UMRI WA MLIMA KILIMANJARO.

UMRI WA MLIMA KILIMANJARO.

Kilimanjaro Ndio Nyumbani, Ndio Makazi Yetu na Ndio Hatma Yetu. Mlima Kilimanjaro Umekuwa Sehemu Muhimu Ya Maisha Yetu, Kutupa Wachagga Uhai na Maana Ya Maisha Yetu Ya Kiroho, Lakini Je, Tunafahamu Mlima Huu Umekuwepo Hapo Moshi Kwa Muda Gani Mpaka Sasa?

Tafiti za Kijiolojia Zinaonyesha Kwamba Mlima Kilimanjaro Umetengenezwa Miaka 5,000,0000 Iliyopita Kutokana na Milipuko wa Volcano Ambayo Ilichukua Miaka Mingi Mpaka Kutengeneza Mlima Mrefu Kama Kilimanjaro.

Katika Vilele Vitatu Vya Mlima Kilimanjaro, Kibo, Mawenzi na Shira Tafiti za Kijiolojia Zinaonyesha Kwamba Mawenzi na Shira Ni Volcano Mfu Ambapo Haiwezi Kulipuka Tena Lakini Kibo Ni Volcano Tuli Kwamba Imetulia Tu Lakini Huenda Ikaja Kulipuka Tena Siku Moja.

Tafiti za Kisayansi Zinaendelea Kuonyesha Kwamba Kilele Cha Shira Kilianza Kutenegenezwa Miaka 2,500,000 Iliyopita na Kwa Mara Ya Mwisho Milipuko Ya Volcano Kwenye Kilele Hiki Cha Shira Ilitokea Miaka 2,000,000 Iliyopita.

Kwa Mujibu wa Tafiti za Kijiolojia Vilele Vya Kibo na Mawenzi Vilianza Kulipuka Kuanzia Miaka 1,000,000 Iliyopita, Yaani Miaka 1,000,000 Mbele Baada Ya Kilele Cha Shira Kutengenezwa. Tafiti Zinaonyesha Kwamba Miamba Yenye Umri Mdogo Zaidi Katika Kilele Cha Mawenzi Ina Umri wa Miaka 500,000, Hivyo Kilele Hiki Cha Mawenzi Kimelipuka Kwa Mara Ya Mwisho Miaka 500,000 Iliyopita.

Tafiti Za Kijiolojia Zinaendelea Kuonyesha Kwamba Milipuko Ya Mwisho Kwenye Kilele Cha Kibo na Kwa Mlima Kilimanjaro Kwa Ujumla Imetokea Miaka 200,000 Iliyopita. Hivyo Kwa Miaka 200,000 Sasa Hakuna Milipuko Yoyote Mikubwa Iliyotokea Katika Mlima Kilimanjaro.

Hata Hivyo Tafiti Zinaonyesha Kwamba Mlima Kilimanjaro Bado Haujatulia Kabisa Kutokana na Kwamba Kilele Cha Kibo Ni Volkano Tuli, Hivyo Huenda Miaka Ya Mbele Ikatokea Milipuko Japo Ni Kwa Kiwango Kidogo.

Urithi Wetu Wachagga

urithiwetuwachagga@gmail.com

You may also like...

Popular Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *