UKOO WA MATERU.

– Materu ni ukoo maarufu wa wachagga unapatikana kwa wingi zaidi eneo la katikati ya Uchagga, Kilimanjaro. Wachagga wa ukoo wa Materu kwa sehemu wamekuwa ni watu wenye haiba ya kupenda dini na maridhiano. Chimbuko la ukoo wa Materu kwa maeneo ya Uchaggani, Kilimanjaro linaweza kuwa ni eneo la Uru mashariki ambapo ukoo wa Materu wanapatikana kwa wingi zaidi.

– Ukoo wa Materu ni moja kati ya zile koo za wachagga ambazo zimekuwa na umashuhuri mkubwa katika eneo fulani kiasi cha kijiji husika kuitwa kwa jina lao ukoo huo. Kijiji cha Materuni, Uru mashariki ni kijiji ambacho ukoo wa Materu unapatikana kwa wingi sana licha ya kwamba ukoo huu umesambaa mpaka kwenye vijiji vingine pia na baadhi kwa wingi pia. Maporomoko maarufu ya maji ya “Mnambe Waterfalls” ni kati ya maeneo maarufu yanayopendwa sana na watalii wa kutoka ndani na nje ya Kilimanjaro na hata nje ya nchi katika kijiji cha Materuni ambacho ni chimbuko la ukoo wa Materu.

– Hata hivyo ukoo wa Materu wameendelea kusambaa zaidi katika maeneo ya vijiji vingine mbalimbali hususan kuelekea mashariki katika maeneo haya ya katikati ya Uchagga, Kilimanjaro ukiwa ni ukoo unaopatikana kwa wingi na kwa uchache katika vijiji mbalimbali.

– Ukoo wa Materu unapatikana kwa uchache katika kijiji cha Kyaseni, Uru.

– Ukoo wa Materu unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Materuni, Uru.

– Ukoo wa Materu unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Korini Kusini, Mbokomu.

– Ukoo wa Materu unapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Korini Juu, Mbokomu.

– Ukoo wa Materu unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Tema, Mbokomu.

– Ukoo wa Materu unapatikana kwa uchache sana katika kijiji cha Mahoma, Old Moshi.

– Ukoo wa Materu unapatikana kwa uchache sana katika kijiji cha Kikarara, Old Moshi.

– Ukoo wa Materu unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Kidia, Old Moshi.

– Ukoo wa Materu unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Shia, Old Moshi.

– Ukoo wa Materu unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Mowo, Old Moshi.

Bado tunahitaji kuendelea kukusanya taarifa zaidi kuhusu ukoo wa Materu na maeneo unakopatikana. Tunahitaji kuwa na maudhui mengi zaidi ya ukoo huu ambao yanaweza kuendelezwa na kupata taarifa zaidi za ukoo kwa faida ya jamii nzima ya ukoo huu kwa kizazi cha sasa na baadaye.

Karibu kwa mchango zaidi wa Mawazo kuhusu ukoo wa Materu.

1. Je, unafahamu nini kuhusiana na ukoo wa Materu?

2. Unafikiri ni kijiji gani ambacho kimesahaulika kutajwa lakini kuna ukoo wa Materu?

3. Kijijini kwenu kuna ukoo wa Materu?

4. Kama wewe ni wa ukoo wa Materu una nini cha kutuambia kuhusu ukoo wenu?

5. Huwa mna maadhimisho yoyote au sherehe za ukoo mwezi gani?

6. Wewe ni Materu wa kutokea kijiji gani?

7. Bado kuna ushirikiano wowote katika matukio mbalimbali muhimu na ndugu zenu wengine wa matawi ya ukoo wa Materu kutoka maeneo mengine ya Uchaggani?

8. Ni tabia gani unazozifahamu za wachagga wa ukoo wa Materu?

9. Wanawake wa ukoo wa Materu huitwaje, na kwa nini?

10. Una rafiki yako yeyote wa kutokea kwenye ukoo wa Materu?

11. Ni watu gani mashuhuri unaowafahamu kutoka kwenye ukoo wa Materu?

12. Kuna mnyama yeyote ambaye labda ni mwiko kuliwa na wachagga wa ukoo wa Materu?

13. Kuna ukoo ambao hawaruhusiwi kuoana na Wako-Materu kwa sababu zilizowahi kuwepo miaka ya zamani au nyingine zozote?

Karibu kwa Mchango zaidi au maswali.

Ahsanteni.

Kesho tutaendelea na ukoo mwingine.

www.wachagga.com

Urithi Wetu Wachagga (Facebook).

Whatsapp +255 754 584 270.

You may also like...

Popular Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *