“THE JEWISH PHENOMENON” #SEHEMU YA 3#

“THE JEWISH PHENOMENON”

#SEHEMU YA 3#

HISTORIA YA KALE YA WAYAHUDI TANGU NYAKATI ZA BIBLIA

Waebrania, Waisrael au Wayahudi ni maneno ambayo yamekuwa yakitumika kuwatambulisha.

Israel ndio jina lililokuwa linatumiwa na mjukuu mwingine wa Ibrahim aliyeitwa Yakobo, na kisha watoto kumi na mbili wa Yakobo ndio walikuja kuitwa watoto wa Israel au Taifa la Israel.

Neno Uyahudi/Jew lilitokana na Yuda ambaye ni mmoja kati ya watoto wa Israel/Yakobo ambaye alikuwa mashuhuri sana.

Neno Uyahudi lilikuja kuwa jina maarufu kwa Waisrael wote baada ya mwaka 722 KK Kabla ya Kristo pale ambapo watu wa kabila au kizazi cha Yuda pekee waliposamilimika wakati makabila yote ya Israel yakipelekwa utumwani. Baadaye mpaka leo wanaitwa kabila zima likaitw Wayahudi, Imani yao inaitwa Uyahudi, lugha yao inaitwa kiebrania na nchi yao ya asili inaitwa Israel.

Nchi ya asili ya Israel kuna nyakati imekuwa chini yao na kuna nyakati nyingine imekuwa ikikaliwa na watu wengine.

Nyakati ambazo wamekuwa uhamishoni na nyakati walizorudi katika nchi yao zimetengeneza matukio mbalimbali wanayoyasherehekea katika sherehe zao mbalimbali za mwaka.

MATUKIO YANAYOAZIMISHWA KWENYE SHEREHE ZA WAYAHUDI.

MAAZIMISHO YA SHEREHE YA “PASSOVER”

Mwandishi anasema mwaka 1,300 Kabla ya Kristo wayahudi walichukuliwa utumwani Misri na kutumikishwa na Farao, hadithi hii ipo katika biblia kwenye kitabu cha kutoka.

Inasemekana kwa mujibu wa biblia Mungu alimtuma Musa kwenda kuwakomboa wana wa Israel kutoka utumwani Misri lakini Farao alikaidi amri ya Mungu mpaka Mungu alipomtumia mapigo kumi yaliyopelekea mwishowe akakubali kuwaachia wana wa Israel kuondoka Misri.

Tukio hili la kuachiwa kutoka utumwani Misri wayahudi wanaliazimisha katika sherehe zao za kila mwaka ambalo wao wanaliita “Passover”.

MAAZIMISHO YA SHEREHE YA PURIM

Mwaka 480 Kabla ya Kristo dola ya Uajemi/Persian empire ambayo ilikuwa imeiangusha dola ya Babeli ilikuwa inaongozwa na Mfalme Artashasta ambaye aliachana na mke wake aliyekuwa na kiburi na jeuri na kuamua kumuoa Esta, mwanamke wa kiyahudi.

Waziri Mkuu wa Mfalme Artashasta aliyekuwa anaitwa Hamani alikosa maelewano na Modekai, Myahudi ambaye ni baba mlezi wa Esta kwa sababu aligoma kumsujudia Hamani, hivyo Hamani alipanga kumuangamiza Modekai.

Namna ambayo Hamani aliibuni ya kumuangamiza Modekai ni kutafuta ruhusu kwa mfalme wa Uajemi ya kuwaangamiza Wayahudi wote, hivyo alimshawishi mfalme wa Artashasta wa Uajemi kwamba Wayahudi wana miongozi yao ya kidini isiyoendana na sheria za Uajemi hivyo hawana heshima kwa utawala wa mfalme Artashasta na hivyo wanapaswa waangamizwe na mfalme Artashasta alishawishika na madai ya Hamani na hivyo kutoa ruhusa.

Modekai alijaribu kuongea na Esta kwamba aangalie namna atawatetea wayahudi katika hilo. Esta aliandaa karamu na kumkaribisha mfalme ambaye alikuwa ni mume wake na kufikisha malalamiko yake mbele za mfalme na mbele za watu wote.

Mfalme alipoelezwa kwamba Wayahudi ni watu wazuri na Hamani ni mchonganishi na mpuuzaji aliamua kumgeuzia kibao Hamani kibao na badala ya wayahudi kuangamizwa Hamani na familia yake ndio waliouawa.

Japo wanahistoria wengi mashuhuri wanasema kwamba hii hadithi ni ya kutunga na haina ukweli, lakini ni moja kati ya matukio makubwa ya mwaka yanayosherehekewa na wayahudi maarufu kama “Purim”, ambapo wanasherehekea ile karamu aliyoiandaa Esta iliyoweza kuwaokoa wayahudi na adhabu ya kifo iliyokuwa imepitishwa na mfalme wa dola ya Uajemi, mfalme Artashasta.

MAAZIMISHO YA SHEREHE YA HANUKA.

Mwaka 165 Kabla ya Kristo Mfalme wa Syria aliyeitwa Antiokasi aliiangusha Israel na kuitawala kwa nguvu na kuwazuia wayahudi kuabudu dini yao, akalifunga hekalu la Yerusalemu na kuzima mishumaa yote iliyokuwa inawaka hekaluni.

Baada ya Wayahudi kuzuiwa kumuabudu Mungu hekaluni Yuda Makabii aliongoza jeshi la Wayahudi kupambana na wasyria na kuwashinda vita na kurudisha upya utawala wa kiyahudi Israel na kulifungua upya hekalu. Sherehe hii inasherehekewa na Wayahudi kila mwaka maarufu kama sherehe za Hanuka menorah.

Mwandishi anasema sherehe hizi tatu kwa Wayahudi zinalenga kuwaamsha Wayahudi kwamba muda wowote wanatakiwa wawe tayari kwa mapambano na kukabiliana na hatari inayoweza kujitokeza dhidi yao.

Itaendelea kwenye makala inayofuata

Urithi Wetu Wachagga

urithiwetuwachagga@gmail.com

You may also like...

Popular Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *