UKOO WA MEENA.

– Meena ni ukoo wa wachagga wanaopatikana katika baadhi ya vijiji vya Uchagga, Kilimanjaro upande wa magharibi ya Kilimanjaro na baadhi ya vijiji upande wa mashariki pia. Huu ni ukoo wenye idadi kiasi cha watu ambao wamesambaa maeneo mbalimbali na wanafanya vizuri sana katika taaluma na biashara mfano Prof. Ruth Meena wa chuo kikuu cha Dar es Salaam ambaye ni mwanaharakati mashuhuri wa mambo ya usawa wa kijinsia.

– Baadhi wa watu wamekuwa wakiuliza kama kuna uhusiano wowote kati ya ukoo wa Meena na ukoo wa Meela. Bado hatujapata taarifa zozote zinazoonyesha kama kuna uhusiano baina ya koo hizi mbili lakini wahusika wenyewe hususan wazee wa zamani wanaweza kuwa na majibu angalau hata ya mapokeo juu ya hilo.

– Ukoo wa Meena umesambaa na unapatikana katika maeneo ya vijiji mbalimbali ya Uchagga kwa wingi kwa baadhi ya vijiji na kwa uchache kwenye vijiji vingine.

– Ukoo wa Meena unapatikana kwa uchache katika kijiji cha Nkwansira, Masama.

– Ukoo wa Meena unapatikana kwa uchache katika kijiji cha Mbosho, Masama.

– Ukoo wa Meena unapatikana kwa uchache katika kijiji cha Mudio, Masama.

– Ukoo wa Meena unapatikana kwa kiasi katika baadhi ya vijiji vya Kata ya Lyamungo, Machame.

– Ukoo wa Meena unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Roo, Masama.

– Ukoo wa Meena unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Foo, kitongoji cha Nkweseko, Machame.

– Ukoo wa Meena unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Foo, kitongoji cha Nkwarungo, Machame.

– Ukoo wa Meena unapatikana kwa wingi sana sana sana katika kijiji cha Lekura, Mamba.

– Ukoo wa Meena unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Kimangaro, Mwika.

Tunahitaji taarifa zaidi kuhusiana na ukoo wa Meena ambao bado hatujaweza kufahamu kwa undani chimbuko lake na matazamo wa wahusika juu ya wao wenyewe. Taarifa zaidi juu ya ukoo wa Meena zitasaidia kuongeza maudhui ya ukoo huu sambamba na kuhamasisha utamaduni wa kujali kuhusu kule watu walipotoka.

Karibu kwa mchango zaidi wa Mawazo kuhusu ukoo wa Meena.

1. Je, unafahamu nini kuhusiana na ukoo wa Meena?

2. Unafikiri ni kijiji gani ambacho kimesahaulika kutajwa lakini kuna ukoo wa Meena?

3. Kijijini kwenu kuna ukoo wa Meena?

4. Kama wewe ni wa ukoo wa Meena una nini cha kutuambia kuhusu ukoo wenu?

5. Huwa mna maadhimisho yoyote au sherehe za ukoo mwezi gani?

6. Wewe ni Meena wa kutokea kijiji gani?

7. Bado kuna ushirikiano wowote katika matukio mbalimbali muhimu na ndugu zenu wengine wa matawi ya ukoo wa Meena kutoka maeneo mengine ya Uchaggani?

8. Ni tabia gani unazozifahamu za wachagga wa ukoo wa Meena?

9. Wanawake wa ukoo wa Meena huitwaje, na kwa nini?

10. Una rafiki yako yeyote wa kutokea kwenye ukoo wa Meena?

11. Ni watu gani mashuhuri unaowafahamu kutoka kwenye ukoo wa Meena?

12. Kuna mnyama yeyote ambaye labda ni mwiko kuliwa na wachagga wa ukoo wa Meena?

13. Kuna ukoo ambao hawaruhusiwi kuoana na Wako-Meena kwa sababu zilizowahi kuwepo miaka ya zamani au nyingine zozote?

Karibu kwa Mchango zaidi au maswali.

Ahsanteni.

Kesho tutaendelea na ukoo mwingine.

www.wachagga.com

Urithi Wetu Wachagga (Facebook).

Whatsapp +255 754 584 270.

You may also like...

Popular Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *