WIVU WA ASILI.

Wote Tunafahamu Kwamba Binadamu Ni Viumbe wa Hisia. Lakini Katika Moja Ya Hisia Zenye Nguvu Sana Ndani Ya Binadamu Ni Pamoja na Hisia Za Wivu. Hisia za Wivu Ni Zile Hisia Ambazo Huamka Ndani Ya Mtu Pale Anapogundua Kwamba Mtu Mwingine Amemzidi Katika Eneo Fulani.

Hizi Ni Hisia Ambazo Binadamu Wote Huwa Tunazo Ndani Yetu.Lakini Hata Hivyo Hizi Ndio Kati Ya Hisia Ambazo Huwa Tuajitajidi Zaidi Kuzificha Kuliko Hisia Nyingine Nyingi, Kwa Sababu Mtu Huona Aibu Kujulikana Kwamba Ana Hisia za Namna Hii.

Mara Nyingi Ikiwa Mtu Ameingiwa na Hisia za Wivu Halafu Anataka Kuchukua Hatua Kuhujumu Kitu Kwa Kusukumwa na Hisia za Wivu Huwa Ana Kawaida Ya Kutengeneza Agenda Ya Tofauti Nyuma Ya Matendo Yako Hayo Akidai Ndio Lengo Lake, Lakini Ndani Kabisa Ya Moyo Anajua Wazi Kinachomsukuma Ni Wivu wa Kutaka Kuhujumu Jambo Husika.

Baadhi Ya Watu Hufikiri Roho Ya Wivu Iko Tu Kwa Watu Wajinga na Wenye Uelewa Mdogo wa Mambo. Hilo Sio Kweli, Roho Ya Wivu Ipo Kwa Kila Binadamu Anayepumua Lakini Huwa Inatofautiana Viwango Kadiri Ya Uwezo wa Mtu Kujidhibiti. Roho Ya Wivu Iko Ndani Ya Watu wa Mataifa Yote Na Wa Rangi Zote, Kuanzia Watu Wanoishi Maporini Kabisa Huko Kwenye Msitu wa Kongo Mpaka Kwa Maprofesa wa Vyuo Vikuu Vya Havard na MIT, Pamoja na Wanafalsafa Wakubwa na Wanasayansi. Tofauti Kubwa ni Kwamba Watu Wenye Wajinga na Wenye Uelewa Mdogo wa Mambo Hawana Uwezo Mkubwa wa Kujidhibiti Wala Kuficha Nia Zao Kama Watu Wenye Uelewa Mpana, Ambao Huweza Hata Kutengeneza Agenda Ya Tofauti na Lengo Lake Halisi Ili Kuweza Kuhadaa Watu.

Wawekezaji Wakubwa wa Kwenye Masoko Ya Mitaji na Maeneo Mengine Kama Wakina Warren Buffet na Bill Gates Wamekuwa Wakikososa Kwamba Udhaifu wa Waandishi Wengi na Walimu Wengine wa Masuala Ya Maendeleo Binafsi na Hususan Ujasiriamali Kwamba Katika Kuelimisha Kwao Hawaweki Msisitizo Katika Eneo La “Wivu” Kama Sehemu Nyeti Sana Ya Saikolojia Ya Binadamu. Eneo Hili La Wivu Limekuwa na Mchango Mkubwa Katika Kuimarika au Kudhoofika Kwa Mikakati Mbalimbali Lakini Limekuwa Halipewi Uzito Mkubwa Kwa Sababu Watu Wengi Wanajua Kuingiza Hadaa Nyingi Kuficha Ule Msukumo Wao Halisi wa Ndani na Hivyo Watu Kuamini Tofauti na Kusudio Halisi.

Lakini Katika Eneo Hili La Wivu Limegawanyika Mara Mbili Kwamba Kuna Ule Wivu Baina Ya Mtu na Mtu na Wivu Baina Ya Jamii na Jamii. Wivu Kati Ya Mtu na Mtu Japo Huwa Unafichwa Lakini Huwa Tunauona Mara Nyingi Mitaani. Lakini Wivu Kati Ya Jamii na Jamii Unaweza Kufichwa Kwenye Agenda Kubwa Zaidi na Kusambazwa Kama Propaganda za Kisiasa Zilijengwa Katika Hoja Zenye Mashiko Sana na Watu Wengi Wakazichukulia Katika Uzito Huo.

Wivu Baina Ya Kundi Moja La Watu au Mtu Mmoja na Kundi Unaweza Kupelekea Hata Watu Kunyang’anywa Mali Zao na Kufilisiwa Kwa Hoja Kwamba Wamezipata Mali Hizo Bila Kufuata Sheria au Wanajuhumu Nchi na Sababu Nyingine Zinazoonekana Zina Mashiko Lakini Lengo Haswa Ni Wivu na Chuki Kwa Watu Husika. Hisia Hizi Zinazopewa Kipaumbele na Watu Wabaya Hasa Wanapofanikiwa Kufika Katika Nafasi za Juu za Madaraka Imekuwa Ni Chanzo cha Anguko Kubwa La Mambo Mengi Katika Nyakati Mbalimbali za Kihistoria Katika Mataifa Mbalimbali.

Kwa Mfano Hata Julius Nyerere Baada Ya Kupewa Madaraka na Waingereza Baada Ya Uhuru wa Tanganyika na Baadaye Akaamua Kudhoofisha na Kuua Kabisa Vyama vya Ushirika na Hata Mifumo Mbalimbali Iliyokuwa na Manufaa Makubwa Kwa Mkoa na Nchi Kwa Ujumla na Kuja na Hoja Kedekede Zenye Mashiko Kama Vile Tunataka Kudhibiti Ubadhirifu, Sijui Watu Wanaonewa N.k., Watu Wengi Wenye Uelewa Mpana Kama Akina Reginald Mengi Wanasema Wanashindwa Kuelewa Sababu Ni Nini. Wanashangaa Kwa Nini Taasisi Ambazo Zimeleta Neema Kubwa Sana Kiuchumi Kama Vile Vyama Vya Ushirika na Mifumo Mingine Vilikuwa Vinahujumiwa na Baadaye Kufutwa Kabisa Bila Kuwa na Sababu Yenye Mashiko? Na Hata Baada Ya Kurudishwa Vikiwa Vimedhoofika Vinaendelea Kuingiliwa? Japo Wengine Wanadhani Ni Sababu za Kisiasa Peke Yake Lakini Ukichunguza Kwa Ndani Zaidi Unaona Wazi Kwamba Kwa Mfumo wa Kisiasa Uliokuwepo na Uliopo, Bado Havikuwa Tishio Kubwa Sana Kisiasa. Hapa Sasa Ndipo Watu Wanasahau Nguvu Ya Hisia Za Wivu Zilizo Ndani Ya Baadhi Ya Binadamu, Wasiotamani Kuona Jamii Nyingine Ikipiga Hatua Ambao Ni Dhaifu Kiasi Cha Kushindwa Kudhibiti Udhaifu wa Namna Hii wa Kihisia na Kuishia Kuhujumu na Kudhoofisha Mambo Yenye Manufaa Makubwa Kwa Watu Wengine. Wanaona Ni Bora Hata Kama Nchi Itakosa Mapato Tukose Wote Kuliko Watu Fulani Waendelee Kutuacha Mbali. Na Katika Kujidhihirisha Kwamba Jambo Hili Linatokana na Msukumo wa Wivu wa Asili Limeendelea Kuonekana Tena Zaidi na Zaidi Kwenye Nyakati za Baadaye Bila Hata Kuwa na Sababu Zozote za Msingi.

Kwa Mfano Hata Sasa Unaweza Kuamua Kupeleka Maendeleo Kijijini Kwenu au Kwa Watu Wako, Ukashangaa Watu Wanakuandama na Kuanza Kukuita Una Ukabila au Ubinafsi, Wewe Ukahadaika na Maneno Haya na Kuhisi Yana Hoja Ya Msingi Ndani Yake na Kuamua Kuachana na Mpango Huo Kumbe Unachofanya ni Kitu Sahihi Kabisa na Muhimu Sana Kwa Jamii Lakini Kinachowasukuma Hao Wanaokwambia Hivyo Ni Ile Roho Ya Wivu wa Kwa Nini Kwenu Kupate Maendeleo. Maneno Kama Hayo Yamechangia Sana Kudhoofisha Umoja na Mshikamano wa Watu wa Jamii Mbalimbali na Kuzidisha Umaskini wa Baadhi Ya Maeneo Kwa Woga wa Watu Kupewa Majina Yasiyofaa Ambayo Mengi Hata Kutungwa Kwake Tu, Yalitungwa Kwa Lengo La Kudhibiti Watu.

Jambo La Msingi ni Kutomfanyia Mtu Mwingine wa Aina Yoyote Ile, wa Dini Yoyote, wa Kabila Lolote au wa Taifa Lolote Hila Mbaya au Matendo Maovu Kwa Sababu Ya Kundi Lake La Kidini, Nchi, Jamii, Kabila n.k., Kama Vile Kumtukana, Kumkejeli Kumwibia, Kumpiga Kumuua au Kumdhalilisha Kwa Namna Yoyote Ile. Lakini Kufanya Jambo Lolote Zuri Kwa Ajili Ya Watu Wengine Wowote Hususan Ndugu Zako au Watu wa Jamii Yako, Hilo ni Jambo Linalopaswa Kupongezwa na Sio Kujengewa Hatia(Guilt).

Uzuri Ni Kwamba Sio Watu Wote Huchukua Hatua Baada Ya Kupata Wivu Juu Ya Mtu Mwingine au Jamii Nyingine Ya Watu. Watu Wengi Hujua Hizo Ni Hisia Dhaifu za Wivu Ndani Yao na Kuzipuuza Lakini Kuna Wale Watu Dhaifu au Kwa Maana Nyingine Wale Watu Ambao Huwa na Matatizo Ya Kisaikolojia Kitalaamu Wanaitwa (Deep Narcisists) Ndio Ambao Hufika Mbali Kiasi Cha Kuchukua Hatua Kuharibu au Kudhoofisha Maendeleo Ya Wengine Kwa Sababu Ya Wivu wa Ndani Yao Wenyewe Hasa Pale Wanapokuwa Wamepewa Madaraka Makubwa Hususan Ya Kisiasa. Ambapo Wanakuwa Wamedhamiria Kufanya Hata Kabla Ya Hapo.

Lengo La Makala Hii ni Kututia Ujasiri na Kutuondoa Kwenye Imani Potofu Ambazo Zimetujengea Hatia Kwamba Unapofanya Kitu Fulani Kwa Ajili Ya Watu Wenu Basi Unakuwa Unafanya Kosa, Au Hata Kuzungumzia Mambo Ya Kwenu Unakosea Bali Unatakiwa Kuzungumzia Mambo Ya Watu Wengine au Kujitolea Kwa Watu Wengine Hata Kama Huna Shauku Nao Ilimradi Uonekane Unafanya Mambo Sahihi. Kwa Sehemu Imani Hizi Zilijengwa Kwa Msukumo wa Wivu au Kwa Maslahi Fulani Ya Kisiasa.

Tuna Jukumu La Kusimama na Kujijenga Kama Jamii Bila Kusita Wala Kukubali Kudhitiwa Kwa Kujengewa Hatia Za Imani Potofu na Watu Wengine Ambao Kimsingi Wanafanya Hivyo Sio Kwa Nia Njema Kwetu Bali Kwa Kusukumwa na Nia Ovu za Wivu na Chuki.

Ahsanteni.

Karibu kwa Maoni, Ushauri au Maswali.

Urithi Wetu Wachagga

urithiwetuwachagga@gmail.com

You may also like...

Popular Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *