UKOO WA MOSI.

– Ukoo wa Mosi ni ukoo unaopatikana katika himaya ya umangi Siha/Sanya Juu. Hakuna taarifa nyingi juu ya chimbuko la ukoo huu wala uelewa zaidi kama laba ni tawi la ukoo mwingine mkubwa unaojulikana zaidi.

– Hata hivyo ukoo wa Mosi ni ukoo wa watu makini na wapambanaji pia. Tumekutana na watu kadhaa wenye uwezo mkubwa kutoka ukoo wa Mosi licha ya kwamba sio ukoo wenye idadi kubwa ya watu. Tunaweza kusaidiana taarifa zaidi juu ya vijiji ambavyo ukoo wa Mosi unapatikana kwa wingi na sifa zao.

Tunahitaji mchango wa mawazo zaidi juu ya ukoo huu Mosi ambao ni mkongwe sana magharibi ya Kilimanjaro.

1. Je, unafahamu nini kuhusiana na ukoo wa Mosi?

2. Kijijini kwenu kuna ukoo wa Mosi?

3. Kama wewe ni wa ukoo wa Mosi una nini cha kutuambia kuhusu ukoo wenu? Huwa mna maadhimisho yoyote au sherehe za ukoo mwezi gani?

4. Bado kuna ushirikiano wowote katika matukio mbalimbali muhimu na ndugu zenu wengine wa matawi ya ukoo huo kutoka maeneo mengine ya Uchaggani?

5. Ni tabia gani unazozifahamu za wachagga wa ukoo wa Mosi?

6. Wanawake wa ukoo wa Mosi huitwaje?

7. Una rafiki yako yeyote wa ukoo wa Mosi?

8. Watu gani mashuhuri unaowafahamu kutoka kwenye ukoo wa Mosi?

Karibu kwa Maoni na Maswali.

Kesho tutaendelea na ukoo mwingine.

Whatsapp +255 754 584 270

You may also like...

Popular Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *