UKOO WA MUNISHI.

– Munishi ni ukoo maarufu wa wachagga wanaopatikana kwa wingi zaidi maeneo ya magharibi ya kati ya Uchagga, Kilimanjaro. Ukoo wa Munishi ni ukoo mkubwa wenye watu wengi lakini pia wenye utata fulani nyuma yake kutokana na kuhusianishwa na koo nyingine za kichagga zinazoshabihiana nao kwa majina.

– Kuna dhana inayoaminika kwamba kuna uhusiana wa karibu kati ya ukoo wa Munishi na ukoo wa Mushi kwamba Munishi ni tawi lililotokea kwenye ukoo wa Mushi na hilo lilitokana na matukio ya kihistoria yaliyotokea zamani yakapelekea utengano huo. Lakini pia ukoo wa Munishi unahusianishwa na ukoo wa Munisi wa Machame. Inasemekana kwamba ukoo wa Munishi umetokana na ukoo wa Munisi kwamba Munisi inatumika Machame lakini kwa Kibosho unaitwa Munishi ukiwa ni ukoo huo huo mmoja.

– Hata hivyo hizo dhana ni tetesi tu ambazo pengine zimetungwa na watu walioamua kufikiria kwa mfuatano huo wa matamshi ya jina, japo pia kuna uwezekano wa kuwepo kwa mahusiano hayo kwa sababu ya kwamba wachagga na jamii moja na inayofanana kwa mengi. Hivyo uwezekano wa mahusiano ya hivyo bado ni jambo linalowezekana kwani kupata “coincidence” ya namna hiyo nayo ni nadra sana pia. Yote kwa yote tutapenda kufahamu zaidi kutoka kwa wahusika.

– Ukoo wa Munishi umesambaa zaidi katika vijiji vya upande wa magharibi ya kati ya Uchagga, Kilimanjaro ukipatikana kwa wingi katika baadhi ya vijiji hususan vijiji vya Kibosho Magharibi na kwa uchache katika vijiji vingine.

– Ukoo wa Munishi unapatikana kwa uchache katika kijiji cha Usari, Narumu, Machame.

– Ukoo wa Munishi unapatikana kwa uchache katika kijiji cha Orori, Narumu, Machame.

– Ukoo wa Munishi unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Tella, Narumu, Machame.

– Ukoo wa Munishi unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Mulama, Narumu, Machame.

– Ukoo wa Munishi unapatikana kwa wingi sana sana sana katika kijiji cha Manushi Sinde, Kibosho.

– Ukoo wa Munishi unapatikana kwa wingi sana sana katika kijiji cha Manushi Ndoo, Kibosho.

– Ukoo wa Munishi unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Kombo, Kibosho.

– Ukoo wa Munishi unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Umbwe Onana, Kibosho.

– Ukoo wa Munishi unapatikana kwa wingi sana sana katika kijiji cha Kifuni, Kibosho.

– Ukoo wa Munishi unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Kindi Kati, Kibosho.

– Ukoo wa Munishi unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Kindi Muyuni, Kibosho.

– Ukoo wa Munishi unapatikana kwa wingi sana sana katika kijiji cha Kitandu, Kibosho.

– Ukoo wa Munishi unapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Boro, Kibosho.

– Ukoo wa Munishi unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Mweka, Kibosho.

– Ukoo wa Munishi unapatikana kwa kiasi sehemu za Uru pia.

Tunahitaji kufahamu zaidi ukweli juu ya ukoo wa Munishi na koo nyingine ambazo ukoo huu unahusianishwa nazo katika Uchagga, Kilimanjaro. Tunahitaji kuwa na hazina ya maarifa mengi na maudhui ya kutosha juu ya ukoo wa Munishi ili kuongeza katika utafiti na maktaba ya koo za wachagga katika mchakato wa kukuza hamasa itakayopelekea mshikamano zaidi na ari ya kupigania mafanikio makubwa zaidi kwa ngazi za watu binafsi na jamii kwa ujumla.

Karibu kwa mchango zaidi wa Mawazo kuhusu ukoo wa Munishi.

1. Je, unafahamu nini kuhusiana na ukoo wa Munishi?

2. Unafikiri ni kijiji gani ambacho kimesahaulika kutajwa lakini kuna ukoo wa Munishi?

3. Kijijini kwenu kuna ukoo wa Munishi?

4. Kama wewe ni wa ukoo wa Munishi una nini cha kutuambia kuhusu ukoo wenu?

5. Huwa mna maadhimisho yoyote au sherehe za ukoo mwezi gani?

6. Wewe ni Munishi wa kutokea kijiji gani?

7. Bado kuna ushirikiano wowote katika matukio mbalimbali muhimu na ndugu zenu wengine wa matawi ya ukoo wa Munishi kutoka maeneo mengine ya Uchaggani?

8. Ni tabia gani unazozifahamu za wachagga wa ukoo wa Munishi?

9. Wanawake wa ukoo wa Munishi huitwaje, na kwa nini?

10. Una rafiki yako yeyote wa kutokea kwenye ukoo wa Munishi?

11. Ni watu gani mashuhuri unaowafahamu kutoka kwenye ukoo wa Munishi?

12. Kuna mnyama yeyote ambaye labda ni mwiko kuliwa na wachagga wa ukoo wa Munishi?

13. Kuna ukoo ambao hawaruhusiwi kuoana na Wako-Munishi kwa sababu zilizowahi kuwepo miaka ya zamani au nyingine zozote?

Karibu kwa Mchango zaidi au maswali.

Ahsanteni.

Kesho tutaendelea na ukoo mwingine.

www.wachagga.com

Urithi Wetu Wachagga (Facebook).

You may also like...

Popular Posts

1 Comment

  1. Ndugu mwandishi,

    Ni kweli kuna tetesi sana za uwezekano wa mahusiano ya ukoo wa Munishi na koo zingine hasa Mushi na Munisi. Ni imani na masimulizi yaliyojikita sana kwa baadhi ya koo na wazee lakini hata hivyo ni kweli pia kwamba hakuna ushahidi wa moja kwa moja wa mahusiano hayo isipokuwa ni imani zaidi za kufikirika (myths) na maelezo ya kuungaunga ambayo kihistoria kama taaluma, hazina mashiko.

    Labda pia hiyo inaweza kuwa imechangiwa na kwamba ukoo huu wa Munishi hauna historia ndefu sana kiukoo (Kibosho) na hivyo kuwa sababu ya imani hizo. Hata hivyo, kwa mila za kichaga kuna uwezekano wa koo/familia ngeni kuchukua jina linalofanana na ama ukoo uliowakaribisha uchagani au kutumia jina linalofanana na hilo ili nao wawe na mfanano wa kijina na wachaga.

    Kwa hiyo kuna hayo madai pia kwamba Munishi walichukua jina hilo ili kufanana na majina ya kichaga lakini ikiwa pia kuhusianisha na ile taaluma waliyokuwa nayo.

    Ni kweli pia kwamba jina Munishi lina asili ya kumaanisha watu wanaoongoza ibada za matambiko, ishi lina maana ya ardhi au nchi (kwa matamshi ya kikibosho), hivyo, ni ukoo ambao inaonekana kihistoria walikuwa maarufu katika kuongoza ibada za matambiko. Hata hivyo, utata wa hili ni kuwa, ibada hizi zilifanywa zaidi na watu ambao asili yao ilikuwa ni ya hapo, yaani, walifahamika na mizimu ya hilo eneo (kama wachaga walivyoamini zamani hizo). Kwa hili, inamaanisha kuwa Munishi lazima walikuwa na asili ya Kibosho kiasi cha kuaminika kuitwa wenye ardhi (au watu wanaoaminika na mizimu ya eneo).

    Hivyo basi, changamoto ni kubwa sana za kutambua historia sahihi ya ukoo huu, maana wazee waliposimulia asili ya koo za kibosho, Munishi haitajwi, bali zinatajwa koo za Massawe, Kulaya, na Kiwoso. Labda hii itaweza kupelekea kuamini kuwa ukoo huu wa Munishi unaweza kuwa ni tawi la moja ya koo hizo kubwa tatu za asili Kibosho, na hasa Kulaya au Kiwoso ambazo ndizo zinaonekana kuwa na nguvu zaidi katika historia Kibosho.

    Ni kweli kuwa unahitajika utafiti zaidi kupata taarifa zinazoweza kuwa ni sahihi zaidi kuhusiana na ukoo huu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *