MAENEO 17 UNAYOHITAJI KUYATEMBELEA UCHAGGANI, KILIMANJARO.

*MAENEO 17 UNAYOHITAJI KUYATEMBELEA UCHAGGANI, KILIMANJARO.*

*1. KANISA KATOLIKI KIBOSHO NA TAASISI ZAKE – KIJIJI CHA SINGA.*

– Hii Ni Parokia Ya Pili Ya Katoliki Kilimanjaro Baada Ya Ile Ya Kilema.

– Ukifika Eneo Hili Ndio Utaelewa Kwa Nini Limekuwa Likizungumzwa Sana na Utafurahia Kulitembelea.

– Ni Eneo Lenye Mazingira Mazuri Sana Kutembelea na Ni Sehemu Pia Unayopata View Nzuri Sana Ya Mlima Kilimanjaro.

KANISA KATOLIKI, PAROKIA YA KIBOSHO SINGA NA TAASISI ZAKE
KANISA KATOLIKI, PAROKIA YA KIBOSHO SINGA NA TAASISI ZAKE
KANISA KATOLIKI, PAROKIA YA KIBOSHO SINGA NA TAASISI ZAKE
KANISA KATOLIKI, PAROKIA YA KIBOSHO SINGA NA TAASISI ZAKE

*2. ENEO LA NKWARUNGO MACHAME NA TAASISI ZAKE – NKWARUNGO, MACHAME*

– Hapa Utakutana na Kanisa La Kwanza La Kilutheri Afrika mashariki na Mazingira Yanayovutia Sana.

– Utakutana na Hospitali Ya Kilutheri Machame Nkwarungo na Maeneo Ya Jirani Kama Nkwamwasi, Kyalia, Wari, Nronga ni Maeneo Yenye Kuvutia Sana.

KKKT, NKWARUNGO, MACHAME
KKKT, NKWARUNGO MACHAME

*3. ENEO LA TSUDUNYI, OLD MOSHI NA MAKUMBUSHO YA MANGI MELI MANDARA – TSUDUNYI, OLD MOSHI.*

– Hili ni Eneo La Kihistoria Zaidi Ambapo Ndio Uliokuwa Mji wa Moshi na Centre Ya Kaskazini Ya Tanganyika Kuanzia Karne Ya 19 Ulipoanzia, Mpaka Baadaye Mwaka 1919 Ulipohamia Rasmi Moshi mjini.

– Kwa Sasa Ndipo Zilipo Ofisi za Halmashauri Ya Wilaya Ya Moshi Vijijini na Ndipo Ilipokuwa Shule Kongwe Ya Sekondari Old Moshi Iliyokuwa Mashuhuri Sana Zamani Kama Sekondari Ya Kwanza Ya Serikali Kaskazini Ya Tanganyika.

– Utakutana Pia na Makumbusho Ya Mangi Meli Mandara Pamoja na Kuangalia Movie(Filamu) Ya Vita Yake na Wajerumani Karne Ya 19. Utaweza Kuona Pia Sanamu Ya Mangi Meli Mandara na Mti Walionyongewa Wamangi wa Kichagga Wakiongozwa na Mangi Meli Mandara Mwaka 1900.

MJI WA ZAMANI WA MOSHI, OFISI ZAUTAWALA
SANAMU YA MANGI MELI MANDARA, TSUDUNYI, OLD MOSHI
TSUDUNYI, OLD MOSHI, MAKUMBUSHO YA MANGI MELI MANDARA

*4. KILIMANJARO NATIONAL PARK, MARANGU GATE – LYASONGORO, MARANGU.*

– Hili Ndilo Lango Kuu na Kongwe Zaidi La Kupanda Mlima Kilimanjaro na Lililozoeleka, Rahisi na Njia Ya Kupanda Mlima Yenye Makazi kwa Kila Kituo.

– Kwenye Eneo Hili Utaweza Kupata Historia na Rekodi Zote za Watalii Waliowahi Kupanda Mlima Kilimanjaro na Pia Unaweza Nawe Kwenda Day Trip Ya Kupanda Mlima Mpaka Maundi Crater, Juu Kidogo Ya Mandara Hut kwa Siku Moja na Kurudi Siku Hiyo Hiyo kwa Gharama Nafuu Sana.

– Ni Eneo Zuri na Linalovutia Sana.

GETI LA MARANGU LA KUPANDA MLIMA KILIMANJARO
GETI LA KUPANDA MLIMA KILIMANJARO KUPITIA MARANGU

*5. CHAGGA ANCIENT CAVES NA NDORO WATERFALLS – LYAMRAKANA, MARANGU.*

– Hapa Utakutana na Historia Fupi Ya Mapango Haya Ya Zamani na Jinsi Yalikuwa Yanatumika Wakati wa Vita.

– Katika Hiki Hiki Kijiji Cha Lyamrakana Utakutana na Maporomoko Ya Maji Yanayovutia Sana Maarufu Kama Ndoro Waterfalls.

MAPANGO YA WACHAGGA YA ZAMANI MARANGU
MAPOROMOKO YA MAJI YA NDORO WATERFALLS, MARANGU

*6. ZIWA CHALLA – MAMSERA CHINI, ROMBO*

– Ziwa Challa ni Ziwa Maarufu Sana na Lenye Kuvutia Sana, Ukilitembelea Unaweza Kufahamu Zaidi na Maajabu Yake. Ni Eneo Linalotembelewa na Watalii Mara kwa Mara Sana.

ZIWA CHALLA, MAMSERA CHINI, ROMBO
ZIWA CHALLA, MAMSERA CHINI, ROMBO

*7. BWAWA LA NDUONI – KIRUA VUNJO*

– Inawezekana Kuna *”Nduwa”* Nyingi Kilimanjaro Kama Zilizopo Huko Vijiji Vya Mmbahe, Marangu na Kwingineko Lakini Tuliweza Kuona Eneo Hili Ni Lenye Kuvutia Zaidi na La Kipekee. Hakuna Uwekezaji Wowote Uliofanyika Mpaka Sasa Lakini Ni Maeneo Unaweza Kutembelea na Kutuliza Sana Akili, na Wenyeji ni Watu Wakarimu Sana.

BWAWA LA NDUONI, KIRUA VUNJO
BWAWA LA NDUONI, KIRUA VUNJO

*8. “CHAGGA LIVE MUSEUM” – KIJIJI CHA KYALA, MARANGU*

– Makumbusho Hii Ya *”Chagga Live Museum”* Iko Pembeni Ya Hotel Ya Kilimanjaro Mountain Resort Karibu na KNCU Kyala.

– Hapa Utakutana na Mzee Maarufu wa Historia za Zamani *”Mzee Mamiro”*, Atakueleza Mambo Kadhaa Ya Kale Kidogo.

CHAGGA LIVE MUSEUM, KIJIJI CHA KYALA MARANGU
CHAGGA LIVE MUSEUM, KIJIJI CHA KYALA MRANGU

*9. MTI MREFU ZAIDI AFRIKA KATIKA MSITU WA KIJIJI CHA TEMA – TEMA, MBOKOMU.*

– Huu Msitu wa Eneo Hili La Mbokomu Ni Msitu Mkubwa, Mnene, Wenye Jiografia Maridadi na Wenye Kuvutia Sana, Kuna Maji Mengi Sana, Kuna Maporomoko Mengi Ya Maji(Waterfalls) na Kuna Unyevu na Manyunyu Ya Mvua Muda Wote. Inawezekana Mbokomu na Marangu Ndio Maeneo Yanayoongoza Kwa Kuwa na Maji Mengi Zaidi.

– Hapa Pia Utakutana na Mti Mrefu Kuliko Yote Afrika Nzima, Wenye Urefu wa Mita 81.5 na Una Umri wa Zaidi Ya Miaka 600. Mti Huu Ambao Kwa Kiswahili Unajulikana Kama *MKUKUSU*, kitaalamu unaitwa *ENTANDROPHRAGMA EXCELSUM*.

MTI MREFU KULIKO YOTE AFRIKA, KIJIJI CHA TEMA, MBOKOMU, OLD MOSHI
MSITU WA MTI MREFU KULIKO YOTE AFRIKA, KIJIJI CHA TEMA, MBOKOMU, OLD MOSHI
MTI MREFU KULIKO AFRIKA NDANI YA MSITU WA MLIMA KILIMANJARO, MBOKOMU, OLD MOSHI

*10. MWEKA KIBOSHO MASHARIKI – MWEKA, KIBOSHO.*

– Eneo hili la Mweka ambayo ndio moja ya njia za kupanda Mlima Kilimanjaro kupitia *”Mweka Route”* lina mazingira yenye kuvutia sana.

– Katika Eneo Hili Ndipo Kwenye Chuo cha Wanyamapori wa Kiafrika cha “Mweka African Wildlife College” na Ni Moja ya Maeneo Unayoweza Kupata Muonekano Bora Sana wa Mlima Kilimanjaro.

– Kwa Sababu Ni Eneo Haliko Mbali na Mjini Watu Wamekuwa Wakitembelea Kupiga Picha na Kufurahia Mandhari Yake.

BARABARA YA KIBOSHO MWEKA
BARABARA YA KIBOSHO MWEKA

*11. KANISA KATOLIKI KILEMA NA TAASISI ZAKE – MKYASHI, KILEMA.*

– Hii Ndio Parokia Ya Kwanza Ya Katoliki Kilimanjaro Iliyoanzishwa na Father August Gommenginger na Moja Ya Maeneo Yenye Historia Kubwa.

– Hapa Utakutana na Shule Kongwe Ya Msingi Kilema Ya Ghorofa Tatu, Chuo cha Ufundi PAPA BRIDGE, Hospitali Ya Kilema, Shule za Msingi na Sekondari, Pamoja na Taasisi Nyingine Nyingi Eneo Moja.

– Ni Eneo Kongwe Lenye Historia Kubwa Unalohitaji Kutembelea.

SHULE KONGWE YA MSINGI KILEMA
KANISA KATOLIKI, PAROKIA YA KILEMA, PAROKIA YA KWANZA KATOLIKI BARA TANGANYIKA

*12. MAPANGO YA SIENYI MACHAME – KIJIJI CHA USWAA NA MASAMA NGIRA, MACHAME.*

– Hili Ni Eneo Linalotisha Zaidi Kuliko Kuvutia Lakini Lenye Mvuto wa Kipekee.

– Eneo Hili Ndipo Inapokutana Mito Miwili Mikubwa Ya Namwi na Marire na Kuwa Mto Mmoja Ambao Mbele Yake Kidogo Unaungana na Mto Mkubwa na Mashuhuri Kikafu Unaoelekea Chini Kwenye Tambarare.

– Eneo Hili Lina Mapango Makubwa Kwa Chini Yanayoenda Umbali Mrefu Yakipita Chini kwa Chini, na Linatambulika Kama Eneo La Mwanzo Zaidi La Makazi Ya Wachagga, Kilimanjaro.

MAPANGO YA SIENYI, MASAMA NGIRA, MASAMA
MAPANGO YA SIENYI, MASAMA NGIRA, MACHAME

*13. KILIMANJARO NATIONAL PARK, MACHAME GATE – NKWESEKO, MACHAME.*

– Hili ni Lango La Kupanda Mlima Kilimanjaro Kupitia Njia Ya Machame Katika Kijiji cha Nkweseko, ni Lango La Pili Kwa Umaarufu Baada Ya Lile Marangu.

– Haya Ni Mazingira Yenye Kuvutia Sana na Yenye Hali Ya Hewa Nzuri Sana. Njia Hii Ya Machame Pia Unaweza Kwenda Day Trip Ya Kupanda Mlima Kilimanjaro na Kurudi Siku Hiyo Hiyo Kwa Gharama Nafuu Sana.

GETI LA MACHAME LA KUPANDA MLIMA KILIMANJARO
GETI LA MACHAME LA KUPANDA MLIMA KILIMANJARO
GETI LA MACHAME LA KUPANDA MLIMA KILIMANJARO

*14. ENEO LA MSITU RONGAI NA GETI LA KUPANDA MLIMA RONGAI ROUTE – RONGAI, ROMBO*

– Huu Msitu wa Rongai ni Moja Ya Maeneo Yenye Kuvutia Sana Kilimanjaro, Ni Moja Kati Ya Njia za Kupanda Mlima Kilimanjaro Kupitia Upande wa Mashariki Kabisa na Ni Maeneo Ya Mpakani Kabisa na Kenya.

– Huu Msitu wa Rongai Ni Mkubwa na Mrefu Ambapo Ukiumaliza Unaingia Mji Mdogo wa Kamwanga Uliopo Mpakani na Wilaya Ya Longido Mkoa wa Arusha.

– Rongai Ni Eneo Lenye Mito na Maji Mengi.

MSITU WA RONGAI, ROMBO
MSITU WA RONGAI, ROMBO

*15. KITIMBIRIHU HOLISTIC CENTRE(ENEO TAKATIFU LA KITIMBIRIHU), KITIMBIRIHU – MDAWI, OLD MOSHI*

– Hili ni Eneo Ambalo Liko Katika Kijiji cha Mdawi, Old Moshi Ambalo Limetangazwa Rasmi na Kanisa La KKKT Kuwa Eneo Takatifu La Kanisa na Mradi wa Ujenzi Huo Unaendelea.

– Hili Ndio Eneo Ambapo Dini Ya Kikristo Ilianzia Rasmi Katika Bara Tanganyika Mwaka 1885. Eneo Hili Pia Ndipo Shule Ya Kwanza Ya Kisasa Ilianzia Katika Bara Tanganyika Kwa Misingi Iliyojengwa Tangu Mwaka 1872.

Sio Eneo Lilioendelea Sana Kwa Sasa kwa Sababu Lilitelekezwa Kutokana na Migogoro Ya Zamani na Ile Misheni Kuhamishwa Lakini Limeanza Kuchangamka Tena, na Kwa Kuwa Wachagga Wengi Ni Wakristo Basi Ni Eneo Lenye Umuhimu Mkubwa Kiimani Kama Sehemu Ambayo Habari za Yesu Zilianza Kutangazwa.

ENEO TAKATIFU LA KITIMBIRIHU HOLISTIC CENTRE
ENEO TAKATIFU LA KITIMBIRIHU HOLISTIC CENTRE

*16. ENEO LA KANISA LA KILUTHERI KOTELA – KOTELA, MAMBA*

– Hili Ni Moja Kati Ya Makanisa Makubwa Sana na Lenye Mvuto wa Kipekee. Pia Ndani Ya Kanisa Hili Ndipo Amezikwa Askofu Mkuu wa Kwanza wa KKKT Dayosisi Ya Kaskazini Ambaye Pia Ndiye Mkuu wa Kwanza wa Kanisa La KKKT Tanzania na Mwanzilishi wa Hospitali Ya KCMC Dr. STEFANO REUBEN MOSHI na mke wake NDEAMBILIASIA MOSHI.

– Pembeni Ya Kanisa Hili Kuna Moja Kati Ya Majengo Makubwa na Mazuri Uchaggani “MAMBA ROYAL COMPLEX” Lenye Ofisi Kadhaa Japo Ni Kijijini.

MAMBA ROYAL COMPLEX
KKKT, USHARIKA WA KOTELA MAMBA

*17. KANISA LA KKKT MWIKA NA TAASISI ZAKE – MWIKA.*

– Hili Eneo La Mwika Ni Kati Ya Maeneo Yenye Mazingira Yanayovutia Sana, Ni Eneo Lenye Taasisi Nyingi Hasa za Kanisa La Kilutheri. – Katika Eneo Hili Kuna Chuo Kikuu cha Kumbukumbu Ya ASKOFU STEFANO MOSHI, Kampasi Ya Mwika, Kuna Mwika Bible School, Chuo cha Uinjilisti Mwika, Kuna Christian Bookshop Mwika, Kanisa Lenyewe, Shule Ya Msingi na Taasisi Nyingine.

– Ni Eneo Lenye Mandhari Bora Sana.*Maeneo Haya 17 Tumeona Ni Maeneo Muhimu Zaidi Unayohitaji Kuyatembelea Kwa Ziara Tuliyofanya, Lakini Unaweza Kuongezea Maeneo Mengine Zaidi Unayofikiri Yastahili Kuwepo Kwenye Orodha Hii.

