kesho tutaendelea na ukoo mwingine.

www.wachagga.com

Urithi Wetu Wachagga (Facebook).

Whatsapp +255 754 584 270.

You may also like...

Popular Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *