UKOO WA MURO.

– Muro ni ukoo wa wachagga wanaopatikana upande wa magharibi zaidi ya Uchagga, Kilimanjaro. Japo majina ya Muro yamepata kuonekana Uchaggani katika nyakati tofauti tofauti kwenye koo mbalimbali lakini ukoo wa Muro unasemekana kuwa ni tawi la ukoo mkubwa wa Mboro uliosambaa uchaggani kote.

– Watu mbalimbali mashuhuri waliowahi kufahamika sana katika historia ya wachagga Kilimanjaro kwa jina la Muro ni pamoja na Mzee Muro Mboyo aliyekuwa jemedari mashuhuri ndani ya majeshi ya Mangi Rengua wa Machame. Mtu mwingine anayeitwa Muro anayefahamika kwenye historia ya wachagga Kilimanjaro ni Muro mashuhuri aliyeamua kumuunga mkono Lyamari aliyekuwa mpinzani na muasi wa serikali ya Mangi Ndesserua wa Machame ambaye alielekea upande wa magharibi kuungana na watu wa Masama na kupelekea vita kubwa sana iliyopiganwa Machame wenyewe kwa wenyewe katika miaka 1850’s/1860’s.

– Huyu Muro Mboyo ni baba yake na Kirama Muro ambaye alipigania sana dini ya kiislamu kuenea Machame kuanzia miaka ya 1930’s. Akitokea katika kijiji cha Nkuu, Machame Kirama Muro mtoto wa Muro Mboyo aliyefariki katika miaka ya 1960’s anatambulika kama jemedari wa uislamu Machame.

– Mchagga mwingine aliyeitwa Muro ni moja kati ya watu waliokuwa mashuhuri sana Machame katika miaka ya 1870’s/1880’s katika serikali ya Mangi Ngamini wa Machame akiwa moja kati ya washauri waliokuwa na ushawishi mkubwa. Huyu Muro mashuhuri katika serikali ya Mangi Ngamini alikuwa mmoja kati ya washauri wakuu kwenye ule mgogoro maarufu wa Machame na Kibosho.

– Hata hivyo pamoja na hayo ukoo huu wa Muro unasemekana ni tawi lililotokea kwenye ukoo mkubwa sana katika historia ya wachagga Kilimanjaro, ukoo wa Mboro.

– Ukoo wa Muro umesambaa sana katika vijiji mbalimbali vya Uchagga, Kilimanjaro hususan upande wa magharibi katika eneo la kiko za mto Kikafu, upande wa magharibi na mashariki ya mto Kikafu.

– Ukoo wa Muro unapatikana kwa uchache sana katika kijiji cha Kyuu, Masama.

– Ukoo wa Muro unapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Shari/Uraa, Machame.

– Ukoo wa Muro unapatikana kwa uchache katika kijiji cha Kiselu, Machame.

– Ukoo wa Muro unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Nshara, Machame.

– Ukoo wa Muro unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Uduru, Machame.

– Ukoo wa Muro unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Nkuu Sinde, Machame.

– Ukoo wa Muro unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Nkuu Ndoo, Machame.

– Ukoo wa Muro unapatikana kwa kiasi katika vijiji vya Kata ya Lyamungo, Machame.

Tunaomba msaada wa taarifa zaidi kuhusu ukoo wa Muro ambao unaonekana umesambaa zaidi upande wa Mashariki wa himaya ya Machame. Huu ni ukoo wenye idadi kubwa pia ya waumini wa dini ya kiislamu hivyo pengine una uhusiano wa moja kwa moja na Mzee Kirama Muro aliyetokea kwenye ukoo wa Nkya ambaye ni moja kati ya waanzilishi walioipigania dini ya kiislamu Uchaggani kwa nguvu zote. Pia maeneo ya vijiji ukoo wa Muro unapopatikana kwa wingi sana vya Nkuu, Lyamungo, Uduru na Nshara ndio maeneo ya jirani na nyumbani kwa Mzee Kirama Muro katika kijiji cha Nkuu, Machame aliyekuwa jemedari wa kupambania uislamu Uchaggani na hususan Machame na magharibi ya Machame kwa nguvu zote.

Karibu kwa mchango zaidi wa Mawazo kuhusu ukoo wa Muro.

1. Je, unafahamu nini kuhusiana na ukoo wa Muro?

2. Unafikiri ni kijiji gani ambacho kimesahaulika kutajwa lakini kuna ukoo wa Muro?

3. Kijijini kwenu kuna ukoo wa Muro?

4. Kama wewe ni wa ukoo wa Muro una nini cha kutuambia kuhusu ukoo wenu?

5. Huwa mna maadhimisho yoyote au sherehe za ukoo mwezi gani?

6. Wewe ni Muro wa kutokea kijiji gani?

7. Bado kuna ushirikiano wowote katika matukio mbalimbali muhimu na ndugu zenu wengine wa matawi ya ukoo wa Muro kutoka maeneo mengine ya Uchaggani?

8. Ni tabia gani unazozifahamu za wachagga wa ukoo wa Muro?

9. Wanawake wa ukoo wa Muro huitwaje, na kwa nini?

10. Una rafiki yako yeyote wa kutokea kwenye ukoo wa Muro?

11. Ni watu gani mashuhuri unaowafahamu kutoka kwenye ukoo wa Muro?

12. Kuna mnyama yeyote ambaye labda ni mwiko kuliwa na wachagga wa ukoo wa Muro?

13. Kuna ukoo ambao hawaruhusiwi kuoana na Wako-Muro kwa sababu zilizowahi kuwepo miaka ya zamani au nyingine zozote?

Karibu kwa Mchango zaidi au maswali.

Ahsanteni.

Kesho tutaendelea na ukoo mwingine.

www.wachagga.com

Urithi Wetu Wachagga (Facebook).

Whatsapp +255 754 584 270.

You may also like...

Popular Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *