UKOO WA KESSY.

– Kessy/Kessi/Kesi ni ukoo mashuhuri sana wa wachagga wenye historia inayokwenda karibu miaka 400 iliyopita ukiongezeka vizazi na vizazi mpaka sasa ambapo umekuwa ni ukoo mkubwa uliosambaa katika vijiji vingi sana Kilimanjaro. Wachagga wa ukoo wa Kessy wamekuwa wakifanya vizuri katika nyanja mbalimbali za kimaisha katika maeneo mbalimbali ndani na nje ya Kilimanjaro na hata nje ya nchi.

– Kutoka kwenye historia chimbuko la ukoo wa Kessy inasemekana ni katika kijiji cha Yamu, Kirua Vunjo ambapo mtawala Kessy mtoto wa Msanja ndiye mwanzilishi wake upande wa magharibi wa himaya ya Kirua Vunjo. Ukoo wa huu ulisambaa sana maeneo ya Kirua Vunjo mashariki na magharibi kadiri ulivyopata nguvu zaidi kiutawala na mali zaidi. Ni ukoo ulioongezeka kwa kasi sana kwa idadi ya watu kadiri utajiri wao ulivyoendelea kukua.

– Kutokea maeneo ya himaya ya umangi Kirua Vunjo ukoo wa Kessy uliendelea kusambaa upande wa magharibi na mashariki ya Uchagga katika vijiji vingine vingi sana. Hivyo ukoo huu umeendelea kukua na kuongezeka sana idadi ya watu ukipatikana zaidi maeneo ya katikati na mashariki ya Uchaggani, Kilimanjaro.

– Hivyo ukoo wa Kessy unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Mruwia na Materuni, Uru.

– Ukoo wa Kessy unapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Mwasi Kusini, Uru.

– Ukoo wa Kessy unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Kishumundu, Uru.

– Ukoo wa Kessy unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Mahoma, Old Moshi.

– Ukoo wa Kessy unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Mdawi, Old Moshi.

– Ukoo wa Kessy unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Shia, Old Moshi.

– Ukoo wa Kessy unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Sango Old Moshi.

– Ukoo wa Kessy unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Yamu, Kirua Vunjo.

– Ukoo wa Kessy wanapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Uparo, Kirua Vunjo.

– Ukoo wa Kessy wanapatikana kwa wingi katika kijiji cha Mrumeni, Kirua Vunjo.

– Ukoo wa Kessy wanapatikana kwa wingi katika kijiji cha Nduoni, Kirua Vunjo.

– Ukoo wa Kessy unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Kanango, Kirua Vunjo.

– Ukoo wa Kessy unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Kwamare, Kirua Vunjo.

– Ukoo wa Kessy unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Iwa, Kirua Vunjo.

– Ukoo wa Kessy unapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Kanji, Kirua Vunjo.

– Ukoo wa Kessy unapatikana kwa wingi sana sana katika kijiji cha Manu, Kirua Vunjo.

– Ukoo wa Kessy unapatikana katika kijiji cha Pofo, Kilema.

– Ukoo wa Kessy unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Masaera, Kilema.

– Ukoo wa Kessy unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Kilema chini, Kilema.

– Ukoo wa Kessy unapatikana katika kijiji cha Ngangu, Kilema.

– Ukoo wa Kessy unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Kyou, Kilema.

– Ukoo wa Kessy unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Ruwa, Kilema.

– Ukoo wa Kessy wanapatikana kwa wingi katika kijiji cha Makami Juu, Kilema.

– Ukoo wa Kessy unapatikana katika kijiji cha Kyura, Kilema.

– Ukoo wa Kessy wanapatikana kwa wingi katika kijiji cha Kyala, Marangu.

– Ukoo wa Kessi wanapatikana kwa wingi katika kijiji cha Lyamrakana, Marangu.

– Ukoo wa Kessy wanapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Lyasomboro, Marangu.

– Ukoo wa Kessy wanapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Mmbahe, Marangu.

– Ukoo wa Kessy wanapatikana kidogo sana katika kijiji cha Komalyangoe, Marangu.

– Ukoo wa Kessy unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Komela, Marangu.

– Ukoo wa Kessy wanapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Nduweni, Marangu.

– Ukoo wa Kessy wanapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Kimbogho, Mamba.

– Ukoo wa Kessy wanapatikana kidogo katika kijiji cha Mkolowony, Mamba.

– Ukoo wa Kessy wanapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Kimangaro, Mwika.

– Ukoo wa Kessy unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Leto, Usseri, Rombo.

Tunahitaji taarifa zaidi kuhusu ukoo wa Kessy ambao umesambaa sana Uchaggani, ili kuongezea katika maudhui ya ukoo huu na maudhui ya koo za wachagga kwa ujumla katika utafiti unaoendelea kufanyika. Lengo la maarifa haya ni kujenga jamii yenye kujitambua na yenye mshikamano katika kujenga hamasa kuelekea kufanya makubwa kwa ngazi ya mtu mmoja mmoja na ngazi ya koo kwa ujumla.

Karibu kwa mchango zaidi wa Mawazo kuhusu ukoo wa Kessy.

1. Je, unafahamu nini kuhusiana na ukoo wa Kessy?

2. Unafikiri ni kijiji gani ambacho kimesahaulika kutajwa lakini kuna ukoo wa Kessy?

3. Kijijini kwenu kuna ukoo wa Kessy?

4. Kama wewe ni wa ukoo wa Kessy una nini cha kutuambia kuhusu ukoo wenu?

5. Huwa mna maadhimisho yoyote au sherehe za ukoo mwezi gani?

6. Wewe ni Kessy wa kutokea kijiji gani?

7. Bado kuna ushirikiano wowote katika matukio mbalimbali muhimu na ndugu zenu wengine wa matawi ya ukoo wa Kessy kutoka maeneo mengine ya Uchaggani?

8. Ni tabia gani unazozifahamu za wachagga wa ukoo wa Kessy?

9. Wanawake wa ukoo wa Kessy huitwaje, na kwa nini?

10. Una rafiki yako yeyote wa kutokea kwenye ukoo wa Kessy?

11. Ni watu gani mashuhuri unaowafahamu kutoka kwenye ukoo wa Kessy?

12. Kuna mnyama yeyote ambaye labda ni mwiko kuliwa na wachagga wa ukoo wa Kessy?

13. Kuna ukoo ambao hawaruhusiwi kuoana na Wako-Kessy kwa sababu zilizowahi kuwepo miaka ya zamani au nyingine zozote?

Karibu kwa Mchango zaidi au maswali.

Ahsanteni.

Kesho tutaendelea na ukoo mwingine.

Whatsapp +255 754 584 270.

You may also like...

Popular Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *