UKOO WA KIMATHI.

– Kimathi ni ukoo mkubwa wa kichagga unaopatikana kwa wingi zaidi katika eneo la ukanda wa magharibi ya karibu ya Uchagga, Kilimanjaro. Wachagga wa ukoo wa Kimathi ni watu wenye bidii kubwa ya maisha na wanapatikana maeneo mbalimbali ndani na nje ya Kilimanjaro na hata nje ya nchi wakifanya vizuri katika maeneo mbalimbali hususan katika biashara na ujasiriamali.

– Ukoo wa Kimathi pia kwa sasa ni ukoo wenye wasomi wengi wanaofanya vizuri katika taasisi mbalimbali za kitaaluma na katika mashirika ya binafsi na ya umma ndani na nje ya nchi. Kutoka kwenye historia kuna taarifa ambazo bado sio za uhakika kwamba ukoo wa Kimathi nao ni tawi la ukoo mkubwa wa Mboro uliovunjika na kuunda matawi mengi sana ya ukoo huu katika maeneo yote ya Uchaggani Kilimanjaro.

– Ukoo wa Kimathi umesambaa kwenye vijiji mbalimbali katika maeneo ya magharibi ya karibu ya Uchagga, Kilimanjaro wakipatikana kwa wingi sana katika baadhi ya vijiji na kwa uchache katika vijiji vingine.

– Hivyo ukoo wa Kimathi unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Uri, Kibosho.

– Ukoo wa Kimathi unapatikana kwa wingi sana sana katika kijiji cha Otaruni, Kibosho.

– Ukoo wa Kimathi unapatikana kwa uchache sana katika kijiji cha Uchau Kaskazini, Kibosho.

– Ukoo wa Kimathi unapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Uchau Kusini, Kibosho.

– Ukoo wa Kimathi unapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Maua, Kibosho.

– Ukoo wa Kimathi unapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Kirima Juu, Kibosho.

– Ukoo wa Kimathi unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Kirima Kati, Kibosho.

– Ukoo wa Kimathi unapatikana kwa uchache sana katika kijiji cha Rau, Uru.

– Ukoo wa Kimathi unapatikana kwa uchache sana katika kijiji cha Kitandu, Uru.

– Ukoo wa Kimathi unapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Kishumundu, Uru.

Karibu kwa mchango wa mawazo kwa wale wenye taarifa zaidi juu ya ukoo wa Kimathi. Tunahitaji kufahamu zaidi kuhusu ukoo wa Kimathi ili kuongeza maudhui ya mtandaoni na baadaye katika maktaba halisi ili kuweza kujenga uelewa zaidi na kujitambua kwa wanaukoo wa Kimathi na wachagga kwa ujumla. Maudhui haya yanalenga kujenga hamasa, umoja na mshikamano miongoni mwa wanaukoo na wachagga kwa ujumla katika kujenga kujiamini kuelekea kufanikisha mambo makubwa katika maisha. Maudhui haya pia yanalenga kujenga misingi sahihi kwa vizazi vinavyofuata kutopoteza asili yao na chimbuko lao pamoja na utambulisha wa ukoo na jamii nzima ya wachagga kwa ujumla.

Karibu kwa mchango zaidi wa Mawazo kuhusu ukoo wa Kimathi.

1. Je, unafahamu nini kuhusiana na ukoo wa Kimathi?

2. Unafikiri ni kijiji gani ambacho kimesahaulika kutajwa lakini kuna ukoo wa Kimathi?

3. Kijijini kwenu kuna ukoo wa Kimathi?

4. Kama wewe ni wa ukoo wa Kimathi

una nini cha kutuambia kuhusu ukoo wenu?

5. Huwa mna maadhimisho yoyote au sherehe za ukoo mwezi gani?

6. Wewe ni Kimathi wa kutokea kijiji gani?

7. Bado kuna ushirikiano wowote katika matukio mbalimbali muhimu na ndugu zenu wengine wa matawi ya ukoo wa Kimathi kutoka maeneo mengine ya Uchaggani?

8. Ni tabia gani unazozifahamu za wachagga wa ukoo wa Kimathi?

9. Wanawake wa ukoo wa Kimathi huitwaje, na kwa nini?

10. Una rafiki yako yeyote wa kutokea kwenye ukoo wa Kimathi?

11. Ni watu gani mashuhuri unaowafahamu kutoka kwenye ukoo wa Kimathi?

12. Kuna mnyama yeyote ambaye labda ni mwiko kuliwa na wachagga wa ukoo wa Kimathi?

13. Kuna ukoo ambao hawaruhusiwi kuoana na Wako-Kimathi kwa sababu zilizowahi kuwepo miaka ya zamani au nyingine zozote?

Karibu kwa Mchango zaidi au maswali.

Ahsanteni.

Kesho tutaendelea na ukoo mwingine.

www.wachagga.com

Urithi Wetu Wachagga (Facebook).

Whatsapp +255 754 584 270

You may also like...

Popular Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *