UKOO WA NATAI

– Ukoo wa Natai ni ukoo mkongwe pia na mashuhuri sana upande wa Magharibi ya Kilimanjaro. Huu ni ukoo ambao unapatikana kwa wingi zaidi katika eneo la Masama magharibi katika vijiji vya Lukani, Mashua, Nkwansira, Ng’uni, Kyuu, Losaa n.k. Ukoo wa Natai wanapatikana kwa wingi pia katika vijiji vya himaya ya umangi Sanya Juu.

– Kutoka kwenye historia ukoo wa Natai kama ilivyo kwa ukoo wa Munuo ni nao walishuka kutokea kwenye plango ya Shira magharibi kama mwa Kilimanjaro na kuweka makazi yao katika kijiji cha Ng’uni, Masama magharibi. Ukoo wa Natai ndio walikuwa watawala katika kijiji cha Ng’uni na waliteka maeneo makubwa ya ukanda wa juu na ukanda wa chini wa kijiji cha Ng’uni kwa ajili ya utajiri mkubwa wa mifugo waliokuwa na zamani.

– Kiongozi wa mwanzoni zaidi anayekumbukwa wa ukoo wa Natai wa karne nyingi zilizopita anasemakana kwamba aliitwa Ondumai wakati huo ukoo huo ukiishi katika maeneo ya juu zaidi ambayo leo hii ni eneo la msitu wa mlima Kilimanjaro katika ukanda wa juu wa kijiji cha Ng’uni. Karne kadhaa baadaye kiongozi wa ukoo wa Natai aliyeitwa Msariko ndiye alihamisha makazi ya utawala wa ukoo wa Natai kutoka huko ukanda wa juu na kuweka makazi ya kudumu katika kijiji cha Ng’uni.

– Wakati wa utawala wa Mangi Ndesserua wa Machame mtawala wa kijiji cha Ng’uni kutoka kwenye ukoo wa Natai aliitwa Mangi Keyo. Mangi Keyo wa ukoo wa Natai aliungana na Lyamari ndugu yake Mangi Ndesserua wa Machame pamoja na watawala wengine wa magharibi ya Machame au Masama kupambana na utawala kikatili wa Mangi Ndesserua katika vita ya wenyewe kwa wenyewe iliyoidhoofisha sana Machame ya magharibi au Masama na hata Machame yenyewe kwa ujumla.

– Ukoo wa Natai umeendelea kuwa mkubwa na maarufu sana na umesambaa sana katika maeneo ya vijiji vya Masama magharibi na hata vijiji vya Siha/Sanya Juu pia.

Tunahitaji mchango wa mawazo zaidi juu ya ukoo huu mkongwe na mashuhuri wa Munuo.

1. Je, unafahamu nini kuhusiana na ukoo wa Natai?

2. Kijijini kwenu kuna ukoo wa Natai?

3. Kama wewe ni wa ukoo wa Natai una nini cha kutuambia kuhusu ukoo wenu? Huwa mna maadhimisho yoyote au sherehe za ukoo mwezi gani?

4. Bado kuna ushirikiano wowote katika matukio mbalimbali muhimu na ndugu zenu wengine wa matawi ya ukoo huo kutoka maeneo mengine ya Uchaggani?

5. Ni tabia gani unazozifahamu za wachagga wa ukoo wa Natai?

6. Wanawake wa ukoo wa Natai huitwaje?

7. Una rafiki yako yeyote wa ukoo wa Natai?

8. Watu gani mashuhuri unaowafahamu kutoka kwenye ukoo wa Natai?

Karibu kwa Maoni na Maswali.

You may also like...

Popular Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *