UKOO WA TARIMO.

– Tarimo ni ukoo mkubwa sana, maarufu sana na mashuhuri sana katika historia ya wachagga Kilimanjaro. Huu ni ukoo ambao umekuwa ukoo mama kwa baadhi ya koo na ni moja kati ya koo zinapatikana karibu kila mahali Uchaggani. Ukoo wa Tarimo ni mkongwe sana na unafahamika kusambaza vizazi vyake katika maeneo mengi ya Uchagga tangu karne nyingi zilizopita na hata kuzalisha watawala wa maeneo mengi.

– Kutoka kwenye historia ukoo wa Tarimo umekuwa ni ukoo wenye ushawishi mkubwa katika vijiji vingi vya Uchagga. Kwa kuanzia ukoo wa Tarimo ulikuwa ndio ukoo wenye nguvu na kutawala katika kijiji cha Tsudunyi, Old Moshi huku ukiwa na nguvu sana pia katika kijiji cha Tella, Old Moshi walikohamia ndugu wengine kutokea Tsudunyi na kusambaa kuelekea upande wa magharibi. Ukoo huu wa Tarimo ulielekea upande wa magharibi zaidi na kuweka makazi ya mengine na kutawala katika himaya ndogo ya Mweka, Kibosho.

– Inasemekana kwamba ni tawi la ukoo huu wa Tarimo kutokea katika kijiji cha Tella, Old Moshi lililoenda kutawala katika himaya ndogo ya Mweka, Kibosho ambayo baadaye ilikuja kufanya kuwa sehemu ya Kibosho na kutawaliwa kutokea Kibosho. Kisha tawi lingine la ukoo huu wa Tarimo inasemekana lilielekea upande wa mashariki wa Uchagga na kuweka makazi ya kudumu maeneo ya mashariki kabisa ya Rombo. Ukoo huu wa Tarimo ulisambaa katika maeneo mengine ya Rombo na kuwa na nguvu kubwa sana ya ushawishi na hata kutawala maeneo mengi ikiwemo himaya ya Mkuu ya zamani. Inasemekana pia baadhi ya koo nyingine zilitokea kwenye ukoo huu mkubwa sana.

– Ukoo wa Tarimo uliendelea kusambaa zaidi katika vijiji vingi vya Uchagga mashariki na magharibi ya Kilimanjaro na kuendelea kupatikana na kuongezeka sana idadi katika maeneo mengine mengi zaidi. Katika himaya ya umangi Kilema miaka ya zamani sana ukoo wa Tarimo ulikuwa na nguvu sana na waliokuwa ndio watawala katika kijiji cha Makami chini, Kilema. Ukoo wa Tarimo pia ndio walikuwa watawala wa himaya ndogo ya umangi Kerio, Rombo. Mangi Leikturu wa himaya ya umangi Kerio aliyeuwa wazungu waliokuwa wanaelekea Usseri mwaka 1894 kisha na yeye kukamatwa na kunyongwa Old Moshi alitokea kwenye ukoo wa Tarimo ambapo baadaye Mangi Ndebarika wa himaya hiyo alikuja kuwa maarufu zaidi.

– Tawi lingine kubwa la ukoo wa Tarimo lilielekea upande wa magharibi na kupatikana kwa wingi sana maeneo ya Masama au Machame ya magharibi.

– Ukoo Tarimo umekuwa ni ukoo wa watu mashuhuri na wenye kujituma sana. Ukoo wa Tarimo umekuwa ni ukoo wenye wasomi wengi na watu wajasiri na wajasiriamali wadogo na wakubwa. Ndani na nje ya Kilimanjaro na hata nje ya Afrika mashariki utakutana na watu wanaofanya vizuri sana katika maeneo mbalimbali kutokea kwenye ukoo wa Tarimo.

Kutokana na kukua sana kwa ukoo wa Tarimo umesambaa na unapatikana katika maeneo mengi mbalimbali ya Uchagga.

– Wachagga wa ukoo wa Tarimo wanapatikana kuanzia magharibi kwa wingi sana katika kijiji cha Nkwansira, Masama.

– Ukoo wa Tarimo wanapatikana kwa wingi pia katika kijiji cha Mbosho, Masama.

– Ukoo wa Tarimo wanapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Lemira, Masama.

– Ukoo wa Tarimo wanapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Isuki, Masama.

– Ukoo wa Tarimo wanapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Mroma, Masama.

– Ukoo wa Tarimo wanapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Ng’uni, Masama.

– Ukoo wa Tarimo wanapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Sonu, Masama.

– Ukoo wa Tarimo wanapatikana kwa kiasi kidogo sana katika kijiji cha Sawe, Masama.

– Ukoo wa Tarimo wanapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Kyeeri, Machame.

– Ukoo wa Tarimo wanapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Shari/Uraa, Machame.

– Ukoo wa Tarimo wanapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Uswaa, Machame.

– Ukoo wa Tarimo wanapatikana kwa kiasi upande wa mashariki ya Kibosho.

– Ukoo wa Tarimo wanapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Ongoma, Uru.

– Ukoo wa Tarimo wanapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Shimbwe, Uru.

– Ukoo wa Tarimo wanapatikana katika kijiji cha Tema, Kata ya Mbokomu, Old Moshi.

– Ukoo wa Tarimo wanapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Tella, Old Moshi.

– Ukoo wa Tarimo wanapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Sango, Old Moshi.

– Ukoo wa Tarimo wanapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Iwa, Kirua Vunjo.

– Ukoo wa Tarimo wanapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Nduoni, Kirua Vunjo.

– Ukoo wa Tarimo wanapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Masaera, Kilema.

– Ukoo wa Tarimo wanapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Makami, chini, Kilema.

– Ukoo wa Tarimo wanapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Makami Juu, Kilema.

– Ukoo wa Tarimo wanapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Lyamrakana, Marangu.

– Ukoo wa Tarimo wanapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Kotela, Mamba.

– Ukoo wa Tarimo wanapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Msae Nganyeni, Mwika.

– Ukoo wa Tarimo wanapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Kondeni, Mwika.

– Ukoo wa Tarimo wanapatikana katika kijiji cha Kiruweni, Mwika.

– Ukoo wa Tarimo wanapatikana katika kijiji cha Uuwo, Mwika.

– Ukoo wa Tarimo wanapatikana katika kijiji cha Mahida, Mamsera, Mamsera, Rombo.

– Ukoo wa Tarimo unapatikana katika kijiji cha Kidondoni, Mamsera, Rombo.

– Ukoo wa Tarimo wanapatikana kwa wingi katika kijiji cha Mamsera kati, Mamsera, Rombo.

– Ukoo wa Tarimo wanapatikana katika kijiji cha Manda Juu, Mengwe, Rombo.

– Ukoo wa Tarimo wanapatikana katika kijiji cha Ngoyoni, Mengwe, Rombo.

– Ukoo wa Tarimo wanapatikana katika kijiji cha Mengeni chini, Keni, Rombo.

– Ukoo wa Tarimo wanapatikana katika kijiji cha Aleni chini, Keni, Rombo.

– Ukoo wa Tarimo unapatikana katika vijiji vya kata ya Shimbi, Mkuu, Rombo.

– Ukoo wa Tarimo wanapatikana kwa wingi katika kijiji cha Mokala, Mkuu, Rombo.

– Ukoo wa Tarimo wanapatikana katika kijiji cha Ibukoni, Mkuu, Rombo.

– Ukoo wa Tarimo wanapatikana katika kijiji cha Ushiri, Mkuu, Rombo.

– Ukoo wa Tarimo unapatikana katika kijiji cha Ubaa, Ushiri, Mkuu, Rombo.

– Ukoo wa Tarimo unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Kerio, Tarafa ya Mashati, Rombo.

– Ukoo wa Tarimo unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Mrao. Tarafa ya Mashati, Rombo.

– Ukoo wa Tarimo unapatikana katika Mmomwe, Tarafa ya Mashati, Rombo.

– Ukoo wa Tarimo unapatikana kwa wingi katika kijji cha Kiraeni, Mashati, Rombo.

– Ukoo Tarimo unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Mrere, Mashati, Rombo.

– Ukoo wa Tarimo unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Katangara, Mashati, Rombo.

– Ukoo wa Tarimo unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Kisale, Mashati, Rombo.

– Ukoo wa Tarimo unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Msaranga, Mashati, Rombo.

– Ukoo wa Tarimo unapatikana kwa kiasi katika vijiji vya Kata ya Olele, Tarafa ya Mashati, Rombo.

– Ukoo wa Tarimo unapatikana katika kijiji cha Kirongo Juu, Usseri, Rombo.

– Ukoo wa Tarimo unapatikana katika kijiji cha Kirongo chini, Usseri, Rombo.

– Ukoo wa Tarimo unapatikana kwa wingi katika kijji cha Lesoroma, Usseri, Rombo.

– Ukoo wa Tarimo unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Ngasseni, Usseri, Rombo.

– Ukoo wa Tarimo unapatikana katika kijiji cha Kwalakamu, Usseri, Rombo.

– Ukoo wa Tarimo unapatikana katika kijiji cha Leto, Usseri, Rombo.

– Ukoo wa Tarimo unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Ubetu, Usseri, Rombo.

– Ukoo wa Tarimo unapatikana katika kijiji cha Kingachi, Usseri, Rombo.

– Ukoo wa Tarimo unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Msangai, Tarakea, Rombo.

– Ukoo wa Tarimo unapatikana katika kijiji cha Nanjara, Tarakea, Rombo.

– Ukoo wa Tarimo unapatikana katika kijiji cha Mbomai, Tarakea, Rombo.

– Ukoo wa Tarimo unapatikana katika kijiji cha Kikelelwa, Tarakea, Rombo.

Kwa sababu ukoo wa Tarimo ni mkubwa sana na uliosambaa kila mahali kuanzia magharibi mpaka mashariki ya Uchagga bado kuna taarifa nyingi muhimu zisizojulikana kuhusiana na ukoo huu. Hivyo tunahitaji kupata taarifa zaidi kutoka kwenye ukoo husika ili kuboresha tafiti na hata kuongeza kwenye maudhui ya koo za wachagga kwa faida ya kizazi cha sasa na vingine vingi vinavyokuja.

Karibu kwa mchango zaidi wa Mawazo kuhusu ukoo wa Tarimo.

1. Je, unafahamu nini kuhusiana na ukoo wa Tarimo?

2. Unafikiri ni kijiji gani ambacho kimesahaulika kutajwa lakini kuna ukoo wa Tarimo?

3. Kijijini kwenu kuna ukoo wa Tarimo?

4. Kama wewe ni wa ukoo wa Tarimo una nini cha kutuambia kuhusu ukoo wenu?

5. Huwa mna maadhimisho yoyote au sherehe za ukoo mwezi gani?

6. Wewe ni Tarimo wa kutokea kijiji gani?

7. Bado kuna ushirikiano wowote katika matukio mbalimbali muhimu na ndugu zenu wengine wa matawi ya ukoo wa Tarimo kutoka maeneo mengine ya Uchaggani?

8. Ni tabia gani unazozifahamu za wachagga wa ukoo wa Tarimo?

9. Wanawake wa ukoo wa Tarimo huitwaje?

10. Una rafiki yako yeyote wa kutokea kwenye ukoo wa Tarimo?

11. Ni watu gani mashuhuri unaowafahamu kutoka kwenye ukoo wa Tarimo?

12. Kuna mnyama yeyote ambaye labda ni mwiko kuliwa na wachagga wa ukoo wa Tarimo?

13. Kuna ukoo ambao hawaruhusiwi kuoana na Wako-Tarimo kwa sababu zilizowahi kuwepo miaka ya zamani?

Karibu kwa Mchango zaidi au maswali.

Ahsanteni.

Kesho tutaendelea na ukoo mwingine.

Whatsapp +255 754 584 270.

You may also like...

Popular Posts

4 Comments

  1. Mnafanya kazi nzuri sana. Ila uchunguzi zaidi wa kina unahitajika ikiwemo kwenda kutembelea maeneo husika na kuongea na wazee husika ili kupata taarifa zaidi.

    Kama kuna nyaraka za zamani pia ambazo zinagusia taarifa husika ni vyema pia kuzipitia. Ni kweli iuwa kazi hii kubwa ya utafiyi na m mchakato husika utahitaji kujitoa sana na rasilimali, hasa fedha, ila ni project yenye thamani na hazina kubwa kwa vizazi vya leo na vijavyo.

  2. Kwa mfano, kuna uwezekano mkubwa kwamba wanaoitwa wa Tarimo leo hii, jina linaweza kusikika kama ni lile lile ila ni tofauti kabisa na matamshi yamekosewa na kuonekana kama ni ukoo mmoja.

    Kwa nini nasema hivyo?
    Inaonekana Tarimo wa Magharibi (Kibosho – Machame – Masama) na wale wa Rombo, wana asili moja na hata masimulizi yao yanaonekana kukubaliana kwamba asili yao ni umasaini.

    Kuna madai kwamba koo za Tarimo na Orio, ndiyo jamii kubwa mbili za kimasai zilizohama kutoka Olmolog (West Kilimanjaro) na kupanda mlima kuingia uchagani. Ila haya masimulizi yanahitaji utafiti na uhakiki zaidi.

    Hata hivyo, ukoo ambao nao unaitwa Tarimo (au Tarimu), wa katikati ya uchagani, hasa maeneo ya Old Moshi, asili yao ni tofauti kabisa. Kwa masimulizi ya wazee wa ukoo husika, wanasema asili yao ni wakilindi kutoka milima ya Usambara, na wanakiri kuwa na uhusiano na Mbega, babu yake Kimweri Simbamwene.

    Kwa hiyo, utaona moja kwa moja ukianza kwenda ndani zaidi kiuchunguzi unakuta hizi ni jamii mbili tofauti. Sasa ikawaje majina yakafanana? Hapo sasa, fikra zaidi ya kiutafiti itahitajika.
    Ahsante.

    1. Kuna upotoshaji pia kwenye historia, kwa sababu kuna tafiti zinasema kwamba Tarimo ya Old Moshi ndio hiyo hiyo moja na Tarimo ya Kibosho – Mweka mpaka Rombo. Inasemekana hivi kwamba Tarimo ya kijiji cha Tella, Old Moshi ndio hiyo Tarimo moja na Kibosho na Rombo lakini Tarimo ya Old Moshi,Tsudunyi ni tofauti na kwamba inatoka huko Kilindi. Lakini ajabu ni kwamba hiyo Tarimo ya Old Moshi Tella ni ndugu wa ukoo mmoja na wanatambika pamoja na hao wa Tsudunyi wakati Tarimo hiyo ya Old Moshi Tella pia ni ndugu na Tarimo ya Kibosho. Ukiunganisha unakuta yote ni moja, anyway hiyo ni tafiti nyingine ambayo nayo ina utata vile vile.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *