UKOO WA NJAU.

– Ukoo wa Njau ni ukoo mkubwa na mashuhuri sana unaopatikana katika maeneo karibu yote ya Uchaggani, Kilimanjaro. Ukoo wa Njau ni ukoo mkongwe ambao umekuwepo kwenye matukio mbalimbali ya kihistoria tangu karne nyingi zilizopita. Wachagga wa ukoo wa Njau wamekuwa ni watu makini, wasomi na waliofanya mambo mengi makubwa Kilimanjaro.

– Moja kati ya wanazuoni na wanaharakati mashuhuri wa sera za chama cha siasa cha wachagga wahafidhina cha Kilimanjaro Chagga Citizens Union (KCCU) aliitwa Petro Njau kutoka kwenye ukoo huu. Petro Njau alikuwa ni msomi na mwanafalsafa wa mwanzoni Uchaggani aliyekuwa mahiri sana katika kutengeneza hoja nzito zenye mashiko na hata kuboresha falsafa zilizosaidia kujenga siasa imara sana za jamii/taifa la wachagga kabla ya Tanganyika kuwa nchi huru na baadaye Jamhuri. Sera hizo ndizo zilikiwezesha pia chama cha (KCCU) kushinda uchaguzi wa nafasi ya umangi mkuu kupitia mgombea waliompitisha Thomas Marealle. Hivyo kupitia maandiko yake Petro Njau aliweza kupigania mambo mengi ya msingi katika nyakati zake na hata sasa tumejifunza mengi kutoka kwenye sera na mitazamo ya kiuchumi na kisiasa kutoka kwa wazee wetu wa kichagga wa 1930’s/1940’s/1950’s.

– Kutoka kwenye historia tunapata kufahamu kwamba ukoo wa Njau ndio walikuwa watawala wa kijiji cha Kidia, Old Moshi kwa miaka ya zamani sana na hata taasisi ya umangi ilivyoendelea kuimarika iliwapa kipaumbele kwa kuwatambua kwamba ndio watawala wa eneo hili. Umashuhuri wa ukoo wa Njau kutoka maeneo mengine mengi ya Kilimanjaro umeendelea kujidhihirisha kwa kutoa watu mbalimbali waliofanya vizuri na wanaoendelea kufanya vizuri katika maeneo kama misheni na kwenye taaluma nyingi kama vile uandishi wa vitabu, kilimo na hata kisiasa.

– Ukoo wa Njau unapatikana kwenye vijiji mbalimbali vya Kilimanjaro kuanzia katika kijiji cha Lawate, Sanya Juu.

– Ukoo wa Njau unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Nkuu, Machame.

– Ukoo wa Njau unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Njari, Uru.

– Ukoo wa Njau unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Mrawi, Uru.

– Ukoo wa Njau unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Shimbwe, Uru.

– Ukoo wa Njau unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Mnini, Uru.

– Ukoo wa Njau unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Kyaseni, Uru.

– Ukoo wa Njau unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Mwasi Kaskazini na Mwasi Kusini, Uru.

– Ukoo wa Njau unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Kishimundu, Uru.

– Ukoo wa Njau unapatikana maeneo ya kijiji cha Remeni, Uru.

– Ukoo wa Njau unapatikana katika kijiji cha Materuni, Uru.

– Ukoo wa Njau unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Mruwia, Uru.

– Ukoo wa Njau unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Tela, Old Moshi.

– Ukoo wa Njau unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Kidia, Old Moshi.

– Ukoo wa Njau unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Shia, Old Moshi.

– Ukoo wa Njau unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Sango, Old Moshi.

– Ukoo wa Njau unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Iwa, Kirua Vunjo.

– Ukoo wa Njau unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Kmare, Kirua Vunjo.

– Ukoo wa Njau unapatikana katika kijiji cha Mkyashi, Kilema.

– Ukoo wa Njau unapatikana katika kijiji cha Masaera, Kilema.

– Ukoo wa Njau unapatikana katika kijiji cha Ashira, Marangu.

– Ukoo wa Njau unapatikana katika kijiji cha Lyasongoro, Marangu.

– Ukoo wa Njau unapatikana katika kijiji cha Kimangaro, Mamba.

– Ukoo wa Njau unapatikana katika kijiji cha Kokirie, Mamba.

– Ukoo wa Njau unapatikana katika kijiji cha Kiruweni, Mwika.

– Ukoo wa Njau unapatikana katika kijiji cha Lole, Mwika.

– Ukoo wa Njau unapatikana katika kijiji cha Kondeni, Mwika.

– Ukoo wa Njau unapatikana katika kijiji cha Msae, Mwika.

– Ukoo wa Njau unapatikana katika kijiji cha Keni-Aleni, Rombo.

– Ukoo wa Njau unapatikana katika vijiji vya kata ya Shimbi, Mkuu, Rombo.

– Ukoo wa Njau unapatikana katika kijiji cha Mokala, Mkuu, Rombo.

– Ukoo wa Njau katika vijiji vya Tarafa ya Usseri, Rombo.

Kama tunavyoona ukoo wa Njau unapatikana maeneo mengi sana na ni ukoo mashuhuri na mkongwe lakini bado kuna taarifa nyingi zisizojulikana kuhusu ukoo huu wenye wanazuoni wengi. Tunahitaji sana kujua mengi muhimu kutoka kwenye ukoo huu, hivyo tunaomba mchango zaidi wa mawazo kuhusu ukoo wa Njau ili kuweza kuongezea kwenye utafiti na kuongeza zaidi maudhui kuhusu ukoo huu yatakayosaidia hata kuwahamasisha wahusika na kuimarisha mshikamano wao. Pia tunaomba kufahamu vijiji zaidi unakopatikana ukoo huu ili kusaidia katika kurahisisha utafiti zaidi.

1. Je, unafahamu nini kuhusiana na ukoo wa Njau?

2. Unafikiri ni kijiji gani ambacho kimesahaulika kutajwa lakini kuna ukoo wa Njau?

3. Kijijini kwenu kuna ukoo wa Njau?

4. Kama wewe ni wa ukoo wa Njau una nini cha kutuambia kuhusu ukoo wenu? Huwa mna maadhimisho yoyote au sherehe za ukoo mwezi gani? Wewe ni Njau wa kutokea kijiji gani?

5. Bado kuna ushirikiano wowote katika matukio mbalimbali muhimu na ndugu zenu wengine wa matawi ya ukoo wa Njau kutoka maeneo mengine ya Uchaggani?

6. Ni tabia gani unazozifahamu za wachagga wa ukoo wa Njau?

7. Wanawake wa ukoo wa Njau huitwaje?

8. Una rafiki yako yeyote wa kutokea kwenye ukoo wa Njau?

9. Watu gani mashuhuri unaowafahamu kutoka kwenye ukoo wa Njau?

Karibu kwa Mchango zaidi au maswali.

Ahsanteni.

Kesho tutaendelea na ukoo mwingine.

Whatsapp +255 754 584 270

You may also like...

Popular Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *