UKOO WA MINJA.

– Minja ni ukoo mkubwa sana wa wachagga waliosambaa katika vijiji na maeneo mbalimbali ya Uchagga, Kilimanjaro. Ukoo wa Minja umetoa wachagga wengi mashuhuri katika nyanja mbalimbali kuanzia watumishi wa umma, wanasiasa, wafanyabiashara, maprofesa wa vyuo vikuu na wajasiriamali wengi sana wa ngazi mbalimbali. Ni ukoo wa wachagga wengi wenye kujituma sana na kuna ambao wana mafanikio makubwa.

– Kutoka kwenye historia Minja anatajwa katika vita ya utawala ambapo kutokea Kirua Vunjo alikuja kumsaidia Makishingo kumwongezea nguvu dhidi ya Lyimo katika utawala wa vijiji vya ukanda wa juu Marangu. Kwa msaada huo Makisingo wa maeneo ya vijiji vya Mmbahe alifanikiwa kumdhibiti Lyimo akalipa kisasi na kurudisha mifugo yake yote iliyokuwa imechukuliwa kwa nguvu.

– Hivyo Minja anatajwa kama mtu au ukoo uliokuwa una koloni kubwa maeneo ya Kirua Vunjo. Hata hivyo ukoo wa Minja wameendelea kusambaa na wanapatikana maeneo ya vijiji vingi vya Uchagga kuanzia katikati ya Uchagga mpaka mashariki.

– Hivyo ukoo wa Minja wanapatikana kwa kiasi kwenye baadhi ya vijiji Uru.

– Ukoo wa Minja wa Minja wanapatikana wa wingi kiasi katika kijiji cha Mrumeni, Kirua Vunjo.

– Ukoo wa Minja wanapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Iwa, Kirua Vunjo.

– Ukoo wa Minja wanapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Legho, Kirua Vunjo.

– Ukoo wa Minja wanapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Mkyashi, Kilema.

– Ukoo wa Minja wanapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Kilema chini, Kilema.

– Ukoo wa Minja wanapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Pofo, Kilema.

– Ukoo wa Minja wanapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Samanga, Marangu.

– Ukoo wa Minja wanapatikana kwa wingi sana sana katika kijiji cha Lyasomboro, Marangu.

– Ukoo wa Minja wanapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Mmbahe, Marangu.

– Ukoo wa Minja wanapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Komela, Marangu.

– Ukoo wa Minja wanapatikana kwa wingi sana sana katika kijiji cha Komalyangoe, Marangu.

– Ukoo wa Minja wanapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Kiraracha, Marangu.

– Ukoo wa Minja wanapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Nduweni, Marangu.

– Ukoo wa Minja wanapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Kyala, Marangu.

– Ukoo wa Minja wanapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Mkolowony, Mamba.

– Ukoo wa Minja wanapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Kotela, Mamba.

– Ukoo wa Minja wanapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Mboni, Mamba.

– Ukoo wa Minja wanapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Masia, Mamba.

– Ukoo wa Minja wanapatikana kwa wingi sehemu za Ugweno pia.

Ukoo wa Minja ni ukoo mkubwa sana na wenye watu wengi mashuhuri lakini hauonyeshi kuwa na taarifa nyingi sana kutoka katika historia hivyo tunahitaji taarifa nyingi zaidi ili kuongeza kwenye maudhui ya ukoo huu na koo za wachagga kwa ujumla kwa faida ya kizazi cha sasa na baadaye. Taarifa hizi pia zinachangia katika kuongeza hamasa kwenye kujituma na kuleta mshikamano baina ya wanaukoo kuelekea kufanya makubwa kwa ngazi ya mtu mmoja mmoja na ngazi ya ukoo.

Karibu kwa mchango zaidi wa Mawazo kuhusu ukoo wa Minja.

1. Je, unafahamu nini kuhusiana na ukoo wa Minja?

2. Unafikiri ni kijiji gani ambacho kimesahaulika kutajwa lakini kuna ukoo wa Minja?

3. Kijijini kwenu kuna ukoo wa Minja?

4. Kama wewe ni wa ukoo wa Minja una nini cha kutuambia kuhusu ukoo wenu?

5. Huwa mna maadhimisho yoyote au sherehe za ukoo mwezi gani?

6. Wewe ni Minja wa kutokea kijiji gani?

7. Bado kuna ushirikiano wowote katika matukio mbalimbali muhimu na ndugu zenu wengine wa matawi ya ukoo wa Minja kutoka maeneo mengine ya Uchaggani?

8. Ni tabia gani unazozifahamu za wachagga wa ukoo wa Minja?

9. Wanawake wa ukoo wa Minja huitwaje, na kwa nini?

10. Una rafiki yako yeyote wa kutokea kwenye ukoo wa Minja?

11. Ni watu gani mashuhuri unaowafahamu kutoka kwenye ukoo wa Minja?

12. Kuna mnyama yeyote ambaye labda ni mwiko kuliwa na wachagga wa ukoo wa Minja?

13. Kuna ukoo ambao hawaruhusiwi kuoana na Wako-Minja kwa sababu zilizowahi kuwepo miaka ya zamani au nyingine zozote?

Karibu kwa Mchango zaidi au maswali.

Ahsanteni.

Kesho tutaendelea na ukoo mwingine.

Whatsapp +255 754 584 270.

You may also like...

Popular Posts

3 Comments

  1. Arthur A.Assenga says:

    Tunahitaji kujua kwa nini wachagga wanajiita wamarangu na marangu ni tarafa iko kwenye jimbo la Vunjo?

    1. Nani amekwambia wachagga wanajiita wamarangu?

      Wachagga wanajiita wachagga, Marangu ni moja kati ya maeneo wanakotokea wachagga.

  2. PROSPER PAUL MALLY says:

    Wamarangu tupo kweli ni sawa na wakobosho , wamachame ,wa rombo kwaiyo inamaanisha wachaga wanaotokea eleo flani

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *