UKOO WA LYARUU.

– Lyaruu ni ukoo wa kichagga unaopatikana kwa kiasi katika vijiji vichache vya maeneo ya ukanda wa mashariki ya kati ya Uchagga, Kilimanjaro. Ukoo wa Lyaruu ni ukoo mdogo lakini wenye watu wengi makini wanaofanya vizuri katika tasnia mbalimbali ndani na nje ya Kilimanjaro na hata nje ya nchi kuanzia kwenye taaluma, biashara na ujasiriamali. …

UKOO WA RIMOY.

– Rimoy ni ukoo wa wachagga wanaopatikana kwa wingi zaidi katika eneo la himaya ya umangi Kilema. Huu ni ukoo ambao sio mkubwa sana wala maarufu sana lakini ni ukoo wa watu mashuhuri wanaofanya vizuri sana kwenye masuala ya biashara na ujasiriamali. Ukoo wa Rimoy ni ukoo wa watu wenye kujiamini na wengi wenye hadhi …

UKOO WA UISSO/OISSO/WOISSO

– Uisso ni ukoo mkubwa wa kichagga unaopatikana kwa wingi katika maeneo ya ukanda wa mashariki ya kati ya Uchagga, Kilimanjaro na kwa wingi zaidi katika eneo la ukanda wa mashariki ya mbali ya Uchagga, Kilimanjaro. Huu ni ukoo wa watu wajasiri na wenye kujiamini sana katika mapambano ya aina yoyote ile. Ukoo wa Uisso/Oisso/Woisso …

HATA BILA UKOLONI WALA UJIO WA DINI ZA KIGENI WACHAGGA WANGEENDELEA KUWA BORA ZAIDI NA ZAIDI (KUSTAARABIKA).

– Moja kati ya maneno ambayo huwa yananipa ugumu au ukakasi sana kuyatumia ni pamoja na neno hili “ustaarabu” kutokana na asili ya neno lenyewe. Naamini wote tunajua maana ya neno ustaarabu kwamba ni kuishi au kuwa na utamaduni ambao unaonekana kuwa ni wa hadhi ya juu zaidi katika maisha, au kama unavyojulikana kwa kiingereza …