KKKT, USHARIKA WA MWIKA, MWIKA
CHUO KIKUU CHA KUMBUKUMBU YA STEFANO MOSHI

*Karibuni Kwa Maoni Au Nyongeza

Urithi Wetu Wachagga

urithiwetuwachagga@gmail.com

You may also like...

Popular Posts

13 Comments

 1. Ndugu;

  Kazi mliyofanya ni kubwa sana inayostahili pongezi.

  Hapa mnahifadhi historia ya sehemu muhimu sana ya nchi yetu kwa namna nyingi yaani kujikomboa kiuchumi(KNCU), ki-elimu, ki-tamaduni n.k.

  Binafsi nimekuwa nikifikiri ni namna gani historia ya Wachagga inaweza kutunzwa. Kuna wakati unafikiria labda tungekuwa na museum n.k.

  Mmeonyesha njia kwamba tunaweza kuhifadhi historia, utamaduni, hatua za maendeleo Uchaggani kwa kutumia njia ya kisasa ya Website.

  Binasfi nitakuwa nawatumia chochote kuhusu Kilimanjaro na hasa watu wake katika miteremko ya Mlima.

  Hivi karibuni niliwatumia Thesis iliyofanywa huko Marekani kuhusu Joseph Merinyo ambaye alikua muhimu sana katika kuwakomboa Wachagga kukiwepo kuanzisha chama cha ushirika KNCU.

  Pongezi nyingi sana na ahsanteni.

  Arnold

  Dar es Salaam

  1. Ahsante sana kaka. Karibu sana.

  2. Ahsante sana kaka.

   Tunashukuru sana kwa kujali na mchango wako.

   Tuko pamoja kaka.

   1. Gregory Eliufoo Urima Mboro says:

    Binafsi, nimesoma habari juu ya kabila langu na kweli najivunia kuwa sehemu yake. Nashukuru sana kwa jitihada hii kubwa mliyofanya na inayohitaji kweli kuungwa mkono. Nimehamasishwa sana kufanya ziara sehemu zote hizo. Nimezaliwa Moshi nimekulia na kusoma huko, nimeenda baadhi ya sehemu lakini nikiri sihufahamu mkoa wangu vizuri. Ni mtu mzima na nina familia, naishi Dar kwa sasa. Ninayo kazi muhimu ya kufanya kwa ajili ya ustawí wa kizazi changu. Nawashukuruni sana kwa mara nyingine.

    1. Ahsante sana, karibu sana.

 2. Pia waterfalls kama Ndoro kilasiya kinukamori ghona nk

  1. Sawa, karibu sana.

 3. fredy joas mlay says:

  kiukweli leo nimefarijika saana kuona napata maeneo maalum na historia zake za nyumbani kwetu nimefurahi saaan hongera kwa kazi nzuri kuna maeneo cijawah fika kwa historia hii nzuri na hadith yake ntaanza kuyatembelea umesahau maeneo
  1 kinuka mori water fals
  2 klyasia water fals
  4 maeneo mazuri ya kwa mangi mariale
  na kuna mapango yako marangu hapo

  1. Ahsante sana.

   Karibu sana kaka.

   1. fredy joas mlay says:

    MKO VIZURI IKIWEZEKANA PIA TUTENGENEZE KITABU CHENYE HISTORIA YA WACHAGA NA TAMADUNI ZETU.. WATOTO NA WAJUKUUU WAJE WAKUTE ……
    .. AMA MAKITABA NDOOGO ENEO LA MARANGU MTONI LENYE VITABU NA VITU VTA ASILI VYA KICHAGA AMABAPO WATU WAKITEMBELEA WATAKUWA WANA CHANGIA KIAS KWA AJILI YA MUENDELEZO wa vitu vyetu vya asili i’m proud to be chaga

    1. Kitabu kipo kinaitwa “Miaka 700 Ya Wachagga”, Karibu +255 754 584 270

 4. Mkoa vizuri sana katika kutupa habari za kale ambazo kimsingi zinatujenga na kutuimarisha kama itapendeza tuwe na kitabu chenye historia ya wachaga hii itatusaidia kurithisha tamaduni zetu kizazi na kizazi

  1. Kipo kitabu cha historia kinaitwa “Miaka 700 ya Wachagga”, tucheki whatsapp +255 754 584 270.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *