“THE JEWISH PHENOMENON”, #SEHEMU YA 2#

“THE JEWISH PHENOMENON”

#SEHEMU YA 2#

WAYAHUDI/WAISRAEL NI NANI?

Wayahudi/Waisrael au kwa kiingereza maarufu zaidi kama “Jews” ni jamii ya watu, ni taifa, ni dini na ni kabila pia.

Wayahudi wana dini yao rasmi ya kiyahudi ambayo ndio imezaa dini ya kikristo na baadaye uislamu, lakini Wayahudi hawa waliendelea kubaki kwenye dini yao ile ile ya kiyahudi japo kwa sehemu kubwa historia takatifu inayotumiwa na wakristo kuhusu miongozo ya Mungu kwa manabii wa kale ambayo kwa mujibu wa wakristo, waislamu na biblia inasemekana Mungu ndiye alikuwa anawaongoza na kuwaagiza.

Historia hii takatifu kwa wakristo pia ni historia ya maisha ya Wayahudi na vizazi vyao kutokea wakati wa Ibrahimu takriban miaka 4,000 iliyopita mpaka kufikia miaka 2,000 iliyopita yalipokuja mapinduzi mapya yaliyochochewa na makundi yaliyokuwa yanashindana ndani ya Uyahudi kama Mafarisayo, Masadukayo n.k,.

Hata hivyo ukristo huu ulioanza kama mabadiliko na maboresha ya dini ya kiyahudi ulianzishwa na Wayahudi wenyewe takriban miaka 2,000 iliyopita lakini baada ya wasambaza injili ya kikristo kama akina mtume Paulo na wengine kuruhusu ukristo kuingiliwa na watu wa mataifa mengine/gentiles na kutaka kuusambaza zaidi Wayahudi wengi waligoma kujiunga na ukristo na badala yake wakarudi kwenye dini yao ya kiyahudi.

Makundi ndani ya dini ya kiyahudi kama mafarisayo na masadukayo walipingana na wakristo kuanzia Yesu mwenyewe japo wanahistoria wanadai kwamba mafarisayo walikuwa wanaelewana zaidi na wakristo kuliko masadukayo ambao walikuwa ndio wasomi zaidi.

Hata hivyo kitendo cha wayahudi kugoma kujiunga na ukristo mwanzoni na kung’ang’ania dini yao ya kiyahudi kilikuja kuwagharimu sana kwani walipitia manyanyaso, mateso na hata mauaji mengi kutoka kwa watawala wa dola ya Rumi/Roman empire na baadaye tawala za Ulaya kutokana msimamo wao huo.

Tawala hizi zilikuwa zinalazimisha kila mtu kuwa mkristo na anayekaidi anapewa adhabu kali na mara nyingi ni adhabu ya kifo, lakini bado hilo halikuwazuia wayahudi kuendelea kung’ang’ana na dini yao wakati mwingine wakisali kwa siri.

Wayahudi au maarufu pia kama Waisraeli wana nchi yao ya asili ambayo ni Israel iliyopo mashariki ya kati, wana mila na desturi zao, wana sherehe zao na maazimisho mbalimbali, wana lugha yao, wana vyakula vyao maalum n.k,.

Dini ya kiyahudi ni dini inayoruhusu mtu yeyote kujiunga ikiwa tu umekubalika na kupitishwa na kiongozi wa kiyahudi wa eneo lako husika anayejulikana kama Rabbi.

Mwandishi anasema linapokuja suala la mafanikio ya wayahudi basi tamaduni na desturi za kiyahudi zinahusika ambazo zimeweza kuwasaidia wayahudi kufanikiwa sana ndani ya Marekani na hata katika mataifa mengine.

Mwandishi anasema kupitia dini ya kiyahudi, wayahudi wamekuwa na mtazamo chanya sana juu ya utajiri ukilinganisha na wakristo kwa ujumla, wayahudi wao wanaamini utajiri ni kitu kizuri. Mwandishi anasema wakristo wamekuwa na vifungu vingi vyenye mtazamo hasi juu ya utajiri na ametolea mfano agano jipya kutoka Matayo 9;24, Marko 10;25 na Luka 18;25 ambayo inasema “Ni Rahisi Kwa Ngamia Kupita Kwenye Tundu La Sindano Kuliko Mtu Tajiri Kuingia Katika Ufalme wa Mbinguni”.

Mwandishi anaamini maandiko kama haya yanajenga mtazamo hasi juu ya utajiri na yana madhara kwa wafuasi wa dini husika.

Maandiko mengine ambayo mwandishi ameyakosoa kwenye biblia katika agano jipya ambalo ndio hasa limewatenganisha Wayahudi na wakristo ni pamoja na Luka 16;23 inayosema huwezi kutumikia mabwana wawili kwa wakati mmoja, yaani huwezi kumtumikia Mungu na utajiri.

1 Timotheo 6;8-9 inasema “Watu Wanaotamani Kuwa Matajiri Huanguka Katika Majaribu na Mtego na Tamaa Nyingi Mbaya na za Kijinga, Ambazo Huwatokomeza Wanadamu Katika Upotevu na Maangamizi”.

1 Timotheo 6;10 “Maana Kupenda Pesa Ni Chanzo Cha Uovu Wote”.

Hiyo ni baadhi ya mistari katika agano jipya ambayo mwandishi ameitaja kwamba inaleta mitazamo hasi kwa watu wa jamii nyingine na kuwapunguzia ile ari ya wao kuutafuta utajiri na mafanikio kwa ujumla.

Kwa upande wa dini ya kiyahudi mwandishi anasema wana imani kwamba utajiri ni kitu kizuri na chenye thamani kubwa kinachostahili mtu kuweka juhudi kukipambania. Kufilisika ni jambo baya kwao.

Wayahudi kwa mitazamo yao hawauoni umaskini kama ni utakatifu kama jinsi agano jipya la biblia linahimiza. Mwandishi anasema kwa bahati nzuri ni kwamba wayahudi wa mwanzo hawakuwa maskini.

Anasema waanzilishi wa Taifa la Wayahudi Ibrahimu, Isaka na Yakobo walikuwa matajiri wakubwa wa mifugo na ardhi kubwa.

Mwandishi anasema kujikana nafsi yako na mambo ya dunia na kutojihangaisha na kutafuta mali sio jambo lenye thamani kwa wayahudi badala yake wao wanaamini ukiwa tajiri ndio unaweza kuishi maisha matakatifu ya kiroho kwa usahihi zaidi.

Katika maandiko ya wayahudi kwenye kitabu cha “Mishna” kuna usemi unasema kwamba, “Pasipo na unga, hapana biblia”.

Maandiko mengine ya wayahudi yanasema “Umaskini ndio chanzo cha uovu na uhalifu”.

Kitabu cha Talmud cha dini ya Wayahudi kinasema “Umaskini ni mbaya zaidi ya magonjwa hatari 50 ya kuambukiza mfano wa korona au tauni.

Ahsanteni

Kwenye makala inayofuata tutaendelea na historia ya kale ya Wayahudi tangu nyakati za biblia katika agano la kale.

YESU KRISTO ALIKUWA MYAHUDI

Urithi Wetu Wachagga

urithiwetuwachagga@gmail.com

You may also like...

Popular Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *