UKOO WA MREMA.

– Ukoo wa Mrema ni kati ya koo kubwa, maarufu na mashuhuri sana zilizofanya mambo makubwa katika historia ya wachagga Kilimanjaro. Ukoo wa Mrema umeweza kutoa wachagga wengi mashuhuri wanaofanya vizuri katika maeneo na nyanja mbalimbali ndani na nje ya Kilimanjaro.

– Kutoka kwenye historia ukoo wa Mrema wa tawi la kutoka kijiji cha Tema katika eneo la Natiro, katika kata ya Mbokomu Old Moshi ndio unaonekana kuwa mkongwe zaidi. Hata hivyo kwa kuzingatia historia kwamba wachagga asilia wa mwanzoni waliweka makazi katika eneo la Machame na Mbokomu hili linaongezeka uzito.

– Ukoo wa Mrema wamekuwa ni watawala wa eneo hilo walioanzia katika eneo la Natiro na kusambaza nguvu yao mbali zaidi na kuwa na kuendelea kutoa watawala wa eneo hilo. Ukoo wa Mrema uliendelea kusambaa maeneo mengine ya Uchaggani na kuwa ni kati ya koo kubwa na maarufu sana.

– Moja kati ya wachagga mashuhuri kutokea kwenye ukoo huu mkongwe na maarufu wa Mrema ni mwanasiasa aliyewahi kuwa na nguvu sana kwenye siasa za Tanzania zamani Augustino Lyatonga Mrema. Huyu ni mwanasiasa aliyewahi kutingisha sana siasa za nchi hii na hata kukaribia kushinda kiti cha uraisi ambaye anatokea katika kijiji cha Kiraracha, Kaskazini magharibi ya Marangu. Mwingine ni tajiri mkubwa aliyekuwa anamiliki mahoteli makubwa ya kitalii kama vile Impala, Naura Spring, Ngurdoto n.k., aliyekuwa anatokea katika ukoo wa Mrema wa kijiji cha Mokala, Mkuu, Rombo.

– Wachagga wa ukoo wa Mrema wanapatikana katika vijiji mbalimbali vya Uchaggani, Kilimanjaro kuanzia katika kijiji cha Umbwe, Kibosho.

– Wachagga wa ukoo wa Mrema wanapatikana katika maeneo ya Mawella, Uru.

– Ukoo wa Mrema wanapatikana katika vijiji vya Kata ya Shimbwe, Uru.

– Ukoo wa Mrema wanapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha kitongoji cha Kiwalaa, Kijiji cha Korini chini, Kata ya Mbokomu.

– Ukoo wa Mrema wanapatikana kwa wingi sana Fukeni, katika kijiji cha Korini Juu, Kata ya Mbokomu.

– Ukoo wa Mrema wanapatikana kwa wingi sana Natiro, katika kijiji cha Tema, Kata ya Mbokomu.

– Ukoo wa Mrema wanapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Kidia, Old Moshi.

– Ukoo wa Mrema wanapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Mahoma, Old Moshi.

– Ukoo wa Mrema wanapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Kikarara, Old Moshi.

– Ukoo wa Mrema wanapatikana kwa wingi katika kijiji cha Mdawi, Old Moshi.

– Ukoo wa Mrema wanapatikana kwa wingi katika kijiji cha Sango, Old Moshi.

– Ukoo wa Mrema wanapatikana kwa wingi katika kijiji cha Kmare, Kirua Vunjo.

– Ukoo wa Mrema wanapatikana kwa wingi katika kijiji cha Nduoni, Kirua Vunjo.

– Ukoo wa Mrema wanapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Mkyashi, Kilema.

– Ukoo wa Mrema wanapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Kyou, Kilema.

– Ukoo wa Mrema wanapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Samanga, Marangu.

– Ukoo wa Mrema wanapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Kyala, Marangu.

– Ukoo wa Mrema wanapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Kiraracha, Marangu.

– Ukoo wa Mrema wanapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Mmbahe, Marangu.

– Ukoo wa Mrema wanapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Lyasongoro, Marangu.

– Ukoo wa Mrema wanapatikana kwa kiasi katika vijiji vya Mamba.

– Ukoo wa Mrema wanapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Msae Kinyamvuo, Mwika.

– Ukoo wa Mrema wanapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Kondiki, Mwika.

– Ukoo wa Mrema wanapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Kondeni, Mwika.

– Ukoo wa Mrema wanapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Mawanjeni, Mwika.

– Ukoo wa Mrema wanapatikana kwa kiasi katika vijiji vya kata ya Shimbi, Mkuu, Rombo.

– Ukoo wa Mrema wanapatikana kwa kiasi Mokala, Mkuu, Rombo.

– Ukoo wa Mrema wanapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Samanga, Usseri, Rombo.

Wachagga mashuhuri kutoka kwenye ukoo wa Mrema ni wengi sana na vijiji ambavyo ukoo wa Mrema unapatikana ni vingi zaidi lakini tunajitahidi kuorodhesha baadhi ili kurahisisha utafiti zaidi baadaye tukitegemea wale wenye kufahamu maeneo zaidi ambapo ukoo huu unapatikana watusaidie kuongeza vile vilivyosahaulika ili kurahisisha zoezi hili la utafiti. Kufahamu zaidi pia kutasaidia kuongeza maudhui(content) ya ukoo husika ambayo ni sehemu muhimu ya kuhamasisha mshikamano zaidi miongoni mwa wahusika kuelekea kufanya mambo makubwa zaidi mbeleni kwa ngazi ya jamii nzima na kwa ngazi ya mtu mmoja mmoja pia.

– Hivyo karibu kwa mchango zaidi.

1. Je, unafahamu nini kuhusiana na ukoo wa Mrema?

2. Unafikiri ni kijiji gani ambacho kimesahaulika kutajwa lakini kuna ukoo wa Mrema?

3. Kijijini kwenu kuna ukoo wa Mrema?

4. Kama wewe ni wa ukoo wa Mrema una nini cha kutuambia kuhusu ukoo wenu? Huwa mna maadhimisho yoyote au sherehe za ukoo mwezi gani? Wewe ni Mrema wa kutokea kijiji gani?

5. Bado kuna ushirikiano wowote katika matukio mbalimbali muhimu na ndugu zenu wengine wa matawi ya ukoo wa Mrema kutoka maeneo mengine ya Uchaggani?

6. Ni tabia gani unazozifahamu za wachagga wa ukoo wa Mrema?

7. Wanawake wa ukoo wa Mrema huitwaje?

8. Una rafiki yako yeyote wa kutokea kwenye ukoo wa Mrema?

9. Watu gani mashuhuri unaowafahamu kutoka kwenye ukoo wa Mrema?

Karibu kwa Mchango zaidi au maswali.

Ahsanteni.

Kesho tutaendelea na ukoo mwingine.

Whatsapp +255 754 584 270.

You may also like...

Popular Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *