UKOO WA TILLYA.

– Tillya ni ukoo mkongwe sana wa kichagga na ulioenea katika vijiji vingi mbalimbali ndani ya Uchagga, Kilimanjaro. Huu ni ukoo wenye watu wengi wanaopatikana katika maeneo mbalimbali ndani na nje ya Kilimanjaro na hata nje ya nchi. Wachagga wa ukoo wa Tillya ni watu wenye kujituma na wanafanya vizuri sana katika taaluma zao na biashara maeneo mbalimbali ndani na nje ya Kilimanjaro na hata nje ya nchi.

– Kutoka kwenye historia ukoo wa Tillya unatajwa kuwa chimbuko lake na eneo yalipokuwa makazi ya kudumu ni katika eneo ambalo leo hii ni kitongoji cha Moori, kijiji cha Lyamrakana, Marangu. Tunafahamu kutoka kwenye historia kwamba katika eneo la Lyamrakana baada ya ukoo wa Lyimo kuwazidi maarifa ukoo wa Mboro na kufanikiwa kuwaangusha na kutawala Lyamrakana ukoo wa Tillya walipata hofu na kuamua kutafuta ushirika na wako-Lyimo.

– Hivyo japo ukoo wa Tillya walifanikiwa kuwa washirika wa ukoo wa Lyimo na kubakia Lyamrakana sambamba na ukoo wa Lyimo lakini waliweza kufanikisha hilo kwa gharama kubwa ya usaliti kwa marafiki zao, ukoo wa Kinyagha. Hivyo baada ya ukoo wa Mboro kusambaratishwa na kukimbilia kusambaa maeneo mbalimbali ya Uchaggani na baadhi ya wachagga wa ukoo wa Kinyagha kukimbilia Kilema, ukoo wa Tillya walibakia Lyamrakana katika eneo la Moori upande wa magharibi wa mto Una. Hata hivyo sehemu ndogo ya ukoo wa Mboro walikimbilia upande wa kusini katika kijiji cha Sembeti na kuweka makazi katika kitongoji maarufu cha Kirefure.

– Ukoo wa Tillya waliendelea kusambaa maeneo mbalimbali na wanapatikana katika vijiji vingi mbalimbali vya Uchagga, Kilimanjaro. Hata hivyo baadhi ya wachagga ambao ni tawi la ukoo huu waliosambaa maeneo mbalimbali wanajiita Kitillya na wengine wakijaribu kutumia majina mengine ya ukoo.

– Ukoo wa Tillya wanapatikana kwa wingi kiasi katika maeneo ya kijiji cha Mawella, Uru.

– Ukoo wa Tillya wanapatikana kwa kiasi katika maeneo ya kijiji cha Shimbwe, Uru.

– Ukoo wa Tillya wanapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Kidia, Old Moshi.

– Ukoo wa Tillya wanapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Kikarara, Old Moshi.

– Ukoo wa Tillya wanapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Sango, Old Moshi.

– Ukoo wa Tillya wanapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Kmare, Kirua Vunjo.

– Ukoo wa Tillya wanapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Nduoni, Kirua Vunjo.

– Ukoo wa Tillya wanapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Lyamrakana, Marangu.

– Ukoo wa Tillya wanapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Sembeti, Marangu.

– Ukoo wa Tillya wanapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Komakundi, Mamba.

– Ukoo wa Tillya wanapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Msae, Mwika.

– Ukoo wa Tillya wanapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Kimangaro, Mwika.

Tunahitaji mchango zaidi wa mawazo na taarifa zaidi kuhusu ukoo huu wa Tillya ambao ni mkongwe sana Uchaggani ili kuweza kuongeza kwenye maudhui ya koo za wachagga na ukoo wa Tillya wenyewe kwa faida ya kizazi cha sasa hivi na vinavyokuja. Hii inasaidia kuongeza ari, umoja na mshikamano miongoni mwa wanaukoo na wachagga kwa ujumla katika kusaidiana na kufanya mambo makubwa kwa ngazi ya ukoo na ngazi ya mtu mmoja mmoja.

Karibu kwa mchango zaidi wa Mawazo kuhusu ukoo wa Mushi/Moshi.

1. Je, unafahamu nini kuhusiana na ukoo wa Tillya?

2. Unafikiri ni kijiji gani ambacho kimesahaulika kutajwa lakini kuna ukoo wa Tillya?

3. Kijijini kwenu kuna ukoo wa Tillya?

4. Kama wewe ni wa ukoo wa Tillya una nini cha kutuambia kuhusu ukoo wenu?

5. Huwa mna maadhimisho yoyote au sherehe za ukoo mwezi gani?

6. Wewe ni Tillya wa kutokea kijiji gani?

7. Bado kuna ushirikiano wowote katika matukio mbalimbali muhimu na ndugu zenu wengine wa matawi ya ukoo wa Tillya kutoka maeneo mengine ya Uchaggani?

8. Ni tabia gani unazozifahamu za wachagga wa ukoo wa Tillya?

9. Wanawake wa ukoo wa Tillya huitwaje, na kwa nini?

10. Una rafiki yako yeyote wa kutokea kwenye ukoo wa Tillya?

11. Ni watu gani mashuhuri unaowafahamu kutoka kwenye ukoo wa Tillya?

12. Kuna mnyama yeyote ambaye labda ni mwiko kuliwa na wachagga wa ukoo wa Tillya?

13. Kuna ukoo ambao hawaruhusiwi kuoana na Wako-Tillya kwa sababu zilizowahi kuwepo miaka ya zamani?

Karibu kwa Mchango zaidi au maswali.

Ahsanteni.

Kesho tutaendelea na ukoo mwingine.

Whatsapp +255 754 584 270.

You may also like...

Popular Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *