UKOO WA MUNUO.

– Ukoo wa Munuo ni ukoo mkubwa na mashuhuri sana upande wa magharibi ya mbali ya Uchaggani Kilimanjaro. Ukoo huu unapatikana katika maeneo ya Masama Magharibi hususan katika vijiji vya Lukani, Ng’uni, Kyuu, Mashua, Nkwansira, Losaa n.k. Ukoo huu unapatikana pia kwa kiasi maeneo ya Sanya Juu.

– Kutoka kwenye historia ukoo wa Munuo unafahamika kwamba ndio ukoo uliokuwa unatoa watawala katika kijiji cha Kyuu. Ukoo wa Munuo nao walishuka kutoka kwenye plango ya Shira na kuweka makazi yao ya kwanza katika kijiji cha Ng’uni mtaa wa Matikoni kabla ya baadaye kuhamishia makazi yao ya kudumu katika kijiji cha Kyuu.

– Ukoo wa Munuo ulikuwa ni ukoo wa wafugaji matajiri ambao waliteka eneo kubwa la ukanda wa juu na ukanda wa chini wa kijiji cha Kyuu kwa ajili ya mifugo yao sambamba na kilimo hususan ulezi.

– Mtawala wa zamani zaidi anayetambulika na historia wa ukoo wa Munuo aliitwa Kisangasa. Wakati wa utawala wa Mangi Ndesserua wa Machame kipindi kuna uhasama mkubwa kati ya Machame ya mashariki na Machame ya magharibi au Masama, kiongozi mkuu wa ukoo wa Munuo aliitwa Mangi Kikoka na aliungana na Lyamari ndugu yake Ndesserua na watawala wengine wa upande wa magharibi kupambana na Mangi Ndesserua.

– Ukoo wa Munuo umeendelea kuwa mkubwa na maarufu ukiendelea kutoa watu makini kama vile mwanasheria na mwanaharakati mashuhuri Lord Munuo.

Tunahitaji mchango wa mawazo zaidi juu ya ukoo huu mkongwe na mashuhuri wa Munuo.

1. Je, unafahamu nini kuhusiana na ukoo wa Munuo?

2. Kijijini kwenu kuna ukoo wa Munuo?

3. Kama wewe ni wa ukoo wa Munuo una nini cha kutuambia kuhusu ukoo wenu? Huwa mna maadhimisho yoyote au sherehe za ukoo mwezi gani?

4. Bado kuna ushirikiano wowote katika matukio mbalimbali muhimu na ndugu zenu wengine wa matawi ya ukoo huo kutoka maeneo mengine ya Uchaggani?

5. Ni tabia gani unazozifahamu za wachagga wa ukoo wa Munuo?

6. Wanawake wa ukoo wa Munuo huitwaje?

7. Watu gani mashuhuri unaowafahamu kutoka ukoo wa Munuo?

Karibu kwa Maoni na Maswali.

Urithi Wetu Wachagga.

urithiwetuwachagga@gmail.com

You may also like...

Popular Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *