UKOO WA CHUWA.

– Chuwa ni ukoo maarufu wa wachagga ambao na wenye idadi kubwa kiasi ya watu ukiwa na watu mbalimbali waliosambaa maeneo mengi ndani na nje ya Kilimanjaro na hata nje ya Tanzania. Wachagga wa ukoo wa Chuwa wengi ni watu wenye kujituma sana na wakiwa na wafanyabiashara wengi wanaofanya vizuri ndani na nje ya Kilimanjaro na hata nje ya Tanzania.

– Kutoka kwenye historia ukoo wa Chuwa unafahamika kwamba uliweka makazi yake ya asili ya kwanza ya ni katika kijiji cha Sungu, Kibosho. Hata hivyo inasemekana kwamba ukoo wa Chuwa ambao walifika Kibosho sambamba na Mangi Yansanya mwanzoni walifikia katika kijiji cha Kirima Juu, Kibosho na baada ya muda ndipo wakahamia na kuweka makazi ya kudumu katika kijiji cha Sungu, Kibosho.

– Wachagga wa ukoo Chuwa katika historia ni kati ya koo ambazo zilikuwa na taaluma ya kufua vyuma na hata kutengeneza silaha zamani japo sio kwa kiwango kikubwa. Hivyo ukoo wa Chuwa ulikuwa na heshima fulani kubwa kwenye jamii ya wachagga kwa utaalamu huu ambao ulikuwa muhimu sana kwa wachagga Kilimanjaro na sehemu muhimu pia ya biashara ya bidhaa zilizokuwa zinauzwa kwa wingi sana nje ya Kilimanjaro.

– Wachagga wa ukoo wa Chuwa kutokea katika kijiji cha Sungu, Kibosho kilichopo upande wa mashariki zaidi wa Kibosho waliendelea kusambaa katika vijiji vingine mashariki na magharibi ya eneo lao la makazi. Ukoo wa Chuwa walivuka mipaka na kusambaa mpaka upande wa mashariki zaidi wakavuka mto Ngomberi na kuingia katika himaya ya umangi Uru hususan upande wa magharibi ya Uru.

– Kutokana na kusambaa huku ukoo wa Chuwa unapatikana kwa kiasi katika vijiji vya Manushi, Kibosho.

– Ukoo wa Chuwa unapatikana kwa kiasi katika vijiji vya kata ya Kindi, Kibosho.

– Ukoo wa Chuwa unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Sambarai Kibosho.

– Ukoo wa Chuwa unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Umbwe, Kibosho.

– Ukoo wa Chuwa unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Mloe, Kibosho.

– Ukoo wa Chuwa unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Kitandu, Kibosho.

– Ukoo wa Chuwa unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Uchau kusini, Kibosho.

– Ukoo wa Chuwa unapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Otaruni, Kibosho.

– Ukoo wa Chuwa unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Maua, Kibosho.

– Ukoo wa Chuwa unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Kirima Juu, Kibosho.

– Ukoo wa Chuwa unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Kirima Kati, Kibosho.

– Ukoo wa Chuwa unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Boro, Kibosho.

– Ukoo wa Chuwa unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Singa, Kibosho.

– Ukoo wa Chuwa unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Singa chini, Kibosho.

– Ukoo wa Chuwa unapatikana kwa wingi sana katika Sungu, Kibosho.

– Ukoo wa Chuwa unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Mweka, Kibosho.

– Ukoo wa Chuwa unapatikana katika kijiji cha Njari, Uru.

– Ukoo wa Chuwa unapatikana katika vijiji vya eneo la Mawela, Uru.

– Ukoo wa Chuwa unapatikana katika kijiji cha Okaseni, Uru.

– Ukoo wa Chuwa unapatikana katika kijiji cha Mrawi, Uru.

– Ukoo wa Chuwa unapatikana katika vijiji vya Shimbwe, Uru.

– Ukoo wa Chuwa unapatikana kwa kiasi kidogo katika vijiji vya kata za Uru mashariki.

Tunahitaji mchango zaidi wa mawazo juu ya ukoo huu wa Chuwa ambao ni maarufu lakini ukiwa na uhaba wa taarifa ili kuongezea zaidi katika maudhui haya ya koo kwa faida ya sasa na kizazi cha baadaye.

Karibu kwa mchango zaidi wa Mawazo kuhusu ukoo wa Mushi/Moshi.

1. Je, unafahamu nini kuhusiana na ukoo wa Chuwa?

2. Unafikiri ni kijiji gani ambacho kimesahaulika kutajwa lakini kuna ukoo wa Chuwa?

3. Kijijini kwenu kuna ukoo wa Chuwa?

4. Kama wewe ni wa ukoo wa Chuwa una nini cha kutuambia kuhusu ukoo wenu?

5. Huwa mna maadhimisho yoyote au sherehe za ukoo mwezi gani?

6. Wewe ni Chuwa wa kutokea kijiji gani?

7. Bado kuna ushirikiano wowote katika matukio mbalimbali muhimu na ndugu zenu wengine wa matawi ya ukoo wa Chuwa kutoka maeneo mengine ya Uchaggani?

8. Ni tabia gani unazozifahamu za wachagga wa ukoo wa Chuwa?

9. Wanawake wa ukoo wa Chuwa huitwaje, na kwa nini?

10. Una rafiki yako yeyote wa kutokea kwenye ukoo wa Chuwa?

11. Ni watu gani mashuhuri unaowafahamu kutoka kwenye ukoo wa Chuwa?

12. Kuna mnyama yeyote ambaye labda ni mwiko kuliwa na wachagga wa ukoo wa Chuwa?

13. Kuna ukoo ambao hawaruhusiwi kuoana na Wako-Chuwa kwa sababu zilizowahi kuwepo miaka ya zamani?

Karibu kwa Mchango zaidi au maswali.

Ahsanteni.

Kesho tutaendelea na ukoo mwingine.

Whatsapp +255 754 584 270.

You may also like...

Popular Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *