“THE JEWISH PHENOMENON” 7 Keys To Enduring Wealth of The People. “SEHEMU YA 1.”

“THE JEWISH PHENOMENON”

7 Keys To Enduring Wealth of The People.

“SEHEMU YA 1.”

Utangulizi

Mwandishi wa kitabu hiki cha “The Jewish Phenomenon” ambacho kinazungumzia njia saba zinazopelekea jamii ya watu fulani kuwa na utajiri usio na kikomo na usioisha, Steven Silbiger anasema Wayahudi ndio jamii/kabila la watu matajiri zaidi ndani ya Marekani.

Makampuni makubwa ya teknolojia kama Google, Facebook, Dell Computers n.k., pamoja na makampuni mengine mengi katika nyanja nyingine za kiuchumi yameanzishwa na yanamilikiwa na kuongozwa na watu wa jamii ya Wayahudi.

Lakini anasema kwamba mbinu na njia ambazo jamii ya wayahudi imezitumia kufanikisha haya zinaweza kutumiwa na jamii nyingine yoyote au mtu mwingine na kupata mafanikio makubwa.

Mwandishi wa kitabu hiki Steven Silbiger anasema kwamba utajiri mkubwa uliotengenezwa na jamii ya wayahudi sio utajiri wa pesa peke yake bali umejumuisha maendeleo makubwa katika sanaa, sayansi na sayansi za jamii.

Mwandishi anasema kwamba wayahudi wamekuwa wahanga wa chuki, wivu na visasi vinavyotokana na maendeleo waliyonayo na hasa nadharia kwamba wayahudi ni taifa lililobarikiwa kwa asili, lakini anasema kitabu chake cha “The Jewish Phenomenon” kinajaribu kuelezea kwamba maendeleo ya wayahudi yameletwa na sababu nyingi zinazohusiana na dini yao na tamaduni zao sambamba na mapito mazito waliyopitia katika historia.

Mwandishi anasema haya ni mambo ambayo jamii nyingine yoyote inaweza kuyafuatilia na kujifunza.

Anti-Semitism ni neno maarufu ambalo limekuwa likiwakilisha kitendo cha kuwa na chuki kwa wayahudi ambayo imekuwa na nguvu kwa karne nyingi na maelfu ya miaka lakini sasa hivi inaonekana kufifia sana.

Mwandishi anasema kwa miaka mingi sana maendeleo ya wayahudi yameonekana kama ndio sababu ya matatizo kwa wengine na sababu ya watu wengine kurudi nyuma kutokana na propaganda nyingi zilizoambatana na maendeleo hayo.

Mwandishi anasema hata Rais wa 37 wa Marekani Richard Nixon ambaye alijiuzulu urais baada ya tuhuma nzito zilizomkabili maarufu kama “Watergate Scandal” ambazo zilimlazimu kujiuzulu urais wa Marekani mwaka 1974 alizihusisha na njama zilizosukwa na wayahudi.

Mwandishi Steven Silbiger anasema japo chuki na ubaguzi dhidi ya Wayahudi umekomeshwa katika taasisi za ndani ya Marekani lakini bado kwa mtu mmoja mmoja chuki dhidi ya wayahudi zinaendelea. Mwandishi anasema kwa sasa chuki dhidi ya wayahudi na ubaguzi umedhibitiwa sana katika taasisi zote ndani ya Marekani na kitendo chochote kinachoashiria ubaguzi dhidi ya wayahudi kinashutumiwa na kupingwa vikali kutoka kila kona ya dunia lakini ni miaka 80 tu iliyopita ambapo bilionea Henry Ford alikuwa akifanya kampeni nzito za kuwashutuma wayahudi juu ya mambo mbalimbali.

Henry Ford alikuwa anaamini kwamba wayahudi wanasuka njama za kimataifa kuhujumu uchumi wa dunia na alitumia mamilioni ya pesa kufanya utafiti na kuweka wazi tuhuma hizi katika jarida lake maarufu lililojulikana kama “International Jew”.

Mwandishi anasema hata sasa bado kuna wayahudi wengi pamoja na baadhi ya vyombo vya habari ambao hawataki kuzungumzia mafanikio yao kwa uwazi ili kuepuka chuki kali dhidi yao.

Mwandishi anasema hata mwanzoni wakati anahariri kitabu hiki kwa mara ya kwanza kilipingwa vikali na jamii ya wayahudi kwa sababu waliogopa kitaleta taharuki na kuamsha upya chuki dhidi ya wayahudi.

Mwandishi anasema utafiti uliofanywa na Daniel Yankelovich unaonyesha kwamba zaidi ya asilimia 25 ya watu wanaamini kwamba wayahudi wana nguvu kubwa sana ndani ya siasa za Marekani na wayahudi wenyewe wanaamini kwamba watu wengi wanaamini hivyo.

Mwandishi anasema tafiti zinaonyesha kwamba.

-Kwa wastani familia za kuyahudi zina kipato kikubwa mara mbili ya kipato cha jamii nyingine ndani ya Marekani.

-Licha ya kwamba wayahudi ni asilimia 2% tu ya watu ndani ya Marekani, lakini asilimia 40% ya mabilionea wote Marekani ni wayahudi.

-Na theluthi moja ya matajiri wakubwa wanaokaribia ubilionea Marekani ni wayahudi pia.

-Asilimia 20% ya maprofesa katika vyuo vikuu vikubwa Marekani ni wayahudi.

-Asilimia 40% ya makampuni makubwa ya sheria Marekani hasa katika miji ya New York na Washington DC ni wayahudi pia.

-Asilimia 30% ya washindi wa tuzo za Nobel za sayansi na asilimia 25% ya washindi wa tuzo zote za nobel nchini Marekani ni wayahudi.

Yote haya yanafanyika wakati idadi ya wayahudi nchini Marekani ni asilimia 2% tu ya wamarekani wote, yaani wayahudi wako milioni 6 ndani ya Marekani ambayo ina Zaidi ya watu milioni 300.

Lengo la kitabu hiki ni kujifunza kwamba ni kwa namna gani au sababu zipi zimeiwezesha jamii ya kiyahudi kuweza kukua na kufikia mafanikio makubwa sana ukilinganisha na jamii nyingine ambazo tunaweza kujifunza na kuzitumia pia.

Kwa Mujibu wa Mwandishi wa Kitabu Hiki cha The Jewish Phenomenon Hizi Ndio Sababu 7 Zilizowasaidia Wayahudi Kuwa na Mafanikio Makubwa Sana.

1. Kuelewa Kwamba Utajiri wa Kweli Unabebeka, Ambao Ni Maarifa.

2. Jijali Wewe Mwenyewe Nao Watakujali.

3. Watu Wenye Mafanikio Makubwa Duniani Ni Wanataaluma/Professionals na Wajasiriamali/Enterpreneurs

4. Jijengee Kujiamini Katika Kujieleza

5. Jenga Nidhamu Ya Matumizi Ya Fedha na Weka Akiba Ya Uwekezaji wa Baadaye Isiyopungua 10% Ya Kila Fedha Unayoingiza

6. Jisikie Fahari Kwa Kila Unachofanikisha na Endelea Kujihimiza Katika Ubunifu Zaidi

7. Jitengenezee Saikolojia Ya Kutaka Kuwadhihirishia Watu Kwamba Unaweza Kufanikisha Jambo Fulani.

Ahsanteni

Itaendelea kwenye makala inayofuata

KAMPUNI YA GOOGLE

Urithi Wetu Wachagga

urithiwetuwachagga@gmail.com

You may also like...

Popular Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *