MWANAMAPINDUZI MZALENDO NA MUASISI WA HARAKATI ZA UTAIFA KILIMANJARO.

Anaitwa JOSEPH MERINYO MARO.

– Joseph Merinyo Maro Alizaliwa Mwaka 1879 Katika Kijiji cha Mahoma, Old Moshi.

– Akiwa Bado ni Kijana Mdogo Alisafiri Kwenda Ujerumani na Kuishi Huko Kwa Kipindi cha Miaka 2.

– Alijifunza Biashara na Bookkeeping Kwa Ushauri Wa Mjerumani Dr. Theodor Forster Ambaye Alikuwa Mfanyabiashara wa Kahawa Kilimanjaro.

JOSEPH MERINYO MARO AKIWA KATIKA UMRI WA MAKAMO.

– Joseph Merinyo Maro Akiwa Mmoja Kati Ya Wafanyabiashara Wakubwa Wazawa wa Kahawa wa Mwanzoni Kilimanjaro Miaka Ya 1910’s, Alianza Kujenga Ushawishi wa Kisiasa Kilimanjaro.

– Alikuwa Anafanya Kazi Kwenye Serikali Ya Wakoloni wa Kiingereza Akiwa Kama Mshauri Mkuu Mzawa wa Mambo Ya Utawala Kilimanjaro.

– Hivyo Alikuwa na Nguvu Kubwa Kisiasa Kuliko Mangi Yeyote Kilimanjaro Kwa Wakati Huu.

– Kati Ya Mwaka 1917/1918 Joseph Merinyo Maro Alikuwa Mangi Kamili wa Machame Kwa Kipindi cha Mwaka Mmoja.

– Mwaka 1922 Joseph Merinyo Maro Ndiye Aliyempigania Mangi Abraham Salema Mandara Moshi Kukalia Kiti cha Umangi wa Old Moshi, Wakati Huo Kikikaliwa na Mtoto wa Mangi Meli Aliyeitwa Mangi Malamia au Sudi. Joseph Merinyo Maro Alimpendekeza Abrahamu Badala Ya Malamia Kwa Sababu Abrahamu Alikuwa ni Msomi na Makini Zaidi.

– Mwaka 1923 Joseph Merinyo Maro Ndiye Aliyempigania Mangi Abdiel Shangali Mushi Kufanikiwa Kukalia Kiti cha Umangi wa Machame, Mipango Ambayo Alianza Kuisuka Tangu Mwaka 1918. Wakati Huo Abdiel Mwenyewe Akiwa Sio Chaguo La Baba Yake Katika Nafasi Ya Kurithi Kiti cha Umangi wa Machame.

– Kuna Wamangi Wengine Pia Waliingia Madarakani Kwa Ushawishi wa Joseph Merinyo.

– Mwaka 1924 Joseph Merinyo Maro Alianzisha Chama cha Kwanza Cha Wakulima Wazawa Kilimanjaro Kilichoitwa Kilimanjaro Native Planters Association (K.N.P.A).

MKE WA JOSEPH MERINYO MARO.

– Chama cha (K.N.P.A) Kilipata Mafanikio Makubwa Kikilinda Maslahi Ya Wakulima Wazawa Dhidi Ya Wakulima Wageni Sambamba na Madalali Hususan wa Kihindi.

– Kufikia Mwaka 1929 Joseph Merinyo Maro Alikuwa Mtu Maarufu na Muhimu Sana Kwa Wachagga Kilimanjaro Akiwa Anapambania Sana Jamii Ya Wachagga Dhidi Ya Wafanyabiashara wa Kizungu na Serikali Ya Waingereza Pia.

– Joseph Merinyo Maro Alikuwa Anawawakilisha Maslahi Ya Wachagga Bila Woga Kiasi cha Kuingia Kwenye Migogoro na Serikali Ya Waingereza, Pamoja na Wafanyabiashara Wazungu Kilimanjaro Ambao Mara kwa Mara Walikuwa Wanamshitaki Kwenye Serikali Ya Waingereza.

– Joseph Merinyo Maro Alipata Umaarufu Sana Kisiasa Kilimanjaro Kiasi cha Kuogopwa Sana na Waingereza Kwamba Huenda Akapindua Serikali Hivyo Ililazimu Adhibitiwe.

– Kwanza Chama cha (K.N.P.A) Alichoanzisha Joseph Merinyo Maro na Wenzake Mwaka 1924 Kilitakiwa Kuvunjwa Ili Kuanzishwa Kwa Chama cha Ushirika Ambacho Kitapitishwa Kwa Mujibu wa Sheria Baada Ya Muswada wa Sheria Ya Vyama vya Ushirika Kupitishwa Bungeni.

– Hivyo Mwaka 1932 Baada Ya Sheria Ya Vyama vya Ushirika Kupitishwa Bungeni Kilianzishwa Chama cha Kilimanjaro Native Cooperative Union (KNCU) Ambapo Joseph Merinyo Alizuiwa na Serikali Ya Waingereza Kuwa na Ushawishi Ndani Ya Chama Hiki.

– Hata Hivyo Kuanzishwa kwa (KNCU) Kikiwa Kama Chama cha Kwanza cha Ushirika Barani Afrika, ni Matokeo na Msukumo wa Chama cha (K.N.P.A) Kilichoanzishwa na Joseph Merinyo Maro Mwaka 1924.

– Miaka Ya 1930’s Baada Ya Mivutano Mingi na Serikali Ya Waingereza na Baada Ya Kuingia Pia Kwenye Migogoro na Baadhi Ya Wachungaji wa Kanisa La Kiltheri Dhidi Ya Ubaguzi na Kutetea Baadhi Ya Tamaduni, Mila na Desturi za Wachagga, Joseph Merinyo Maro na Mwenzake Petro Njau Walilazimishwa Kuondoka Kilimanjaro na Kwenda Kuishi Uhamishoni Nje Ya Kilimanjaro.

– Wakianzia Monduli, Arusha na Baadaye Kondoa Mpaka Kigoma Joseph Merinyo Maro na Petro Njau Waliishi Nje Ya Kilimanjaro Kwa Zaidi Ya Miaka Kumi.

– Huko Nje Ya Kilimanjaro Kwenye Miaka Ya 1930’s Walikuwa ni Moja Kati Ya Waasisi wa Chama cha Kisiasa Kilichoitwa African Association.

– Lakini Baada Ya Kuona Chama cha African Association Hakina Falsafa Yenye Misingi Sahihi na Halisi Ya Kuwajenga Wazawa wa Afrika Walishawishi Kuvunjwa Chama Hicho na Kuanzisha Matawi.

– Baadaye Baadhi Ya Wanachama wa Chama cha African Association Walikuja Kuunda Chama Kingine Kilichoitwa Tanganyika African Association(TAA) Ambacho Ndicho Mwaka 1954 Kilikuja Kuwa (TANU), Tanganyika African National Union.

– Miaka Ya 1940’s, Baada Ya Kukaa Nje Ya Kilimanjaro Kwa Zaidi Ya Miaka Kumi Joseph Merinyo Maro na Petro Njau Walirudi Kilimanjaro na Kuanzisha Chama cha Kwanza cha Siasa Cha Wachagga Kilichoitwa Kilimanjaro Chagga Citizens Union(KCCU).

– Chama cha (KCCU) Kilikuwa Kimebeba Agenda za Utaifa Kwa Wachagga na Kilikuwa na Falsafa Bora Sana Ya Namna Ya Kusonga Mbele Kama Taifa La Wachagga Lililojengwa Kutoka Kwenye Misingi Ya Wakale Wetu na Kuondokana na Dhana na Misingi Ya Kikoloni.

– Petro Njau Ambaye Alikuwa ni Mwanaharakati Mkubwa wa Falsafa Hii Ya Dhana Ya Utaifa Kutoka Kwenye Misingi Ya Wakale Wetu Akishirikiana na Joseph Merinyo Maro Walijaribu Kuonyesha Uimara Wake na Udhaifu Uliopo Kwenye Dhana Ya Kuchanganya Watu wa Jamii Zote Kwa Pamoja Na Kupuuza Maadili na Tamaduni Zao Ambazo Ndiyo Misingi Ya Uimara Wao.

– Chama cha Kilimanjaro Chagga Citizens Union(KCCU) Kilichoanzishwa na Joseph Merinyo Maro na Petro Njau Kilipata Umaarufu Mkubwa Sana Kilimanjaro na Kilifanikiwa Kumpigania Thomas Lenana Marealle Kuwa Mangi Mkuu wa Wachagga na Hivyo Kubeba Agenda za (KCCU) na Matokeo Yake Utawala Wa Mangi Mkuu Ulikuwa ni wa Mafanikio Makubwa Kiuchumi na Kitamaduni.

JOSEPH MERINYO MARO KATIKA UMRI WA UZEE.

– Joseph Merinyo Maro Alifariki Dunia Mwaka 1973 Akiwa na Umri wa Miaka 94, na Kuzikwa Nyumbani Kwake Katika Eneo La Kolila Katika Kijiji cha Tsudunyi, Old Moshi.

– Joseph Merinyo Maro Alikuwa ni Mtoto wa Merinyo Maro Ambaye Alikuwa ni Jenerali Mkuu wa Majeshi Ya Askari wa Mangi Rindi Mandara. Merinyo Maro Alikuwa ni Moja Kati Ya Wakuu Mashuhuri Sana wa Majeshi Ya Kilimanjaro Katika Historia Ya Wachagga Aliyeogopwa na Kuheshimiwa Sana.

– Joseph Merinyo Maro Pia Ndiye Babu Yake Mama Anna Mkapa Kwa Mtoto Wake Aliyeitwa Shauri Maro.

Urithi Wetu Wachagga.

urithiwetuwachagga@gmail.com

You may also like...

Popular Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *