TUMEMALIZA!

TUMEMALIZA!

Tumehitimisha Ziara Iliyoanza Septemba 2020 Mpaka Aprili 2021 Ya Kufikia Kila Kijiji Cha Uchagga, Kilimanjaro.

Tunashukuru Kwamba Kwa Ziara Hii Tumeweza Kufika Vijiji Vyote na Kuwaletea 98% Ya Vijiji Vyote Vya Kilimanjaro, Pamoja na Vitu Muhimu Vilivyopo(Landmarks), Japo Kwa Sababu Ya Ugeni Mwanzoni Kuna Baadhi Ya Vijiji Vichache Tulipata Changamoto Ya Kuchukua Picha Hivyo Havijaweza Kuonekana Hapa Lakini Angalau Kuna Vijiji Vya Jirani.

Lengo La Ziara Hii Ilikuwa Ni Kufika na Kuyafahamu Maeneo Muhimu Kihistoria Kilimanjaro, Kuifahamu Kilimanjaro Kwa Undani na Hali Yake Ya Sasa, Kufahamu Hali Ya Kimazingira Ya Utalii wa Ndani Ya Kilimanjaro na Kuileta Kilimanjaro Kwa Wachagga.

Wachagga Wengi Hawaijui Kilimanjaro Zaidi Ya Eneo Analotoka, Tena Wengi Ni Kile Kijiji Tu Anachotokea na Wengine Ni Ule Mtaa Anaotokea Peke Yake, Sasa Ni Vigumu Kuwa Na Uzalendo au Kupenda Kitu Usichokifahamu. Hivyo Ziara Hii Pia Ililenga Kuwahamasisha Wachagga Kuitembelea na Kuifahamu Kilimanjaro Au Angalia Kutembelea Maeneo Muhimu Kihistoria na Yale Yenye Kuvutia Sana.

Kwetu Sisi Ni Ziara Ambayo Ilikuwa na Changamoto Kiasi, Iliyochosha Lakini Inayovutia, Iliyogharimu Sana Rasilimali Muda na Fedha Lakini Iliyoweza Kutoa Thamani Iliyostahili, Waingereza Wanasema “It’s Worth it”.

Tulipata Usumbufu Kiasi Baadhi Ya Maeneo, Tulipoteza Baadhi Ya Vifaa na Nyaraka Muhimu Maeneo Mengine Lakini Kote Tulifanikiwa Kuvuka na Kufikia Lengo Ambalo Hatukua na Uhakika Kama Tutamaliza Wakati Tunaanza. Mpaka Kumaliza Ziara Hii Tumepata Uelewa wa Tofauti Kabisa Juu Ya Kilimanjaro Tofauti na Ule Tuliokuwa Nao Mwanzoni Wakati Tunaanza. Umuhimu wa Ziara Hii Utaendelea Kuonekana Huko Mbele Zaidi.

Sasa Naomba Tushirikiane Katika Kujadili Mambo Mbalimbali Kuhusu Ziara Hii Kadiri Ya Tulivyoweza Kushirikishana Yale Tuliyokutana Nayo Kwenye Makala Zitakazokuwa Zinaendelea.

Karibuni Kwa Maoni.

ZIARA YA VIJIJI VYOTE VYA UCHAGGANI KILIMANJARO

You may also like...

Popular Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *