UKOO WA SHIO.

– Ukoo wa Shio ni ukoo mkubwa na maarufu unaopatikana kwa wingi katika eneo la himaya ya umangi Kibosho hasa katika maeneo vijiji vya kati. Ukoo wa Shio ni ukoo wa watu mashuhuri na makini wanaofanya vizuri maeneo mbalimbali ndani na nje ya Kilimanjaro.

– Kutoka kwenye historia kwa tafiti zilizofanyika mpaka kufikia katikati ya karne ya 20 zinasema kwamba kwa Uchaggani ukoo wa Shio ulihamia Kibosho kutokea katika maeneo yaliyopakana na upande wa magharibi wa mto Nanga. Hiyo maana yake ni kusema kwamba ukoo wa Shio ndani ya Kilimanjaro walihamia Kibosho kutokea maeneo ya vijiji vya Sango au Mowo, Old Moshi ambayo ndio yapo upande wa magharibi wa mto Nanga kwa mujibu wa masilimulizi ya wazee wa wakati miaka ya 1950’s.

– Makazi ya mwanzoni ya wachagga wa ukoo wa Shio kwa Kibosho yalikuwa ni katika kijiji cha Kirima Juu lakini baadaye wakasogea upande wa mashariki kidogo kuweka makazi mengine katika kijiji cha Nsinga, Kibosho. Hata hivyo ukoo wa Shio wameendelea kusambaa katika vijiji vya Nsinga, Kirima yote mpaka Otaruni.

– Ukoo wa Shio wameendelea kusambaa zaidi na kuongezeka sana kwa wingi na hivyo wanapatikana kwa wingi kuanzia katika kijiji cha Kirima Juu, Kibosho.

– Ukoo wa Shio wanapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Kirima Kati na vitongoji vyake kama vile Kidachini, Masoka na Ngirini, Kibosho.

– Ukoo wa Shio wanapatikana kwa wingi sana pia katika kijiji cha Singachini na Singa Juu, Kibosho.

– Ukoo wa Shio wanapatikana katika kijiji cha Sungu, Kibosho.

– Ukoo wa Shio wanapatikana katika kijiji cha Boro, Kibosho.

– Licha ya kwamba ukoo wa Shio ni ukoo mkongwe sana kwa Uchaggani, Kilimanjaro lakini bado kuna taarifa chache sana zinazopatikana juu ya ukoo huu wa wachagga makini na wapambanaji sana ndani na nje ya Kilimanjaro.

-Tunahitaji kupata taarifa zaidi kuhusu ukoo huu wa ili kuongezea kwenye tafiti na hata kuongeza maudhui ya ukoo wenyewe yanayoweza kuwahamasisha wahusika katika kujenga mshikamano zaidi kuelekea kufanikisha mambo makubwa kama ukoo na kama mtu mmoja mmoja. Pia tunahitaji kufahamu vijiji zaidi ambapo ukoo huu unapatikana ili kurahisi zoezi la kufanya tafiti zaidi hapo baadaye.

Karibu kwa mchango zaidi wa mawazo.

1. Je, unafahamu nini kuhusiana na ukoo wa Shio?

2. Unafikiri ni kijiji gani ambacho kimesahaulika kutajwa lakini kuna ukoo wa Shio?

3. Kijijini kwenu kuna ukoo wa Shio?

4. Kama wewe ni wa ukoo wa Shio una nini cha kutuambia kuhusu ukoo wenu? Huwa mna maadhimisho yoyote au sherehe za ukoo mwezi gani? Wewe ni Shio wa kutokea kijiji gani?

5. Bado kuna ushirikiano wowote katika matukio mbalimbali muhimu na ndugu zenu wengine wa matawi ya ukoo wa Shio kutoka maeneo mengine ya Uchaggani?

6. Ni tabia gani unazozifahamu za wachagga wa ukoo wa Shio?

7. Wanawake wa ukoo wa Shio huitwaje?

8. Una rafiki yako yeyote wa kutokea kwenye ukoo wa Shio?

9. Watu gani mashuhuri unaowafahamu kutoka kwenye ukoo wa Shio?

Karibu kwa Mchango zaidi au maswali.

Ahsanteni.

Kesho tutaendelea na ukoo mwingine.

Whatsapp +255 754 584 270.

You may also like...

Popular Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *