“THE JEWISH PHENOMENON” “SEHEMU YA 4”

“THE JEWISH PHENOMENON”

“SEHEMU YA 4”

HISTORIA YA WAYAHUDI KUANZIA MIAKA 2,000 ILIYOPITA.

Mwandishi anasema historia mpya ya Wayahudi inaanzia mwaka 70 Kabla ya Kristo wakati majeshi ya dola ya Rumi yaliyokuwa yakiongozwa na Jenerali Pompey yalipoivamia Yerusalemu na kuiangusha, yakalivunja hekalu na kuwaondoa kabisa wayahudi kutoka nchi yao takatifu ya ahadi Israel ambapo walitawanyika maeneo mbalimbali ya dunia.

Mwandishi anasema kwamba Warumi waliipa nchi ya Israel jina jipya la Palestina na baada ya hapo imechukua karibu miaka 2,000 nchi ya Israel kuja kuanzishwa tena mwaka 1948.

Baada ya dola ya kidikteta ya Rumi ambayo ilikuwa inatawala sehemu kubwa ya Ulaya, mashariki ya kati na kaskazini ya Afrika kukua sana, ukristo na uyahudi zilikuwa ni kati ya dini maarufu ndani ya himaya yote iliyokuwa chini dola ya Rumi.

Mkuu wa dola ya Rumi/Roma, Emperor Constantine alibadili dini na kuwa mkristo na mwaka 300 Baada ya Kristo alitoa amri kwamba ukristo ndio itakuwa dini rasmi ya Dola Takatifu Ya Rumi/Holy Roman Empire ambayo ilikuwa inatawala karibu Ulaya yote, baadhi ya maeneo ya mashariki ya kati na kaskazini mwa Afrika yaani dunia ya magharibi kwa ujumla.

Dola ya Rumi/Roman empire iliwalazimisha watu wote aidha wakubali kubadili dini na kuwa wakristo au wakikaidi wauawe. Wayahudi hawakubadili na badala yake kwa siri waliendelea na dini yao ya kiyahudi, mavazi, desturi zao, vyakula na lugha yao popote walipoishi duniani.

Matokeo yake wayahudi walijikuta wakiishi kwa kujitenga na watu wengine na hili likapelekea wao kuhisiwa vibaya na watu wa jamii nyingine na kusingiziwa kwamba wanahusika na majanga mengi yanayotokea kwenye jamii kama vile magonjwa mbalimbali yanayotokea na matatizo ya kiuchumi yaliyopo.

Zilizuka tetesi kwamba wayahudi walikuwa wakitengeneza mikate yao ya mana kwa kutumia damu za watoto wachanga wa kikristo na hivyo ilikuwa ikitokea mtoto mdogo mkristo amekutwa amefariki sehemu yoyote basi alikamatwa myahudi yeyote aliyehisiwa kuhusika na kifo hicho na kupewa mateso makali mpaka akiri kwamba yeye ndiye aliyemuua na kisha kuhukumiwa.

Katika miaka ya katikati mpaka kufikia karne ya 14 wayahudi walikuwa wakiishi kwa wingi katika nchi za Hispania, Italia, Ujerumani, Ufaransa na Ulaya mashariki hasa Poland na Urusi.

Serikali za Ulaya ziliwapiga marufuku wayahudi kumiliki ardhi hivyo wachache sana walifanya kilimo na badala yake wengi walijiingiza kwenye biashara na viwanda.

Wayahudi walipata mafanikio na waliwekewa kodi nyingi katika nyanja nyingi za kimaisha na watawala walinufaika sana na biashara zao.

“WAYAHUDI NDANI YA MAREKANI”

Mwandishi Steven Silbiger anasema wayahudi wa mwanzo zaidi walifika Marekani mwaka 1654 wakitokea Brazili baada ya Brazili kuanza kutawaliwa na Wareno, ambapo badala ya kurudi Ulaya waliamua kwenda Marekani.

Lakini mpaka kufikia mwishoni mwa miaka ya 1700 bado wayahudi walikuwa ni wachache sana Marekani lakini hata hivyo mwandishi anasema walipewa uhuru mkubwa wa kuabudu katika dini yao tofauti na Ulaya ambapo walikuwa wakichukiwa sana jamii za wakristo wa Ulaya na kunyimwa haki nyingi za msingi kwao.

Ndani ya Marekani wayahudi walipewa haki sawa na wakristo na baadaye Ufaransa baada ya mapinduzi ya Ufaransa ya mwaka 1791 yaliyoondoa utawala wa kifalme, Ufaransa ikawa ni nchi ya kwanza Ulaya kuwapa wayahudi haki sawa na jamii nyingine za wakristo.

Wayahudi waliokuwa wanaishi kwa wingi Ulaya hasa Ujerumani walihamia Marekani kwa wingi sana mwanzoni mwa miaka ya 1800. Walianzisha biashara nyingi sambamba na viwanda vya kutengeneza nguo na walitajirika sana na kuwa na nguvu kubwa za kiuchumi licha ya kwamba mpaka kufikia mwaka 1880 wayahudi walikuwa 250,000 peke yake ndani ya Marekani iliyokuwa na watu zaidi ya milioni 50 kwa wakati huo.

Kuanzia miaka ya 1880’s wayahudi wengi sana walihamia Marekani. Licha ya kwamba mwanzoni Marekani wayahudi walikuwa ni wachache lakini mpaka kufikia wakati wa vita ya kwanza ya dunia zaidi ya wayahudi milioni 2 au theluthi moja ya wayahudi waliokuwa wanaishi Ulaya walikuwa wamehamia Marekani.

Baadaye Urusi iliivamia Poland na nchi nyingine za Ulaya mashariki na hivyo wayahudi waliokuwepo Ulaya mashariki walikaa chini ya utawala wa kimabavu wa Urusi na Warusi hawakuwataka wayahudi hivyo walianzisha kampeni ya aidha kuwabidilisha dini kwa lazima au kuwaua.

Wayahudi zaidi walikimbilia Marekani na kupitia taasisi za kiyahudi ambazo walikuwa wameanza kuzianzisha Marekani walisaidiana sana katika kuinuana kiuchumi na kuzidi kuwa na nguvu kubwa zaidi za kiuchumi ikiwemo kupeana ajira katika viwanda vya nguo walivyokuwa wameanzisha na vilivyokuwa vinakuwa kwa kasi sana.

Uhamiaji mkubwa wa mwisho wa Wayahudi kutoka Ulaya kuhamia Marekani ni ule uliotokea baada ya vita ya pili ya dunia ambapo majeshi ya kinazi ya dikteta wa ujerumani Adolf Hitler yalipofanya mauaji makubwa ya kutisha kwa jamii ya wayahudi ndani ya Ulaya ambapo waliuawa wengi sana ambapo mauaji haya yaliokuwa maarufu kama “Holocaust” yanakadiriwa kufikia takriban milioni 6.

Wayahudi zaidi ya milioni 1 walihamia Marekani wakati huu wa vita ya pili ya dunia kukimbia mkono wa chuma wa dikteta wa Ujerumani Adolf Hitler aliyekuwa ameangusha sehemu kubwa ya Ulaya.

Kuanzia taifa la Israel limeanzishwa wameshakutana na vita kubwa tatu ambazo zingeweza kuisambaratisha kabisa nchi ya Israel lakini wamefanikiwa kushinda zote.

Nchi ya Israel ikiwa imezungukwa na mataifa ya kiarabu ambao ni adui zao wakubwa wamekuwa kwenye hatari ya kusambaratishwa na mara tatu kuanzia nchi yenyewe ya Israel ilipozaliwa upya mwaka 1948.

Mara ya kwanza ni mwaka 1948 yenyewe mataifa ya kiarabu yalipfanya jaribio la kwanza wakiwa hawakubaliana na nchi hiyo ya Israel, mara ya pili ni mwaka 1967 walipopigana vita ya siku 6 na mataifa ya kiarabu na Israel kuibuka washindi na mara ya tatu ni mwaka 1973 walipopigana vita ya Yom Kippur.

Miaka ya 1980’s na 1990’s wayahudi wachache waliendelea kuhamia Marekani kutokea nchi zilizokuwa kwenye Umoja wa Kisovieti zikiongozwa na Urusi wanaokadiriwa kufikia takriban 200,000. Sasa twende tukaangalie siri saba zilizowafanya wayahudi kuwa na mafanikio makubwa ndani ya Marekani.

Ahsanteni.

Itaendeleo kwenye makala inayofuatia.

Urithi Wetu Wachagga

urithiwetuwachagga@gmail.com

You may also like...

Popular Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *