UKOO WA MEENA.

– Meena ni ukoo wa wachagga wanaopatikana katika baadhi ya vijiji vya Uchagga, Kilimanjaro upande wa magharibi ya Kilimanjaro na baadhi ya vijiji upande wa mashariki pia. Huu ni ukoo wenye idadi kiasi cha watu ambao wamesambaa maeneo mbalimbali na wanafanya vizuri sana katika taaluma na biashara mfano Prof. Ruth Meena wa chuo kikuu cha …

UKOO WA KIMARIO.

– Kimario ni moja kati ya koo kubwa na maarufu sana za kichagga unaopatikana kwa wingi upande wa mashariki kabisa ya Uchaggani, Kilimanjaro. Huu ni ukoo wenye watu wengi wanaopatikana ndani na nje ya Kilimanjaro. Ukoo huu wa Kimario unasemekana kwamba ndio uliozaa ukoo wa Utou wa huko Rombo, yaani ukoo wa Utou wa Rombo …

UKOO WA MCHAU.

– Mchau ni ukoo maarufu wa wachagga ulioenea katika vijiji vingi mbalimbali vya Kilimanjaro japo sio kwa wingi sana. Ukoo huu unapatikana kwa wingi kuanzia upande wa katikati magharibi ya wachagga mpaka katikati mashariki ya Uchagga. Wachagga wa ukoo wa Mchau ni watu makini na kuna wasomi wengi wa fani mbalimbali wanaofanya vizuri katika taaluma …

UKOO WA KINYAHA.

– Ukoo wa Kinyaha ni ukoo unaopatikana kwa uchache sana Uchaggani katika maeneo ya katika ya Uchagga. Huu ni ukoo wenye watu wengi makini na wanaofanya vizuri sana kitaaluma wakiwa wanafanya vizuri sana katika taasisi mbalimbali ndani na nje ya Kilimanjaro na hata nje ya nchi. – Kutoka kwenye historia ukoo wa Kinyaha unafahamika kwamba …

UKOO WA MSAKI.

– Msaki ni ukoo wa wachagga wanaopatikana kwa wingi katika eneo la katikati ya kuelekea mashariki ya Uchagga, Kilimanjaro. Ukoo wa Msaki ni ukoo mkubwa uliosambaa katika vijiji vingi vya Uchagga, Kilimanjaro katika maeneo ya katikati kuelekea mashariki. – Ukoo wa Msaki ni ukoo wenye vipaji mbalimbali hivyo una watu wengi wanaofanya vizuri katika nyanja …

UKOO WA MEELA.

– Meela ni ukoo maarufu wa wachagga unaopatikana kwa wingi maeneo ya Uchaggani kati kuelekea mashariki. Huu ni ukoo uliosambaa katika vijiji mbalimbali vya maeneo haya. Hata hivyo japo sio ukoo uliosambaa maeneo mengi sana lakini ukoo wa Meela ni ukoo wenye watu wengi mashuhuri wanaofanya vizuri sana katika nyanja mbalimbali ndani na nje ya …